Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Twiga Cement, Ekwabi Majigo (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Lesoinne Pascal (kulia) wakiwapongeza washindi wa jumla wa Wazambaji Bora wa saruji ya kiwanda hicho, Carol Mworia (wa pili kushoto) wa kampuni ya Kaizari General Supplies wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Twiga Cement kwa ajili ya wasambazaji hao jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Afya Mwambungu wa General Traders. Walipewa zawadi ya mifuko 600 ya saruji.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Twiga Cement, Lesoinne Pascal (kulia) akikabidhi zawadi kwa mshindi wa nne wa Wazambaji Bora wa saruji ya kiwanda hicho, Hassan Luono wa Ujenzi Store wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Twiga Cement kwa ajili ya wasambazaji hao jijini Dar es Salaam jana. Kushoto Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Twiga Cement, Ekwabi Majigo. Alipewa zawadi ya
mifuko 300 ya saruji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga Cement, Lesoinne Pascal ( wa pili kulia) akimpongeza Valence Masaky baada ya kampuni yao ya V.G.K Ltd kuibuka washindi wa tatu wa Wazambazaji Bora wa saruji ya Twiga Cement wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Twiga Cement kwa ajili ya wasambazaji hao jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Twiga Cement, Ekwabi Majigo na wa pili kushoto ni mke wa Msaky, Getrude Masaky. Walipewa zawadi ya mifuko 400 ya saruji.
Ofisa Mauzo wa TPCC, Gloria Stephen Mabada (kushoto) akiagana na baadhi ya wasambazi saruji baada ya hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Twiga Cement kwa ajili ya wasambazaji hao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wasambazaji wa saruji wa kampuni ya Twiga Cement wakiselebuka pamoja na baadhi ya maofisa wa kampuni hiyo katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Twiga Cement kwa ajili ya wasambazaji hao jijini Dar es Salaam jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...