Mtoto wa aliekuwa Waziri Mkuu hayati Edward Moringe Sokoine, Mhe: Namelo Sokoine (MB) akipata maelezo ya jinzi gani kazi ya kuandaa Sanamu hizo ilifanyika kutoka kwa Padri wa kanisa katoliki Dakawa Drazan Klapez, kulia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine, Sarah Motosyo.
Mtengenezaji wa Sanamu ya Sokoine Ivan Klapez na Baba Padri Nikolas Saric wa kanisa katoliki Dakawa wakitoa maelezo kuhusiana na sanamu hiyo kwa Waziri Emmanuel Nchimbi na wananchi wengine waliohudhuria sherehe hizo.
Sanamu ya Sokoine ambayo ilitengenezwa kwa mawe yaliopatikana katika milima ya Iringa.
Waziri wa Habari na Michezo Dr Emmanuel Nchimbi akizindua Sanamu ya Sokoine kwenye viwanja vya kanisa Katoliki Sokoine Dakawa jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. duh...duh.....mhnuu!!!!!!napita jamani!

    ReplyDelete
  2. JAMANI HUYO MBONA KAMA SIO SOKOINE?

    ReplyDelete
  3. kuna mengine yanashushia viongozi heshima kwa kweli...doctor kweli doctor kweli aaah hayaaaa.

    ReplyDelete
  4. Inafanana na mchongaji mwenyewe, kasoro nywele.

    ReplyDelete
  5. Hah.. na nyie.. Dr. Kafanya nini jamani? Mbona picha inapendeza... weka wazi hii ni globu ya jamii...

    ReplyDelete
  6. Watanzania Bwana! Wameshindwa kusoma hata kuangalia picha imeshindikana. Huyo mzungu kachonga picha yake mwenyewe then anamdanganya hata Dr kuwa ni Sokoine neye anashindwa kutambua tofauti! Loooooooooo! hata mtoto wake mwenyewe Mhhhhhhhhh!

    Hii KALI

    ReplyDelete
  7. Muhimu:

    Ni kuenzi aliyoyafanya na kuyaacha Sokoine kuwa kama kigezo cha Uadilifu na Uongozi bora uliotukuka na sio gharama za Ujenzi kama huu!

    ReplyDelete
  8. Angalau mzungu kajaribu, lakini sanamu haifananii Edward Moringe Sokoine hata binti yake ameona hilo ;TAZAMA SURA YAKE!

    ReplyDelete
  9. Mbona picha kama ya mwanamke, haiendani kabisa na Edward mwenyewe! Kwani hii sanamu ilikuwa lazima itengenezwe kama watengenezaji hawakuwa na uwezo wa kutoa picha inayofanana na mwenyewe?

    ReplyDelete
  10. naomba niwe wazi , picha hiyo inabidi ishushwe na kuwapa kazi wanaoweza kutengeneza sanamu yenye mfano wa Mheshimiwa wetu (Hayati Sokoine) Pls! Pls!!! nakumbuka hata ya baba Nyerere Tanga ilikosewa na kurekebishwa so we need to do that as fast as ......

    ReplyDelete
  11. mbona hiyo sanamu iliyo simama kama ya makamba?

    ReplyDelete
  12. mh, yani huyo sio sokoine jamani bora ile sanamu ya kwanza hii ya pili sio kabisaaa! si mngemwambia tu ukweli kuwa amechakachua au kwa vile ni mzungu na binti naye kauchuna hivi hiyo sanamu inafanana na dingi wako kweli manake binti umechukua sura ya baba copy sasa mbona hufanani na hiyo sanamu hapo?!

    ReplyDelete
  13. Mbona sanamu ndefu inafanana na nyerere as opposed to Sokoine

    ReplyDelete
  14. itengenezwe ingine huyu si SOKOINE tunaemjuwa sisi mtu safi namba moja wa wakati ule

    ReplyDelete
  15. Maelezo chini ya picha yamekosewa , Sanamu ya marehemu Sokoine ni hiyo ya ukubwa mdogo Siyo hiyo ndefu, Nadhani mchongaji amejitahidi Maana hilo ni jiwe la Njombe ,nawashukuru kwa ukosoaji uliofanya nitambue palipokosewa. Hiyo ndefu ilikusudiwa Mwl Nyerere ila haikuwa sehemu ya uzinduzi.
    Dr Emmanuel Nchimbi

    ReplyDelete
  16. Asamnte mheshimiwa. Lakini hapo hatuono sanamu ya Mwalimu wala ya Mheshimiwa Marehemu Sokoine. kweli akichonga yako kwa jinsi hiyo utaikubali?
    Ombi: kazi iludiwe. Ni kweli ni jiwe la njombe lakini kazi iwe safi.
    Asante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...