Na Mery Ayo,Arusha
WAGOMBEA ubunge katika jimbo la arumeru mashariki wametakiwa kuwa waaminifu kwa kutotoa fedha kilholela kwa wananchi wao wawapo katika kipindi cha kampeni za uchaguzi kwa kuwa matumizi holela ya fedha hayaruhusiwi katika uchaguzi
Hayo yalisemwa na mjumbe wa halimashauri kuu CCM wilaya ya arumeru na mjumbe wa mkutano mkuu taifa bw Antony Musani wakati alipokuwa akiongea na waandishio wa habari mara baada ya kujitokeza kuchukua fomu ya kinyanganyiro cha kugombea nafasi hiyo ya ubunge .
Aidha alisema kuwa viongozi na wenye fedha waache kutawala demokrasia ndani ya ccm na badala yake wawe makini katika kumchagua mtu anayefaa kuongoza jamii kwa kuwa baadhi ya watu wanachaguana wale wenye fedha ambapo hata sheria inasema matumizi ya fedha kwenye uchaguzi hayatakiwi.
Vile vile aliongeza kuwa ni vema wajumbe wa mkutano mkuu wakawa makini katika kuchagua viongozi kwa kufuata maoni ya wananchi walio wengi na wasifuate miongozo bandia na utashi wa wachache wanaotaka kufamnikisha malengo yao bila kujali maslahi ya wananchi walio wengi
"Katika uchaguzi huu watu wasiangalie fedha au utajiri wa mtu au kundi la mtandao anaotoka mgombea ,bali tuzingatie kilio cha wananchi walio wengi na cha wananchama wa kawaida "alisema Musani.
Musani akielezea sababu zilizomfanya kugombea nafasi hiyo ya ubunge alisema kuwa ni ili aweze kuwakilisha mawazo na matatizo ya wananchi kwa kupigania maendelao ya wanyonge kushughulikia upatikanaji wa maji vijijni pamoja na kuboresha huduma za afya kwa wote.
Aliongeza kuwa endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha kuwa kero mbali mbali za elimu hasa zinazowasibu walimu zinashulikiwa ili kuwapa walimu utulivu katiaka swala zima la kuinua elimu katiaka jimbo hilo.
Aliwataka wagombea wote wa ccm kuacha chuki binafsi za kuchukiana na badala yake wapendane ili pindi mmoja wapo atakapoibuka kidedea katika jimbo hilo,wengine wamuunge mkono na kuacha kuendeleaza makundi ya kumpinga ama kukimbilia vyama vingine vya upinzani.
Hata hivyo CCM inatarajiwa kufanya uteuzi wa mwakilishi wake siku ya jumatatu, februari 20 mwaka huu katika ukumbi wa fikiri kwanza uliopo Usa River wilayani humo ,ambapo hadi jana wagombea wane kati ya sita walikuwa wamechukua fomu ,walirudisha.
Wagombea wa ccm waliojitokeza kuchukua fomu hadi sasa ni pamoja na ,William Sarakikya,Sioi Sumari,Elishilia Kaaya ,Elirehema Kaaya ,Rishiankira Urio na Anthony Musani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...