Mkurugenzi na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air
Alfonse Kioko
Precision Air – Shirika la ndege linaloongoza Tanzania imenyakua tuzo ya Shaba baada ya kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya shirika bora la ndege Afrika kwa mwaka 2011/2012, yaliyoendeshwa na ‘African Aviation News Portal’.

Mara baada ya kupokea taarifa hizo, Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Bw. Alfonse Kioko alisema, “Kutambuliwa na wateja wetu pamoja na washindani wetu ni heshima kubwa sana. Kushika nafasi ya tatu Afrika si jambo dogo. Napenda kuwadhibitishia wateja wetu kwamba tunaendelea vyema na mipango yetu ya kupanuka kibiashara na kuwahakikishia pia huduma bora yatakayopita mategemeo yao.”

Kwa mujibu wa African Aviation kura zilizopigwa na wasomaji wake, wataalam wa masuala ya anga, na wasafiri wa ndege wa mara kwa mara “zimeangalia ukuaji mzima wa kampuni, huduma kwa ujumla, pamoja na sifa na uhakika wa huduma za kampuni.”

Precision Air imeshika nafasi ya tatu nyuma ya Ethiopian Airlines iliyoshinda nafasi ya kwanza na kuzawadiwa tuzo ya Dhahabu ikifuatiwa na Kenya Airways (wapili) walioshinda tuzo ya Fedha.

Kura zilipigwa kutumia njia ya mtandao katika tovuti hiyo, pamoja na kupiga kura za moja kwa moja katika vikao, makongamano, na matukio mbali mbali yaliyoshirikisha shirika hilo la African Aviation. Zaidi ya wapiga kura 20,000 walishiriki.

Jumla ya mashirika ya ndege zilizoshiriki mashindano hayo yalikuwa 25; Air Algerie, Air Botswana, Air Malawi, Air Namibia, Air Nigeria, Air Uganda, Arik Air, Asky Airlines.

Wengine ni; Camair-Co, Comair South Africa, Dana Air, Egyptair, Ethiopian Airlines, Fly540, Kenya Airways, Mozambique Airlines, Precision Air, Royal Air Maroc, Rwandair, Senegal Airlines, South African Airways, Sudan Air, TAAG Angola, TACV and Zambezi Airlines.

African Aviation, pitia wasomaji na wafuatiliaji (followers) wake, wanatambua mashirika yenye maendeleo yaliyojizatiti katika huduma bora kwa wateja, utaalamu, ubunifu na kuchangia mafanikio katika sekta ya utalii Afrika.

Tuzo hii “si tu kipimo cha mafanikio ya mashirika ya ndege bali pia ni ishara ya kuridhishwa kwa wateja katika sekta zote za usafiri wa anga,” inasoma kipande cha taarifa kutoka tovuti ya African Aviation.

Katika miaka ya hivi karibuni shirika la Precision Air limeweza kunyakua zawadi zifuatazo; ‘Best Scheduled Domestic Airline in Tanzania’ kwa mwaka 2011 iliyozawadiwa na Umoja wa Wakala wa Tiketi za ndege Tanzania (TASOTA); ‘Regional Airline of the Year’ iliyotolewa na Asasi ya Mashirika ya ndege Afrika (AFRAA ) 2010; ‘CEO’s Most Respected Company in Tanzania’ iliyofanyika kwa utafiti wa Pricewaterhouse Coopers kwa ukanda wa Afrika Mashariki 2008/9; ‘African Deal of the Year -2008’ iliyotolewa na Jarida la Airfinance kwa ajili ya mkataba wa dola 129 milioni ziliwezesha Precision Air kupata ndege 7 mpya aina ya ATR; pamoja na ‘Aircraft Leasing Deal of the Year in Africa- 2008’ iliyozawadiwa na jarida la Jane's Transport Finance kwa ajili ya mkataba huo huo wa ndege mpya 7.

Tayari African Aviation imeanza tena mchakato wa kutafuta Shirika bora la ndege la Kiafrika kwa mwaka 2012/2013, kwa yeyote anayependa kushirika kwa kupigia kura shirika letu la ndege la Precision Air anaweza tembelea tovuti ifuatayo.

http://www.african-aviation.com/index.php

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Fantestic news...Sasa munatakiwa muongeze mabawa mpaka west Africa na bara la Asia.

    ReplyDelete
  2. Mmejitahidi sana precision,hata hivyo mmetanguliwa na makampuni makubwa ya nchi husika kama Ethiopian Airlines ni kongwe na Kenya Airways pia!Congratulation kwa kazi nzuri!Mna mda mfupi sana lakini mmefanya mambo mengi,,sio kama shirika la Taifa letu(Air labda)...Mkurugenzi Alfonse,nilikuwa naomba nikuone kwa ajili ya kazi,,kama ndio nitashukuru,,nijibu tu humu humu,kisha nitakuja,,baada ya wiki moja
    Ahlam,,,,UK..London

    ReplyDelete
  3. mbona watanzania tunabebwa tuu kila mahali mimi binafsi nasafirigi na presition na nazani hata kwenye top ten airline za afrika nisingewawekaa. Vindege vidogo, kwenye kabini hakuna nafasi ya kutosha ya miguu kwa wale wengine siye warefu. Na hata pakuweka mizigo juu ni mgogoro

    ReplyDelete
  4. Mdau Ahlam wa UK London hapo juu nakuunga mkono!

    Kweli shirika la Taifa letu limekuwa (Air labda) kwa muda mrefu sana kama sio (Air hatihati),au (Air matarajio), au (Air Minshauri Wasiwasi) hivi!!!.

    Mbuni ni ndege kama walivyo ndege wengine na sifa ya ndege wote ni kuruka kwa mabawa yake, lakini wasifu alionao ndege Mbuni tofauti na ndege wengine yeye daima hutumia miguu na abadani haruki kwa mbawa zake!

    Miradi mingi hapa kwetu imekuwa na wasifu wa Mbuni, mingi kuwa ya kiganjani au inawekwa hewani ila ufanisi sifuri!

    Miongoni mwa Mbuni wakubwa kutokea hapa nchini kwetu mmoja wapo ni huyu (Air labda)!

    ReplyDelete
  5. Hongera sana precision..Air Tanzania vipi?(Dar-Kigoma 250000/-)Ila sijajua wamefuata masharti ganni,achana kwanza na haya mashirika ya nchi.Kuna hao ASKYS airline,ni private kama precision, wana makao yao makuu hapo jijini Lome,Togo.Hawa jamaa wana midege kibao mikubwa kuliko precision na wanapaa Afrika ya Magharibi na kati,wako ubia na ET.Kama alivyosema mchangiaji mmoja hapojuu,kunahitajika ndege ya kutoka Dar(Indian Ocean) kwenda North Atlantic sea(Afrika ya Magharibi kwa ujumla)

    ReplyDelete
  6. Kweli Wabongo mna maneno eti Air labda!Teh teh teh imekaa viuri hiyo!

    Ni kwa sababu ukitaka safiri unaambiwa labda itaenda au laa!Ndo maana unakuwa umeishabook kujiandaa na safari,unapigiwa kuwa imehairisha safari,,au unafika Airport ndege hakuna,,Naona kweli iitwe ilo jina Air Labda!!!

    ReplyDelete
  7. Kwa mwenendo wa utazamiaji wa Maendeleo ya Safari za Anga nchini (NDEGE HAJARUKA SAWASAWA KWA KUTUMIA MBAWA ZAKE, BADO ANATEMBELEA KWA MIGUU) ingefaa hili Shirika letu la ndege la Taifa liitwe kwanza (AIR MBUNI) /na pia nembo zake kuwekwa ndege Mbuni ktk mikia yake badala ya Twiga kwa muda wa unangalizi hadi hapo litakapokuwa na sifa na ufanisi ndio lipewe jina la Nchi kabisa (AIR TANZANIA)/ na nembo ya Twiga ni vile kwa sasa linatudhalilisha sana na kutushusha miongoni mwa Mashirika ya Mataifa hasa majirani zetu,Rwanda,Uganda,Kenya,Zambia na Malawi ambao wana mashirika ya Taifa yenye ufanisi!

    TUKUMBUKE KUWA TUKO KATIKA USHINDANI NA ULINGANISHI WA HALI YA JUU WA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI, SADEC NA COMESA.

    ReplyDelete
  8. Uhodari wa Tanzania ni katika Uwekezaji wa Kisiasa na Uenezi wa Kisiasa.

    Isipokuwa katika Ufanisi wa Uendeshaji Biashara na Ushindani wa Biashara, lohhh sifuri!

    Ni vigumu sana kuendesha kwa ufanisi biashara ya ndege zirukazo angani wakati tulishindwa kuendesha kampuni moja ya mji mmoja tu ya mabasi ya UDA yaendayo ardhini!

    Elimu ya Uchumi ,Unedeshaji Fanisi na Biashara ni muhimu sana kwa Watanzania kwa sasa, kuanzia ngazi ya Viongozi wa Taifa hadi chini, kwa vile mfumo wa Siasa ya Ujamaa ulitusaidia ktk upande mmoja na kuua kabisa uwezo wa kiujasiriamali wa Mtanzania.

    BILA HIVYO TUTABURUZWA MKIANI KTK USHINDANI WA MAENEO.

    ReplyDelete
  9. Meneja wa Kiwanda Tanzania anaweza kushindwa ktk maamuzi sahihi ya Kibiashara na Muuza genge kutoka China,Kenya,Arabuni,Somalia au Komoro!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...