Naibu Spika, Mh. Job Ndugai akitoa hotuba yake alipokuwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya kidato cha Sita katika shule ya Sekondari ya Mt. Theresia iliyoko Kisongo mkoani Arusha mwishoni mwa wiki. Katika hotuba yake Mhe. Naibu Spika aliwahimiza vijana kutambua kwamba hivi sasa soko la ajira lina ushindani mwingi sana na hivyo yawapasa vijana kuthamini elimu na pia kupata ujuzi mwingine kama vile lugha za kigeni na kompyuta ili kuwa na sifa za kuajirika vizuri na pia kuweza kushindana vizuri katika sekta binafsi.
Naibu Spika,Mh. Job Ndugai akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita katika shule ya Mtakatifu Theresia mkoani Arusha jana. Shule ya Mtakatifu Theresia inamilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Kaskazini ambapo jumla ya wahitimu 87 walikabidhiwa vyeti vyao vya kumaliza kidato cha sita hapo mwishoni mwa wiki. Hii ni moja ya shule zinazofanya vizuri sana kielimu Kanda ya Kaskazini ambapo katika mitihani ya Kidato cha Pili iliyofanyika mwaka huu shule hiyo ilishika nafasi ya 9 kati ya shule 300 za Kanda.Picha na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hivi jamani haya mavazi si yamepigwa marufuku? hapo unaweza fikiri wamemaliza chuo kikuu na mgeni rasmi ni anatoa vyeti kwa wahitimu wa PhD... naomaba tuacha ne na mavazi ya elimu ya juu ... uniform inatosha tuuuuuuuuuuuuuuuuu.....

    ReplyDelete
  2. Sahihisho: Hakuna Jimbo la Kaskazini katika oganaizesheni ya Kanisa Katoliki.

    Shule ipo Jimbo Kuu la Arusha.

    ReplyDelete
  3. Jamani mavazi ya elimu ya juu yanapendeza saaaana.

    ReplyDelete
  4. Haya mavazi ya elimu ya juu yanapendeza sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...