Mhe. Ombeni Sefue Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza na watanzania hawapo pichani wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watanzania waishiio Jijini NewYork na Vitongoji vyake, kushoto kwake ni Mwenyekti wa Jumuia Bw. Hajji na kulia na Katibu, Bw. Shaban.
Mhe. Balozi akiwa na Mke wake Bibi Anita Sefue( aliyeshika zawadi) ambayo Jumuiya ya Watanzania walimkabidhi Balozi kama kumbukumbu ya kuwa Mlezi wa Jumuiya yao, wengine katika picha ni viongozi wa jumuiya hiyo.

Mhe. Balozi Ombeni Sefue, akiwa na Mke wake Bibi Anita Sefue katika picha ya pamoja na sehemu ya watanzania waliohudhuria hafla hiyo .

Na Mwandishi Maalum

New York

Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ombeni Sefue amesema, amejipanga vema kumsaidia Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Serikali kwa ujumla kupitia wadhifa wake mpya wa Ukatibu Mkuu Kiongozi

“Ninatambua dhamana hii ni kubwa, nzito na yenye changamoto nyingi,lakini nimejipanga kutumia uwezo wangu , maarifa yangu na ujuzi wangu wote kumsaidia Mhe, Rais na Serikali kwa Ujumla na nimejipanga kuzikabili changamoto zinazoambatana na dhamana hiyo”.

Balozi Ombeni Sefue, ameyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kumuanga na kumpongeza kwa wadhifa wake huo mpya, hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watanzania waishio jijini New York na vitongoji vyake.

Katika hafla hiyo iliyofanyika siku ya alhamisi na kuhudhuriwa pia na Mke wa Balozi, Bibi. Anita Sefue, Balozi Sefue licha ya kuwahakikishia watanzania hao kwamba amejipanga vema katika jukumu lake hilo jipya. Amewashukuru kwa kutenga muda wao kuagana naye na vilevile kumpongeza na kwamba ameguswa sana na tukio hilo.

Katika mazungumzo yake na watanzania hao, Balozi Sefue, amesisitiza umuhimu kwa wao, kuzidumisha na kuziendeleza sifa ambazo zimeifanya Tanzania kuwa moja ya kati nchi zinazoheshimika Barani Afrika.

Akazitaja sifa hizo kuwa ni umoja, mshikamano, upendo na kutobaguana kwa misingi ya dini, rangi, kabila au jinsia.

“Watanzania tunaheshimika sana, tunaheshimika kwa sababu tumeweza kuendeleza na kudumisha mambo makuu muhimu ambayo ni utamaduni wetu wa kupendana, kuheshimiana, kutobaguana kwa misingi ya dini, kabila, rangi au jinsia, wito wangu ninapoagana nanyi ni kwamba muyaendeleze haya hasa nyie mnaoishi ugenini” akasema Balozi Sefue.

Na kusisitiza kwamba, licha ya kuwa wao sasa wanaishi na kuendesha shughuli zao nchini Marekani. Lakini nyumbani kwao kwa asili ni Tanzania, na kwa sababu hiyo wanaowajibu pia kuwafundisha mambo hayo watoto wao, ikiwa ni pamoja na kuwarithisha mila na tamaduni za mtanzania na historia nzuri ya kule wazazi wao wanakotoka.

Akisisitiza umuhimu wa kusaidiana, Balozi Sefue amesema watanzania wataweza kusaidiana pale tu watakapokuwa na Jumuiya inayowaunganisha.

Na kwa sababu hiyo akawataka kuienzi na kuendelea kuiimarisha Jumuiya yao ambayo yeyé, licha ya kuwa mlezi wao lakini aliwasaidia sana kwa ushauri na mawazo yaliyopelekea kuanzishwa kwa Jumuiya ya Watanzania New York na vitongoji yake.

Akasema ni kwa kupitia Jumuiya yao ambayo viongozi wake wamepatikana kwa uchaguzi wakidemokrasia. kwamba ndipo mahali ambapo wanaweza kubadilishana mawazo ya namna gani ya kusaidiana wao kwa wao lakini pia kuwasaidia ndugu na jamaa zao waliowaacha nyumbani (Tanzania) na Taifa kwa ujumla.

“ Niwapongenze na kuwashukuru kwa kukubaliana nami pale nilipowapatia ushauri wa kuunda Jumuiya yenu, ninashukuru kwamba tangu kuasisiwa kwake mmekuwa mkiendelea vizuri.

Kwa upande wao na wakizungumza kwa niaba ya watanzania wenzao, Mwenyekiti wa Jumiya hiyo Bw. Hajji na Katibu wake Bw. Shaban Musemba, wamemhakikisha Balozi Sefue kwamba kama sehemu ya kuenzi mchango wake uliotukuka, watahakikisha Jumuiya yao haifi.

Wakasema katika kipindi kifupi ambacho Balozi amekuwa Mlezi wa Jumuia hiyo, wamejifunza mengi kutoka kwake, na kwamba wanasikitika watakosa mchango wake wa mawazo, ushauri na mwongozo. Lakini wanamtakia kila la kheri katika nafasi yake hiyo mpya ya kumsaidia Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ahsante Mhe. Balozi Sefue!

    Ari, Nguvu na Kasi yako kama ile ya UN ni wakati muafaka ukaiendeleza hapa nyumbani ukiwa bega kwa bega na Mhe. ndugu yetu JK ambaye kwa bahati mbaya wengi wanaomzunguka aliowaamini na kuwapa nafasi wamekuwa wakimwangusha na kumfanya yeye aonekane vibaya,,,INGAWA UKITUMIA AKILI UTAGUNDUA KUWA RAISI YEYE BINAFSI HANA NIA MBAYA NA NCHI YETU!

    ANGALIA Mhe. JK JINSI:
    -ALIVYOJITOLEA KTK SUALA LA MICHEZO HASWA SOKA.
    -ALIVYOZINGATIA SUALA LA KILIMO KWANZA.
    -ALIVYO TOA NAFASI KTK SUALA LA MCHAKATO WA KATIBA.
    -MSIMAMO WAKE JUU YA MAMBO KADHA WA KADHA YALIYOJIRI, MFANO SUALA LA MADAKITARI.
    -ANAVYOTOA NAFASI YA UONGOZI WA UMMA CHINI YA USHIRIKISHWAJI WA WATU WOTE.
    -ANAVYOZINGATIA TIJA NA HATMA NJEMA KTK MAMBO MBALI MBALI JUU YA TAIFA.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana mheshimiwa kwa kweli kama mke umempata.Mpende nae akupende muishi maisha marefu ya furaha.All the best.

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na mdau hapo juu...kinachotuangusha kuliko vyote nchi za Afrika ni RUSHWA....Wengi tumependa maisha ya juu ambayo hata wenzetu kwenye nchi zilizoendelea hawana...Kama atatokea kiongozi ambaye atapiga vita Rushwa bila woga hapo ndipo tutakapoona maendeleo...vitu vilivyotajwa hapo juu tunavi-enzi ila kama Rushwa inazidi kushamiri hatuendi mbali...!! Mdau-NYC, USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...