Assallaam Alleykum Ankal

Ankal nakuomba sana nipostie hii habari yangu ili wadau waweze nisaidia jambo hili.
Kwanza kabisa nakushukuru sana kwa kutujuza habari za nyumbani,Mwenyezi Mungu akuzidishie maisha marefu yenye Afya tele!Uzidi kuhabarisha kama kawa.

Hoja yangu ni hivi,,,Baada ya wiki moja toka leo,nataraji kufanya mtihani wa kumaliza masomo yangu huku ughaibuni.

Sasa tumeambiwa kila mwanafunzi aelezee kitu chochote kuhusu nchi yake,na mimi bila hiyana nikachagua kuielezea nchi yangu kwa kuipamba pamba kwa mbuga za wanyama,Mlima Kilimanjaro,na Meru pia,Mito na Maziwa..

Maswali yangu kwa Wadau ni kama Ifuatavyo,,Tafadhali kama kuna mtu yeyote anajuwa,kati ya mambo haya,basi anisaidie ili nami ndugu yenu nisiweze kutoka na buyu ka pepa hilo.-

Mbuga za wanyama ziko ngapi?na ikiwezekana mnitajie kwa majina.
Mito na maziwa ni vingapi na majina yake
Kama kuna mtu yeyote anaweza kujuwa makabila ya Tanzania mangapi?
Mikoa ni mingapi?
Na wilaya pia ngapi?
Na Burudi na Rwanda walishaingia katika umoja wa Africa mashariki? kwa hiyo ni nchi 5?
Na la mwisho,Tanzania iliingia Mwaka gani katika mfumo wa vyama vingi?,na Nation service ilisitishwa mwaka gani?

Nitashukuru wadau kama mkinipa majibu mazuri ili nikajieleze mbele ya kadamnasi kuhusu nchi Yangu.

Ahlam UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. Usiwe mvivu. Ulaya internent ni bwelele. Ingia kwenye mtandao utapata kila kitu. Ninavyokuona unakaribia kumaliza shule lakini haujapata taaluma inayotakiwa. Kama hauwezi kupata hizi taarifa mwenyewe, nakushauri uongeze mwaka mbele ili akili ipanuke kidogo. Maana naona kama bado akili yako ni kama ya mwanafunzi wa CHEKECHEA.

    ReplyDelete
  2. Samahani mkuu, lakini kama unataka kuandikia Tanzania kwa mambo usiyoyajua na pepa ni leo u r bound to fail big time!

    Ni kipi sasa unakifahamu kuhusu Tanzania? Rais wa bongo unamjua anaitwa nani kwa sasa? Mji mkuu je? Mipaka ya Tanzania vp? Du!

    ReplyDelete
  3. Mimi nadhani hawa watu wanakutumia kufanya Ujasusi kwenye nchi yako mwenyewe...!!Mdau-USA

    ReplyDelete
  4. Maswali yako mengi ni ya darasa la nne na sekondari. Mbuga za wanyama kuna Mikumi, serengeti, lake manyara na ngorongoro, katavi na Ruaha nationa parks.

    Kuna ziwa Victoria kanda ya ziwa, ziwa nyasa kanda ya kusini, ziwa Tanganyika kanda ya magharibi. Mito kuna mto Ruvu, malagarasi, wami etc etc....


    Makabila yako 124 etc etc.....info nyingine tumia akili kutafuta Ubalozini au kwenye website ndugu acha kupenda dezo.


    Mikoa 28 au 30 I think na hii iliyoongezwa juzi. Wilaya za kumwaga nenda Tamisemi website hizi info ziko wazi kijana...eheee unaijua katiba kweli kama uko mtupu hizi kwenye nchi yako.


    Burundi na Rwanda wako EAC na ndio kuna nchi 5



    Tanzania iliingia kwenye ruzuku 1992. Usiulize maswali ka mlevi wa chua pale kibololoni.


    National serv ilisitishwa mwaka 1993 not sure on this one...tafuta mwenyewe ustaadhi maana we madrasa tu...


    Mpilipili
    1600 Pennyslvania ave

    ReplyDelete
  5. Ushafeli, sijui utawaeleza nini kijijini kwenu ukirejea. Uwarejeshee na pesa zao.

    Cheki kwenye neti ndugu yangu, kuna kila kitu mbona. Usisahau kuongelea "The Cradle of Mankind" (Olduvai Gorge, a UNESCO Heritage Site) na Msitu wa Gombe (Dr. Jane Goodall's research center for chimpanzees), Selous Game Reserve (one of the largest faunal reserves in the world, Africa's largest protected area uninhabited by man, where Tanzania's greatest population of elephants wander in an area bigger than Switzerland, also a World Heritage Site), na Tanzanite (pia uwaambie haitufaidishi lolote Watanzania). Waambie pia yale machimbo ya mafuta yaliyoahirishwa kwa muda mrefu sasa yameanza, hivyo kiama cha Tanzania kimewadia.

    Ila kwa habari ya idadi ya mikoa na wilaya, japo nasikia aibu sana kulisema hili, angalia websites za CIA na BBC. Website ya serikali hawaja-update bado na ndio wanaobadilisha namba za wilaya na mikoa. Website haipo up-to-date na pia mbayaaaaa!

    ReplyDelete
  6. ni kweli mdau hapo juu kanena. maana jamaa hawezi kuuliza maswali haya madogo madogo tu wakati yeye yupo ulaya na internet kibao tu, alafu yeye muda wake wa kufanya research anautumiaje? yaani sisi tumlaisishie tu wakati yeye uwezo wa kufanya anao. kuuliza si ujinga lakini hili limezidi. kama hana internet aje Tottenham Hale nyumbani kwangu nitamsaidia. tena bure na coffee au Chai na maandazi atatayarishiwa na mke wangu. Mdau UK pia.

    ReplyDelete
  7. mimi nipo UK kama unataka msaada basi mi naweza kukusaidia kukuandikia ripoti fupi. Kwani wewe UK uko sehemu gani.

    Kama unaona shida sana, basi nenda ubalozi tanzania watakupata data zote za vitu ambavyoumevitaja hapo juu.

    Mdau wa Stratford

    ReplyDelete
  8. Ndo yale ya kumshika Ng'ombe mapembe, halafu unauliza macho yake yako wapi. Kwa maswali hayo, sijuwi hilo 'pepa' la huko ughaibuni umelipepetuwa vipi.

    ReplyDelete
  9. Dada/kaka kama alivyosema mwenzangu hapo juu, tumia internet , computer knows everything, wewe iulize tu maswali mafupi mafupi inaji bila wasiwasi.

    ReplyDelete
  10. Kwakweli mm pia nimeshindwa kumuelewa huyu mtu!kha!hivyo vitu anavyouliza vinapatikana kwenye mitandao.Huyu wa wapi huyu!

    ReplyDelete
  11. Nilitaka kusema hivyo vivyo kama jamaa wa saa Tue Feb 21, 11:50:00 PM 2012 alivyosema bila kebei lakini. Jamaa unatakiwa kufanya research na siyo watu humu kwenye mtandao wa kufanyie, halafu wewe upate grade ya bure.

    ReplyDelete
  12. I agree with the previous speaker. All this info is available on the internet. Go to the Tanzania national website and you will get 60% of the information: http://www.tanzania.go.tz/

    ReplyDelete
  13. uvivu kupenda kufanyiwa kila kitu........kwani unadhani internet ina kazi gani kama info kama hizo upewe

    ReplyDelete
  14. ...fungua hapa www.tanzaniaparks.com utaona info kuhusu mbuga za wanyama pia ziko 15na kuhusu Tanzania jaribu kusearch google na wikipedia nadhani huko utapata zaidi. Sikuhizi mtandaoni unapata ujumbe zaidi kuliko kwa mtu binafsi.

    ReplyDelete
  15. Soma kijana acha uvivu.

    David V

    ReplyDelete
  16. So you want somebody to do all the research for you and you get the diploma....do your homework or find another topic.

    ReplyDelete
  17. DUh bwana kweli na mimi nilitaka niseme hivyo hivyo huyu jamaa aibu tupu halafu watu kama hawa wakirudi bongo eti TRA wanawakamatia kama malaika wa bwana au hata akiamua kujiunga na polisi basi ataanzia na cheyo cha juu kisa kasomea UK, na akiongea na kizungu chake cha marembo -mama yangu wee, wake za watu hapo si kupapatika , Msomi !!! kumbe kopo tupu- wewe kama ni kufeli ni halali yako kabisaaa nenda kabebe mabox tu huko huko au dish washer, eti maziwa yako mangapi bongo !! kwani la msingi ulisomea wapi ?? na huko umefikafika vipi ?? siyo soroway ?? . Zebedayo wa Zebedayo.

    ReplyDelete
  18. ..we dogo ni bogus sana..i have never seen b4..hayo maswali hata ukimuuliza mzungu huko atakujibu..we ni mtanzania kweli? if u dont know uaself what else do u know..na umesha feli nakuambia..achana na hyo makitu..andika kuhusu night clubs

    ReplyDelete
  19. Mbona hayo mambo yalikua yanafundishwa toaka tupo shule ya msingi au ulipitishwa tuuu

    ReplyDelete
  20. Visit the Tanzania Tourist Board website utapata info. kibao.

    ReplyDelete
  21. Hata mtandao wa serikali yako huujui, una haja gani sasa ya kuandika kuhusu Bongo tena?

    ReplyDelete
  22. mie nipo tofauti kidogo,kama unaweza kupata mawasiliano na watu husika la sivyo humu utapata majibu ya kuudhi,hebu ulizia idara sahihi otherwise utachemsha kwani hakuna anaekaa darasani kujifunza aina ya makabila

    ReplyDelete
  23. Duu uko huko lakin mtandao haujakukomboa eeeh...unataka utafuniweee kila ki2...utapata shida maishani....just google....unash ngapi?...maana hata huku kwetu kuuliza sh 100,kuelekezwa sh 150,kupelekwa sh. 200

    ReplyDelete
  24. bado sipati picha unasomea kitu gani na kwa level ipi?!?!?

    ReplyDelete
  25. Nakubaliana na Anon hapo huu. Unatia aibu wewe, maswali gani haya unauliza ya kichekechea. google that s**t!

    ReplyDelete
  26. Alaykum Salaam,

    Mdau mwenzetu Ahlam wa UK.


    AHSANTE SANA!

    Ninachoweza kukuchangia ni Mambo Mawili 'NYETI' hapa chini:

    1.Andika ktk Project yako kuwa,licha ya nchi yetu kujaaliwa kwa Rasilimali zote hizo ulizozitaja japo ingawa kwa uchache,MADINI,almasi,dhahabu,chuma,bati,gesi,mafuta karibuni tutapata,urani,makaa ya mawe,tanzanite,ribu,n.k.,BAHARI,MAZIWA YA MAJI YOTE MAKUBWA AFRIKA TUNAYO,MISITU,WANYAMA PORI,ARDHI,....INASIKITISHA SANA TUNA TATIZO KUBWA LA MGAWANYIKO WA RASILIMALI NA UTAJIRI HUU...CHINI YA 5% YA WATANZANIA WANANUFAIKA NA FAIDA YA UTAJIRI HUU NA ZAIDI YA 95% YA WATANZANIA NI MASIKINI WAKUTUPWA!...HILI NI TATIZO KUBWA KTK MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII YETU NA DUNIA KWA UJUMLA.....(((((*****TAFADHALI SIPO KATIKA SIASA NIPO KATIKA UHALISIA WA TATIZO*****))))) MFICHA MARADHI UMAUTI HUMUUMBUA!

    2.NATIONAL SERVICE ilisitishwa mwaka 1994 na hii imetuletea matatizo makubwa sana Nchini Mfano:-

    -Wakati ilipokuwepo kiwango cha Uhalifu kilikuwa chini sana,
    -Wakati ilipokuwepo hatukuwa na Vijana Mateja,Wapiga debe,Matapeli,Mashoga na Wasichana Machangu.
    -Ilipokuwepo hakukuwa na kuanguka kwa Maadili ya Jamii kwa kiasi tulicho fikia sasa.

    -Kwa kuwa kutolewa kwake NATIONAL SERVICE kumeagusha KIWANGO CHA KUJITAMBUA,KUJITUMA UTAIFA NA UZALENDO!

    ReplyDelete
  27. Ningekuwa namfahamu mwalimu wako huko ughaibuni, ningemwambia akupe SIFURI... Yaani umekosa hata AKILI YA KUGUGO!!!!! AArrrggghhhhhh...

    Chiggs, Deslam.

    ReplyDelete
  28. Just Google...

    ReplyDelete
  29. 100% confidence levelFebruary 22, 2012

    Huyu mdau sidhani kama ni mwanafunzi wa masomo ya darasani mfumo maalum.[Formal education].Kwa sababu kama ni mwanafunzi wa mfumo maalum na umekuwa ukijifunza kwa njia mbalimbali,taarifa unazozitaka usinge washirikisha wadau wakusaidie kwani ungekuwa unazielewa toka hujaenda huko uliko.
    Unless ungeweka wazi kama ni mwanafunzi wa taaluma zisizo fomal ambazo kuelewa na kujishughulisha na kufahamu taarifa unazozitafuta ni jambo la kushurutishwa kama ilivyotokea kwako sasa hivi.
    Anyway ngoja tukusaidie.
    1.Mbuga check link hii http://www.tanzaniaparks.com/
    2.Mito na maziwa check na http://www.africanmeccasafaris.com/tanzania/guide/tanzaniawatersource.asp
    3.Makabila check na http://www.africanheart.com/information/tribes_tanzania.htm
    4.Mikoa kumbuka kuongeza Mkoa wa Katavi na wilaya check na http://statoids.com/utz.html,pamoja na http://www.nbs.go.tz/takwimu/references/Tanzania_in_Figures2010.pdf
    5.Kuhusu Rwanda na Burundi kuwa member states wa EAC jibu ni ndiyo.Evidence check na http://www.eac.int/home.html
    6.Mfumo wa vyama vingi Tanzania uliingia mwaka 1992 na kushirikisha vyama vingi kwenye uchaguzi wa mwaka 1995.
    Asante mdau Ahlam

    ReplyDelete
  30. Hivi wewe nu mwanafunzi kweli? inaonekana wewe ni kilaza wa kutubwa na hilo buyu ni stahiki yako maana ulisoma tanzania wewe au nyie ndio mnatumia vyeti vya ndugu zenu au hata watu hamuawajui kupata vyuo ulaya kisa wazazi wenu wana uwezo. Nilikasirika hapo mwanzo ila sasa nahisi nakuonea huruma kwa ujinga uliokuwa nao. haya yote yapo kwenye mitandao ni uvivu na ukilaza ndio unakusumbua, GROW UP!!!!!!!!!! Nyie ndio mkirudi huku eti Tanzania hakuna kitu kwa lipi hili la kutojua chochote kuhusu nchi yako? hivi umefaulu kweli wewe? Umeniharibia siku yangu kabisa

    Mdau Mtanzania Asilia

    ReplyDelete
  31. Inavyoonekana wewe sio mtanzania, yaani hujui hata nchi yako????. Rudi tu Tanzania ukaanze kusoma chekechea. la sivyo utueleze ukweli utaifa wako, ili tunapokusaidia tujue tunamsaidia mgeni. Sio mtanzania weweeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  32. acha ukilaza wewe sasa utafanyaje mtihani endapo unashindwa kuingia google na kusearch mambo ya tanzania mbona yako wazi kabisa? maswali haya ni ya jiografia mwanafunzi wa darasa la nne.

    ReplyDelete
  33. Bendera, bendera yetu nchini ina rangi nne x 2. ya kwanza kijani mimea yetu, ya pili buluu, bahari yetu, ya tatu manjano madini yetu ya nne nyeusi sisi wenyewe!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  34. Ahlam fuata ushaur wa wadau hapo juu, tupilia kebehi zao, na ingia ktk research, hopful utafanikiwa

    -mdau, bongonyoso

    ReplyDelete
  35. What an idiot!!mtanzania usiyeweza jua vitu vya nchi yako basi andika kuhusu huko unakopiga box,ili uki fail useme sio nchi yako,unatutia shaka na shule yako kma unamaliza soon!!

    ReplyDelete
  36. HUYU AKIMALIZA ANAKUJA TANZANIA KUWA WAZIRI, MNATEGEMEA NINI?

    ReplyDelete
  37. asante mdau uliyemjibu muuliza swali na ukamjibu ipasavyo ubarikiwe sana unajua wengine wanamshambulia huyu aliyeuliza haya maswali sio ajabu baadhi yao hawajui hata kitu kuhusu nchi yao lakini wanakuwa wakwanza kushambulia mwenzao na kumkashfu kana kwamba wao wanajua kila kitu kama hujui hili unajua lile kwa hiyo wt wenzangu tujaribu tu kupendana km asili yetu ilivyo tumjibu mtu kufuatanan na jinsi alivyo uliza swali lake sio kushambulia na maneno mbovumbovu mimi mwenyewe ninayeandika hapa nilikuwa sijui kuhusu haya mambo huyu mdau aliye mjibu vizuri muuliza swali hata mimi nimefaidika maana ilikuwa sijui mambo mengi kuhusu tz japo nina kihelimu kidogo cha kunifuta ujinga jamani tupendane kama mtu hajui cha kujibu akae kimya tu kuliko kujibu utmbo tusiwe kama majirani zetu wazio pendana au wameshawaambukiza huo ugonjwa wao waubaguzi hawapendani pls tuache mara moja hii tabia tuna sifika ulimwenguni kote kwa upendo japo sio kiivyo

    ReplyDelete
  38. NAKUSHUKURUNI SANA TENA SANA,KWA MAJIBU MAZURI MLIYONIPA,HASA WALIOPOTEZA MUDA WAO KWA KUNIANDIKIA MANENO MAZURI YA KUNIELEWESHA,NA JINSI NITAKAVYOJIELEZA KUHUSU NCHI YANGU.INSHA'ALLAH NITAFANYA HIVYO

    NAKUSHUKURU SANA MPILIPILI,KWA MAELEZO MAZURI SANA,,UBARIKIWE MNO,,INGAWA UMENIJIBU NA VIGONGO JUU,,NI KWELI MTAKA CHA UVUNGUNI,,

    MDAU Wed Feb 22,12:42:00am
    AHSANTE SANA KWA MAJIBU MAZURI ULIYONIPA,AMA KWELI UMENIKUMBUSHA MAMBO MENGI YA KUZUNGUMZIA AMBAYO ISINGEKUWA RAHISI KUYAKUMBUKA.

    MDAU ULIYESEMA KUHUSU BENDERA NAKUSHUKURU PIA KWA HILO
    MDAU BONGONYOSO NASHUKURU SANA KWA KUNIPA MOYO,KWELI UKITAKA KUJUWA ACHANA NA KEBEHI ZA WENYE MIDOMO MIREFU.UKISIKILIZA YA WATU HUWEZI KUFANYA CHOCHOTE!

    MDAU WA Wed 22,09:08:00am
    NAKUSHUKURU SANA,KWA COMMENT YAKO NZURI SANA,NI KWELI KATIKA ASILIMALI TULIYOKUWA NAYO TANZANIA,SISI WAZALENDO HATUNA MANUFAA NAYO,NI KWELI HIYO 5% PEKE YAKE NDO WANAKULA MATUNDA YA UTAJIRI WA NCHI NZIMA,,MIMI NI MIONGONI MWA WAZALENDO WA HALI YA CHINI SANA,NA NAZUNGUMZIA KUHUSU NCHI YANGU NA LASILIMALI ZAKE SI KWA KUWA NAFAIDI NO!NI KWA SABABU NI NCHI YANGU,NA NAJUWA WAZI TUNAISHI NDIO BONGO LAKINI CHA MOTO TUNAKIONA.INGAWA WADAU WENGINE MMECHANGIA KWA KUSEMA NIMEKUJA HUKU,KWA VYETI VYA KUFORGE,MARA ETI SIJASOMA PRIMARY HOME,,JAMANI MANENO MENGI YA NINI!MIMI NI MZALENDO WA KAWAIDA TU,SINA NDUGU SERIKALINI,NIKO KIVYANGU VYANGU,NI MDADA WA KIJIWENI TU,NA SINA HAJA YA KUWA WAZIRI,KWANI HUYO ALIYEPO NDO NAMUONA BORA KATI YA MAWAZIRI WOTE NILIYO WAHI KUWAFAHAMU(NINA MAANA WAZIRI PINDA NI PERFECT PERSON KUWEPO HAPO).MIMI NAFANYA MAMBO YANGU MWENYEWE NA WALALA HOI WENZANGU,HASA SHUGHLI ZA KIJAMII.YANINI KUPEWA CHEO UKABAKIA WANANCHI WANAKULAANI,SI BORA NIJIFANYIE SHUGHLI ZANGU KAMA ANKAL MICHUZI ANAVYOITUMIKIA JAMII,,ANAEMJUWA NA ASIYEMJUWA WOTE TU ANAWASAIDIA,KAMA ALIVYONISAIDIA MIMI KUNITOLEA HABARI YANGU HII NIKASAIDIWA KWA KIASI KIKUBWA TU.NA UNAFIKIRI MUNGU ATAMLIPA MANGAPI KWA MSAADA WA HABARI ZAKE NA WATU WAKASAIDIWA HATA ZAIDI YANGU MIMI KUPITIA BLOG YAKE,,NINA UHAKIKA HATA RAIS AKUULIZE SASA HIVI ANKAL KAMA UNATAKA UWAZIRI UTASEMA BORA NIENDELEZE LIBENEKE YANGU KWA JAMII.KUTWA HUNASHUSHIWA MADUAH TUUUU!

    NAONA WENGI MNACHANGANYA JINA LA AHLAM NA AHLAN,,,MIMI NI MWANADADA,,,WALA SIO MKAKA KAMA MNAVYOSEMA.NINGEPENDA SANA WADAU MLIOCHANGIA VIZURI KAMA HAO NILIYOWATAJA HAPO JUU,,MGENIPA MAJINA YENU!ILI NIWEZE KUWAJUWA ZAIDI KWA MSAADA WENU.
    NAKUSHUKURU SANA TENA SANA MICHUZI KWA KUNILEKEBISHIA UJUMBE WANGU!SHUKRANI SANA

    BI AHLAM,,,LONDON

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...