Na MERY AYO,Arusha
VIONGOZIwa madhebebu mbalimbali ya dini ya kiislamu mkoani Arusha,wameongoza kongamano maalumu la kulaani mauaji yanayofanywa na kikundi kidogo cha kiislamu chenye msimamo mkali cha Boko haramu nchini Nigeria dhidi ya madhebebu ya dini ya kikristo
Wakizungumza kwenye kongamano la amani lililofanyika mwishoni mwa wiki katika msikiti wa Ah madiyya jijini hapa,walidai kuwa hakuna maagizo ya mwenyezi mungu yanayotoa mamlaka kwa kikundi hicho ama mtu yoyote kutekeleza mauaji hayo dhidi yawaumini wa dini nyingine.
Amiri na mbashirimkuu wa jumuiya ya waislamu wa Ahmadiyya nchini,Tahir Mohmood Choudhlyaliwaomba waislamu kote duniani kuungana na kulaani vitendo vya kinyama kamahivyo vinavyofanyika kwa kutumia
mgongo wa uislamu
.Aliwaomba watanzania kuwalilia wananchi wote waliouawa kutokana na kikundi hicho cha Boko haramu nchini Nigeria,na aliiomba serikali nchini humo, kukakikisha inadhibiti mauaji hayo na kukishighulikia kikundi hicho kinachotumia mgongo wa uislamu.
‘’sisiwaislamu tufike mahali tuelezane ukweli kwani matukio mengi ya uvunjifu waamani yakiwemo kujilipua yanasababishwa sana na waumini wenzetu ,hakunamaandiko yanayoagiza dini ya kiislamu iteketeze dini
nyingine ‘’alisemaChoudhly.
Aidhaaliongeza kwa kuwataka viongozi wamadhehebu ya dini nchini kusimama imara katika kutetea amani na kujiepusha nauchochezi,kwani taifa linawategemea sana katika kuepusha machafuko yanayowezakuibuka
. Katika hatua nyingine, aliwatakawananchi kuheshimu viongozi waliopo madarakani na kuacha kupinga kila kitukinachotamkwa na kiongozi aliyeko madarakani, badala yake watoe mchango wakusukuma maendeleo ya taifa hadi utakapo fanyika uchanguzi mwingine. NayeSheikh mkuu wa Ahamadiyya kanda ya kaskazini,Mzafara
Ahamad,alisema kuwa lengo lakongamano hilo lililowashirikisha viongozi mbalimbali wa madhehebu mbalimbali yadini ya kiislamu nchini ni kutoa mada ya kuomba amani na kulaami mauaji yakikatili yanayoongozwa na kikundi haramu cha kiislamu nchini Nigeria.
Alisemakuwa kongamano hilo lilienda sanjari na uzinduzi wa msikiti huo wa Ahmadiyyamuslim Jamaint uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 70 kwa ajili ya ukarabatiulioanza mwishoni mwa mwaka jana
. Kwa upandewa sheikh mkuu wa Aha madiyya mkoa wa Morogoro,Bakari Kaluta,aliwataka viongozi wa dininchini kutawala kiuadilifu hukuwakiongozwa na mwenyezi mungu katika mahubiri yao na kuacha kuwa
sehemu yakuleta mitafaruku ya kidini.
Ameyasihimadhebebu ya dini kuwa na utaratibu wa kuandaa makongamano ya kuomba amani,kwani bila hivyo nchi itaelekea kubaya kwakuwa baadhi ya viongozi wa diniwamekuwa wakitumia vibaya maandiko matakatifu kwa kuhubiri uvunjifu wa amanikwa maslahi yao binafsi.
Naye meya wa jiji la arusha ,Gaudence Lyimo aliyekuwa mgeni rasimi katika kongamanohilo,aliyasifu madhehebu ya dini ya kiislamu kwa kuandaa kongamano hilo la kuomba amani ,aliwatia moyo viongozi
haokuwa serikali inatambua mchango wao na inawaungamkono kwa jambo hilo.
Aliwasihiviongozi hao wa dini kuwa sehemu ya serikali katika jitihada zakeza kuhakikisha kuwa amani inapatikana kwa kila mtu hapa nchini na duniani kote.
tunashukuru kwa taarifa nzuri lakini wakati mwingine hariri kazi yako vizuri hasa kutenganisha neno na neno. Tujitahidi jamani maana ni aibu kama mtoa habari hawezi kuandika vizuri kazi yake je mtu wa kawawida atafanya nini?
ReplyDeleteNinaunga mkono hoja na jitihada, yanayoendelea Nigeria yanasikitisha sana.
ReplyDeleteMdau, Qatar.
CHANZO CHAKE NINI KWANI????
ReplyDeletePositive thinking. this is good news
ReplyDeletewabongo kupenda kujipendekeza tuu hawajambo.
ReplyDeleteTimbwili liko naijeria, Arusha yawahusu nini?
mavi usoyala wayawingiani kuku?
Mola awabariki wanakongamano wote na matakwa yao.
ReplyDeletebinadamu wote ni sawa na afrika ni moja. tunatoa pongezi angalau thi time arusha wamekuja kivingine yaani kwa kutafuta amani
ReplyDelete