Nimelazimika leo Jumamosi, tarehe 18 Februari, 2012 kutoa taarifa hii kwa vyombo vya habari kufuatia mkutano wa DCI Robert Manumba na waandishi wa habari jana (17/02/12) kuongelea, pamoja na mambo mengine, hali yangu ya afya na kuhitimisha, kienyejienyeji tu kuwa “sikunyweshwa sumu” ila naumwa tu ugonjwa wa ngozi bila kufafanua ugonjwa huo wa ngozi umesababishwa na nini!
Napenda nisisitize mapema kabisa kuwa msimamo huo wa Jeshi la Polisi umenikera sana katika hali niliyonayo ya ugonjwa, kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake unaoendelea hospitali ya Apollo nchini India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu; pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa “sikunyweshwa sumu” wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu; na tatu kwa Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.
Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Februari, 2011 nilimwandikia barua IGP Said Mwema kumtaarifu kuhusu njama za kuondoa maisha yangu na ya viongozi wengine. Kwa kutambua kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania daima husisitiza kuletewa ushahidi kwanza ndipo lifanyekazi, nilihakikisha nimeainisha katika barua hiyo kila ushahidi nilioupata au kupewa. (Utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kusubiri kuletewa ushahidi mezani, kama ambavyo mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani, haupo popote pale duniani (ila Tanzania tu) kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. Polisi wanachohitaji duniani kote ni kupata clue au tetesi tu. Hiyo inatosha kufukua ushahidi wote unaohitajika). Pamoja na kujitahidi kuanika kila aina ya ushahidi niliokuwa nao, mambo manne yalijitokeza ambayo yalionyesha wazi kuwa Polisi hawakuwa na dhamira ya dhati ya kupeleleza suala hilo:
(i) Siku chache baada ya kumkabidhi IGP barua hiyo, nilitumiwa timu ya “wapelelezi” ofisini kwangu kuja kuchukua maelezo yangu ya ziada. Timu hiyo ilikuwa inaongozwa na ACP Mkumbo, afisa wa polisi ambaye wiki chache zilizokuwa zimepita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kumbambikizia madawa ya kulevya mtoto wa Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, suala ambalo mpaka leo hii uongozi wa Polisi umeshindwa kulitolea maelezo ya kuridhisha. Kwa msingi huo, nilikuwa nimeletewa mtuhumiwa wa rushwa/ ujambazi kuendesha uchunguzi wa watuhumiwa wengine wa ujambazi! Nikatambua mara moja kuwa zoezi zima lilikuwa la mzaha, tena mzaha mkubwa!
(ii) Wiki chache baada ya barua yangu kuwasilishwa kwa IGP na timu ya ACP Mkumbo “kuanza kazi”, Jeshi la Polisi likachukua hatua ya kuwapongeza na kuwazawadia askari niliowatuhumu kushirikiana na majambazi! Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwa ujumbe tosha wa kunipuuza.
(iii) Hivi karibuni tuhuma za askari polisi kujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto na kuwagusa askari “wale wale” niliowatuhumu kwenye barua yangu, IGP alichukua hatua ya kuwahamishia mikoa mingine!
(iv) ili kunikatisha tamaa kabisa, barua yangu ya “siri” kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kama habari ambayo ilikebehi na kukanusha taarifa nzima niliyotoa, sijui kwa faida ya nani! Lakini huu ni mchezo wa kawaida kwa polisi kwani hivi karibuni Mhe. Waziri Samuel Sitta alipohojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ofisini kwake, wakiwa wawili tu, taarifa ya kikao hicho ikawa kwenye moja ya magazeti ya mafisadi ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta! The integrity of the police force leadership is on the line.
Nimeelezea vizuri katika barua yangu kwa IGP kuwa kundi hilo la mauaji lilikuwa limeelekezwa kuniua kwa kutumia sumu, taarifa ambayo kwa karibu mwaka mzima Polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wenyewe. Sasa huu msukumo mpya wa Jeshi la Polisi kutaka kujua kama nilipewa sumu au la na kukurupuka kutoa tamko hata kabla ya kunichunguza nilivyo, kunihoji mimi na wasaidizi wangu ofisini na hata kuongea na mabingwa wa Kihindi wanaonifanyia uchunguzi, umetokea wapi? Si ni polisi hawahawa ambao, badala ya kushukuru, wamekuwa wakikerwa na tahadhari ambazo Waziri Sitta amekuwa akitoa ili suala hili lichunguzwe kwa kina?
Aidha napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matatibabu yangu au walisoma taarifa “nyingine”, na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au “walisomewa”! Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa wandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua, kukidhibiti /kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi wala aibu: “hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu”!
Nimesoma darasa moja Kitivo cha Sheria Mlimani na DCI Manumba. Baadaye IGP Mwema alikuwa mwanafunzi wangu wa sheria Mlimani. Vigogo hawa wawili wa usalama wa raia nchini hawajanitendea haki, nao wanajua. Wanajua vilevile kuwa sitakaa kimya au kumung’unya maneno come what may pale ambapo haki inakanyagwa.
Tuendelee kuombeana afya na uhai ili tutendeane haki na vilevile tuitendee nchi yetu haki kwa kuvimalizia viporo vinavyokera vya Dowans, EPA, Kagoda n.k. kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Dk. Harrison G. Mwakyembe (Mb), NW-UJ
Dar es Salaam
18/02/12
Inavyoonekana Mh Mwakyembe amelishwa sumu. Ila kwa maslahi ya mafisadi hili swala linappuzwa. Polisi wakikiri Mh Mwakyembe 'alilishshwa' sumu itawabidi kupeleleza waliomlisha sumu, ambao ni mafisadi. Mimi naamini Mh Mwakyembe anaathiriwa na sumu kutokana na harakati zake kupinga wizi. Tuombeane!! Mungu ibariki Tanzania, nuru italetwa na wapenda haki.
ReplyDeletekazi ipo!!!!na ndio kwanza imeanza!!
ReplyDeletePole sana mheshmiwa endeleza imani kwa mungu kwni yupo na ww pamoja na endelea kuongoza mapambano kwa ufisadi uliokisili.
ReplyDeletePole sana mheshimiwa. Mtu yeyote anayelituhumu jeshi la polisi ninamuamini kwa 100%. Kwa asilimia 98 hili letu ni jeshi la polisi kwenye uniform na vitambulisho tu. Wananchi tujihadhari sana na hawa maofisa 'wetu.' Ni sawa na papa anayeogelea na vidagaa huku akisubiri vikue ili avigeuze mlo.
ReplyDeletemuheshimiwa mwakyembe,pole sana na tunakuombea uugue pole,sisi wananchi tuko na wewe bega kwa bega katika kutokomeza rushwa na pia katika kufichua ufisadi
ReplyDeletembona kikwete au pinda hawaingilii masuala ya muhimu? siyo tu la mwakyembe kulishwa sumu ila la polisi kujihusisha na ujambazi na mkuu wao kutotoa taarifa zozote za hatua?
ReplyDeletemaneno mengiiiii sema unachoumwa
ReplyDeleteTUNAKUOMBEA UPONE INSHALLAH,HV KWELI KUWA MUADILIFU NI KOSA,TUNAWAIDI KUWA WATANZANIA TUPO PAMOJA NA MH SITTA NA MWAKYEMBE,NYIE NDIO MAJEMBE YA UKWELI NA HAKIKA MUNGU YU PAMOJA NANYI NA TUTASHINDA,WAACHE KUJIFANYA MIUNGU WATU.
ReplyDeleteJeshi la polisi ni la kihuni na kisanii kivipi waanze kukanusha badala ya kufanya uchunguzi kwanza? Halafu askari wanatuhumiwa kwa ujambazi na rushwa badala ya kufukuzwa kazi na kufunguliwa mashitaka wanahamishiwa vituo vingine vya kazi?
ReplyDeletedah hii kali jamani haki ya mtu Tanzania itakuwa lini tunajidai kuna demokrasi hakuna kitu.ila Mungu yupo
ReplyDeletepolisi ni kichocheo cha maovu nchini na wao wakiwemo,polisi wa tz wanajilipa posho za ujambazi.Mwakyembe pole sana kwa shida unazozipata.UFISADI NI VITA YETU WOTE NA TUTASHINDA TU.
ReplyDeleteKuwatita hawa watu waheshimiwa ni upuuzi mtupum binadamu wote ni sawa!!!
ReplyDeleteHii inaitwa KUFELI KWA SYSTEM...yaani vyombo vya dola vinachezeana na Waziri wa Serikali hiyohiyo. Mwakyembe vs Nahondha...something is very wrong somewhere. Na wale jamaa wanaoitwa Usalama wako wapi jamani labda watatusaidia kama wako neutral kuliko polisi.
ReplyDelete.....kama Waziri haiamini Polisi nani tena aiamini.
Pole sana ndugu yangu hata wakikuuwa watakuwa hawajafanya kitu na wao kuna siku nao pia watakufa tena wana weza kufa kibaya zaidi ya watakavyokuuwa wewe na pia siku ya HUKUMU ina wangoja MUNGU anakuona usihuhuzunike sana hayo yote waliyokutenda kuna faida kwako ni MAPEMA sana KUIJUA,NINATISHIKA kurudi BONGO ingawa ninaipenda TANZANIA imeandikwa na shangaroro (USA)
ReplyDeleteAnachosema Mh. Mwakyembe ni kweli hakulishwa sumu, na mimi nakubaliana nae kwamba hakulishwa sumu ila ukweli ni kwamba aliwekewa sumu ambayo imemdhuru vibaya sana. Mh. pole sana Mungu alakusaidia na kukuongoza
ReplyDeleteKwa nini mnamuua Mwakyembe? Kwani hiyo kazi ya kubaini kama kulikuwa na ufisadi si mlimteua wenyewe? Mikataba yote mibovu ilianzia awamu ya Tatu na kupkelewa na awamu ya nne...kwani hamkujua yeye ni mwanasheria?....Why Killing? na isitoshe hamkuanzia kwa Mwakyembe tu....You are killing innocent souls
ReplyDeleteMkulu! mkulu! WAPI?
ReplyDeleteMaskini polisi mmeshikwa na Mafisadi.Kazi ipo.DCI unajifanya daktari?Hapo ndipo shughuli imeanza sasa.Polisi wamewasha Mwenge
ReplyDeleteDavid V
Mafisadi watatufikisha pabaya kweli yaani hata Polisi wananshindwa fanya kazi zao. Pole sana Mh. Mwakyembe tupo pamoja katika ukombozi wa nchi yetu.
ReplyDeleteMh Mwakyembe kwanza nakupa pole sana kwa kuugua, Mungu ndiye mponyaji weka imani yako kwake.
ReplyDeletePili, ningependa kukupa ushauri katika wakati huu mgumu ambao unapata matibabu, jaribu kuweka mkazo kwenye tiba yako zaidi kuliko kujipata-stress za hili na lile.
Kama ambavyo umesema kuwa madaktari bado wanaendelea na uchunguzi, basi wale na wewe jitulize hadi hapo taarifa kamili ya kitaalam itakapotolewa.
Tatu, naomba wale wote ambao wamekuwa ni wasemaji wa afya ya Mh wasitishe rumours as mwenyewe leoamesema kuwa madaktari kule India hawajamaliza kazi yao ya uchunguzi.
Kamanda tuko nyuma yako wewe ni mtanzania halisi sauti ya wanyonge,utapona mungu yu pamoja na wenye subira
ReplyDeleteNakubaliana na wadau hapo juu, wakiwa wanampa pole Mh. Mwakyembe (MB)kwa yaliyomfika na kumpa moyo wa kuwanyakuwa watanzania kutoka kwa mafisadi, na wakasema kuwa "wako bega kwa bega na yote ayatendayo kwa Watanzania".
ReplyDeleteMimi muono wangu ni kama ufuatao:
1. Nikiwa ninawaunga mkono wadau hapo juu, na pengine kuwaunga mkono watanzania wote wenye hekima kufuatana na jambo hili, nakutakia kila lakheri ya mapigano ya afya yako NA MUNGU ATAKUSALIMISHA,na nina UHAKIKA utapona.
1(a) Ninaelewa saana maumivu aliyoyapitia na anayoendelea nayo hivi sasa mwilini kwake kutokana na yaliyomsibu; ambayo yeye ndiye anayeyajua zaidi kuliko sisi sote. Kama inavyofahamika yote hayo yanatokana na jinsi alivyojitolea mhanga kuwatendea haki watanzania wenzake, ikijumuisha familia yangu dhidi ya MAFISADI.
2. Ninachotofautiana na wadau hapo juu na hata na watanzania walio wengi nikumuacha Mh. Mwakyembe peke yake asijue la kufanya.
2(a) Huyu Mh. amedhuriwa pengine na maharamia, makaburu au Mafisadi wanaofahamika hapa nchini mwetu; na amedhuriwa kwa kuwatetea wananchi wenzake.
Hivi sasa anaumwa, anateseka mno kwa ajili yetu. na kwa bahati mbaya sanaa ametueleza sisi watanzania kilichomsibu.
3. Final: Hivi sisi Watanzania, ni watu wa aina gani jamani, tuna utamaduni gani? mbona hata mimi ni mtanzania lakini siwaelewi?
Kwa nini hatuna hata fadhila na kuwatendea haki watu kama wakina Mh. Mwakyembe.
4. Hitimisho: Tuwaunge mkono, tuwasaidie (kwa vitendo), tuache longolongo kama ilivyo kawaida yetu Wa-bongo.
hivi mnaelewa kuwa anatusaidia sisi , watoto wetu na wajukuu zetu.
SHIME, TUSHINIKIZE SEREKALI ITUELEZE NI KITU GANI KILICHOTOKEA MPAKA MH.MBUNGE, KIONGOZI WETU WA NCHI AKAFIKIA HAPA ALIPO. mimi si Mnyakyusa na wala huyu si shemeji yangu, ila kama Mtanzania mwenye heshima, hekima, elimu ya juu, nimetafakari nikaona kuwa hatumtendei haki Mh. Mwakyembe kwa kukaa Kimiya. kumbukeni, tunavyozidi kukaa kimiya kesho litampata: Mh. Sita, , Mh.Mama Malecela, Mh. J. Makamba, Mh.Zitto au hata Mh. Raisi wetu tuliomchagua kwa ridhaa zetu.
Nawaomba tusilifungie macho swala hili la kutupiana Miba.
MHESHIMIWA LAZIMA UKILI KUWA MAFISADI WAMEJIPANGA VIZURI NA USIPOANGALIA UTAKUFA KAMA MFUASI WA KIBWETELE.INAELEKEA WAMESHALIWEKA SAWA JESHI LA POLISI NA HIVYO UWEZEKANO WA KUGUNDULIKA WALIOKUSHUGHULIKIA KWA SASA NI MDOGO SANA LABDA SAMWELI SITTA AWE RAIS WA JAMHUSRI YA MUUNGANO ANAWEZA LABDA KUSHINIKIZA WAGUNDULIKE.KWA SASA MHESHIMIWA TUMIA DAWA TU USIZIDI KUJIPANDISHA PRESHA.NCHI UNAIJUA HII MISINGI YAKE NANYI MLICHANGIA KUIWEKA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE.....
ReplyDeletePole sana Mheshimiwa, M'Mungu akuponye haraka. Keep up the faith. Utapona. God is with you.
ReplyDeletepole sana muheshimiwa ila nakuomba ushauri hata hiyo Hospitali unayopatiwa matibabu kuwa nayo macho mwenyewe unajua jinsi wenzetu mafisadi walivyo na nguvu wanaweza kuwapa pesa hao wahindi wa India iliyopo hiyo hospitali na kukumaliza kabisa,ushauri wangu njoo huku marekani hawa wako wazi sana sio rahisi kumuonga daktari na wana vipimo vya hali ya juu sana,lakini kwa India bado usalama wako huko mashakani,ushauri.
ReplyDeletePOLE MWAKYEMBE NENDA LOLIONDO KAMA WENZAKO MAWAZIRI WENGI WAME ENDA KULA KIKOMBE WAMEPONA ACHANA NA INDIA MATAPERI TU KAMA HAO KINA MWEMA UNAOWATUHUMU NENDA KWA BABU KIKOMBE KIMOJA TU NGOZI YAKO ITAKUWA KAMA YA ROSTAM AZIZ AMA REGINALD MENGI. USHAURI TU.
ReplyDeleteHivi unapokuwa na Waziri ama Mawaziri wanaodai hawana imani na uongozi wa Jeshi la Polisi na viongozi hao bado wanaendelea kushikilia nyadhifa zao na Waziri ama Mawaziri hao nao wananendelea kubakia katika Baraza la Mawaziri si ishara ya Searikali iliyo paraganyika? Nasema Mwakyembe na Sitta hawaisaidii Searikaliwala kumsaidia Mhe Rais. Iwapo wanatoa tuhuma za namna hii kwa chombo muhimu cha usalama wa raia hawapaswi kuendelea kuwa sehemu ya Serikali. Wangekuwa na maadili ya kutosha wangejiuzulu wasingoje kufukuzwa. Huruma za Rais wasizione ne unyonge. Pamoja na kuwa na huruma na kumpa pole Mhe Mwakyembe kwa hali ya maradhi yanayomkabili naamini wamevuka mipaka!
ReplyDeleteHivi unapokuwa na Waziri ama Mawaziri wanaodai hawana imani na uongozi wa Jeshi la Polisi na viongozi hao bado wanaendelea kushikilia nyadhifa zao na Waziri ama Mawaziri hao nao wananendelea kubakia katika Baraza la Mawaziri si ishara ya Searikali iliyo paraganyika? Nasema Mwakyembe na Sitta hawaisaidii Searikaliwala kumsaidia Mhe Rais. Iwapo wanatoa tuhuma za namna hii kwa chombo muhimu cha usalama wa raia hawapaswi kuendelea kuwa sehemu ya Serikali. Wangekuwa na maadili ya kutosha wangejiuzulu wasingoje kufukuzwa. Huruma za Rais wasizione ne unyonge. Pamoja na kuwa na huruma na kumpa pole Mhe Mwakyembe kwa hali ya maradhi yanayomkabili naamini wamevuka mipaka!
ReplyDeleteKikwete UPO ?? ni wewe peke yako unaweza kuweka mambo ya Dr Harrison, wazi wazi maana wote hawa kina Kanumba na kina mwema wako chini yako, angelikuwa Nyerere tungeliwasikia aidha hawana wizara maalum au kanumba balozi mpya Burundi huko hakuna ulaji wala kufisadi ni yeye tu na mshahara wake na akitolewa huko anasitaafishwa ndo kifo chake , na hii ni kwa sababu watu kama hawa huwa na siri nyingi za serikali ambazo huwezi kumkurupusha ghafla-lazima iwe hatua kwa hatua ndivyo mwalimu alivyokuwa anawafanya madingi kama hawa, sasa wewe kikwete najua unasita, ngoma nzito UONGOZI jamani, tusione tu kila siku tunaamuka na kupanda daladala na kubadilisha bia leo malta kesho lager-lakini !!! kaeni mkijua IKULU ni joto kali,na kukichafuka tu ,tusiombe. Wasomali wanamkumbuka Siadbare ingawa alikuwa fisadi lakini kulikuwa na amani, siwatetei mafisadi bali na hofia amani.Bora kukokota mkokoteni najua kesho nitaamuka na kuuchukua tena mkokoteni wangu nikiwa na amani moyoni mwangu kwamba sijamdhuru mtu na wala sina chupa ya sumu niliyoiandaa kwa ajili ya Mwakyembe.
ReplyDeletekaka Mwakyembe u r a role model of young honest politician..tuko pa1 kaka sisi wananchi! hata wakikuuwa, love is greater than death..siku 1 aibu yao wote akiwemo DCI Manumba itawarudia.
ReplyDeletekama waziri hatendewi haki sisi wadogo tutaenda wapi???
ReplyDeleteanonymus Sun Feb 19, 04:17:00 AM 2012. una matatizo ya akili, au na wewe ni fisadi in one way or another. kama unajua Mwakyembe na Sitta walivyolisaidia Taifa hili usingesema unayosema au umetumwa nini? ni nani kwny historia ya Tz aliweza kuwa na ujasiri wa kumsema Waziri mkuu waziwazi na kuuanika ufisadi wake kama sio Mwakyembe na kamati yake aliyouvunja huo mwiko? kama sio Sitta akiwa spika kuruhusu huo mjadala uendelee? hivi wewe unajua wakati mgumu waluioupitia kufikia hayo mafanikio? USIKATISHE TAMAA WAPIGANAJI WETU. TUKO PA1 NAO SISI WATANZANIA.
ReplyDeleteLAKINI NA WEWE MH. MWAKYEMBE KWA NINI USINDE KWENYE HOSPITALI NYINGINE ZA NCHI ZILIZOENDELEA ZAIDI KULIKO INDIA (APOLLO) UKAPATE WORLD CLASS TREATMENT?. AU UNASUBIRI MAMBO YAWE MABAYA HALAFU MAJUTO?????
ReplyDeleteKILICHOBAKI KWA UPANDE WA SERIKALI SASA NI KULETA TIMU HUTU YA UCHUNGUZI KUTOKA MAREKANI ILI KWELI UPATIKANE. NARUDIA TIMU ITOKE MAREKANI....LA SIVYO HILI SUALA LITAENDENEA KUWA TATA
DCI= Director of crimes investments.
ReplyDeleteDefender of crimes involvements.
CID= Crimes installations department
Crimes investments department
Mheshimiwa Dr Harisson M. pole sana kwa haya yanayokupata, siku zote ukombozi au ushindi huja kwa njia ngumu sana lakini hatimaye utayashinda yote, polisi hawa DCI na IGP wanatakiwa kujiuzulu kwa kuudanganya umma wa watanzania.
ReplyDeletePole sana Dr Mwakyembe,endelea kuliamini jina pekee la mwana pekee wa Mungu Bwana Yesu Kristo.
ReplyDeleteMimi naamini utapata uponyaji kumbuka aliweza kumfufua Lazaro aliyekuwa tayari akinuka na amekwisha fukiwa kaburini itakuwaje wewe hata bado hujafa.Yesu bado anaponya hata sasa maana ni yule yule jana,leo na hata milele.Msaada wa Tanzania utatoka kwa Mungu pekee na si vinginevyo.Watu wa Mungu tuendelee kuomba kwa ajili ya Tanzania na kumwombea Dr Mwakyembe.
Watanzania wenzangu tufikie mahali tuwe na michango ya kujenga na si kukebehi pale mtu anapotoa hisia za kile kilichomkuta. Binafsi nakubali sana kazi ya mwakyembe, sita, magufuli na wengine wachache BUT nchi yetu tumekuwa kama tumelishwa limbwata tunatishwa na mabomu ya machozi ili tusiongee tusipolikemea hili hali itazidi kuwa mbaya zaidi. Mimi jeshi la polisi sina hamu nalo hata kidogo.Niliwahi kupoteza ndugu yangu wa karibu sana ambaye kwangu mimi alikuwa ni kama mzazi tu aliyekuwa akigharimikia ada na kila kitu akavamiwa majambazi wakafanya kila wanachotaka ikiwemo kumuua kwa risasi na wakaanza kunywa pombe mlemle ndani watu wakakimbia hadi polisi kuwambia wakawajibu eti tuleteeni gari ndo tutaenda na ni sehemu ya kukimbia tu na kuwawahi majambazi but majambazi walijiondokea taratiibu after two hours ndo nao wanafika eti kupima hatua ilinikera sijapata ona. Rais ni kama kapingwa ganzi hana la kusema Mungu atujalie 2015 labda neema itafunguliwa jeshi lisafishwe maana kubambika kesi wanaongoza and worse enough these days wanaoenda huko mafunzoni ni watoto wao waliofeli form four hata si kwa nia ya kulinda raia wakipewa hela na majambazi wanawapa bunduki shame shame shame! nenda ngra huko, kigoma, karagwe watu wanavouliwa safarini eti tuna polisi bora hata waweke jeshi huko maporini but with these police always watakuja baada ya tukio and will always be conducting endless investigations. Pole sana Dr. Mwakyembe Mungu wetu aliye hai hatakuacha tunakuombea upone and trust no one except GOD hawa mafisadi kuwaondoa ni kwa neema ya Mungu na njaa za wabongo hata chai jiungie tu au mkeo awe anakufungia asubuhi unaenda nayo na ukiweza usishikane mikono na watu. Always jifunike kwa Damu ya Yesu kabla ya kufanya chochote, usiingie ofisini bila kutanguliza Damu ya YESU. MUNGU AKUTETEEE NA KUKULINDA
ReplyDeleteMWAKIYEMBE HAMA NA HOSPITAL SASA UENDE NYINGINE KWANI LAZIMA UTIBIWE APOLLO?...HIVI HUJUI NA APOLLO MAFISADI WANAMKONO WAO?WEWE PIGA MAKELELE TU UONE WATAKAVYOKUZIMISHA HUKOHUKO URUDI KWENYE SANDUKU.APOLLO NI MRADI WA MAFISADI WA KUDIDIMIZA MUHIMBILI NA KUCHUMA FEDHA ZA NCHI KWA KUPELEKA WATU HUKO.HAMA UPESI KABLA HAWAJAKUFIKIA HAPO WAKAKURESTISHA INI PISI
ReplyDeleteHii yote ni njama za kunyamazisha vita kali ya ufisadi. Kulikuwa na wanaume Col. Muamar Gaddafi na akina Hosni Mubaraka wakang'olewa na jamii ya aina ya Mh. Mwakyembe, na wengine, watu wapenda nchi yao, wenye uchungu na rasilimali za Tanzania zinazogawanywa kwa wabinafsi wachache huku wengine wakitaabika. Nini hawa mafisadi wachache waliojilimbikizia mali? Wao pia watakiona cha mtema kuni na kung'olewa hapo walipo. Nahisi harufu ya North Africa inakuja
ReplyDeleteAnon wa feb19,03:04:00 umemaliza yote niliyotaka kusema, imagine tin namba za lesen mpya zinatolewa bure ila dar zinanunuliwa i mean ukienda tra, polisi lazma hela ikutoke. Dr. mwakiembe nakuombea kwa mungu utapona, wewe na sita ndo tunaowaamin maana bila nyinyi mafisadi wasingegundulika tz.
ReplyDeleteNaungana sana na jamaa wa sunday ni kweli Apolo ni mradi wa mafisadi na ni hao wenye sauti kuwa macho sana hama haraka then kama ni gharama watu watakulipia tu kwa kwa kuchanga harambee chonde hata ukilalamika vipi hakuna msaada wowote wahi haraka.wana watu wao kule Apolo na ndio wanaoratibu matibabu yako please please Ondoka hao jamaa ni mafia na wana pesa walizoiba nyingi tu hata Rais anawaogopa yaani anangoja muda wake ufike aondoke madarakani kwani jamaa ni hatari.
ReplyDeleteHAIWEZEKANI TUMWACHE AFE PEKE YAKE:
ReplyDeleteTUTAKUWA NA KOSA LA KUJIBU MBELE ZA MUNGU!
Haiwezekani nchi yetu yenye watu 45 Milioni ika dhibitiwa na watu wasiozidi 45 tu!, wanaofahamika na kuhesabiba hata kwa mkono bila kutumia Komputa au mashine!
Haiwezekani Genge hili dogo likaendesha mambo kama wana vyotaka wao kwa kutaka kuimiliki Nchi nzima bila kujali wengine.
Ni lazima wapatikane na kuadhibiwa vilivyo wote waliohusika katika madhambi haya ya kumlisha sumu Mpiganaji Nguli Dr. Harrison Mwakyembe!
HAWA WATU WACHACHE WANATAKA DUNIA ITUELEWEJE?
POLE SANA DR. HARRISON MWAKYEMBE, AMINI KUWA UMENUSURIKA, MUNGU AMEKUPONYA NA ANAKUJAALIA UTAPONA HARAKA.ILIYOPO TULIA BABA CHA MSINGI NA MUHIMU ZAIDI KWANZA KABISAA FUATILIA TIBA YAKO KWA KINA IKIWA UMENUSURIKA THEN, ALUTA KONTINUA!!!!!! NAKUOMBEA KWA MOLA NINA IMANI UTAPONA KABISA NA UTAENDELEA NA SHUGHULI ZAKO KAMA KAWA. SHETANI ASHINDWE NA WAMESHINDWA KWA JINA LA YESU. BARIKIWA,AMEN
ReplyDeleteHakuna kinachoshindikana chini ya jua.Tukiamua na tukiwa na nia moja hakika tunaweza kupunguza kasi ya mafisadi na tusiwape nafasi katika kutuongoza kwani kwa majina tunawajua baadhi.Pia watanzania wenzangu tujishuhulishe kwa kufanya kazi kwa bidii na hakika tusipende kupokea rushwa kwani mwisho wa ubaya ni aibu na pia.Tupende kuridhika na hali tulizokuwa nazo.Hakika katika chaguzi zijazo yatupa tuwe macho.SAY NO FOR CORRUPTION..!
ReplyDeletePole sana Muheshimiwa Mwakyembe! Stay focused and don't get into a trap of finger pointing people...GOD will take care of them if any. Since it is very well- known that "Great Spirits always encountered violent opposition from mediocre mind"(Albert Einstain) and Let them know if any..... that " if you once forfeit the confidence of your fellow citzens, you can never regain their respect and esteem. and further you may fool allm of the people some of the time; nyou can even fool someof the people all the time; but you can fool all of the people all of the time. Finally three things can not be hiden, the sun, the moon and the truth. Mwenye macho na aone na mwenye masikio na asikie. Mungu ibariki Tanzania...Mungu ibariki Afrika!!
ReplyDelete