Mtoto wa aliekuwa Waziri Mkuu hayati Edward Moringe Sokoine, Mhe: Namelo Sokoine (MB) akipata maelezo ya jinzi gani kazi ya kuandaa Sanamu hizo ilifanyika kutoka kwa Padri wa kanisa katoliki Dakawa Drazan Klapez, kulia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine, Sarah Motosyo.
Mtengenezaji wa Sanamu ya Sokoine Ivan Klapez na Baba Padri Nikolas Saric wa kanisa katoliki Dakawa wakitoa maelezo kuhusiana na sanamu hiyo kwa Waziri Emmanuel Nchimbi na wananchi wengine waliohudhuria sherehe hizo.
Sanamu ya Sokoine ambayo ilitengenezwa kwa mawe yaliopatikana katika milima ya Iringa.
Waziri wa Habari na Michezo Dr Emmanuel Nchimbi akizindua Sanamu ya Sokoine kwenye viwanja vya kanisa Katoliki Sokoine Dakawa jana.
duh...duh.....mhnuu!!!!!!napita jamani!
ReplyDeleteJAMANI HUYO MBONA KAMA SIO SOKOINE?
ReplyDeletekuna mengine yanashushia viongozi heshima kwa kweli...doctor kweli doctor kweli aaah hayaaaa.
ReplyDeleteInafanana na mchongaji mwenyewe, kasoro nywele.
ReplyDeleteHah.. na nyie.. Dr. Kafanya nini jamani? Mbona picha inapendeza... weka wazi hii ni globu ya jamii...
ReplyDeleteWatanzania Bwana! Wameshindwa kusoma hata kuangalia picha imeshindikana. Huyo mzungu kachonga picha yake mwenyewe then anamdanganya hata Dr kuwa ni Sokoine neye anashindwa kutambua tofauti! Loooooooooo! hata mtoto wake mwenyewe Mhhhhhhhhh!
ReplyDeleteHii KALI
Muhimu:
ReplyDeleteNi kuenzi aliyoyafanya na kuyaacha Sokoine kuwa kama kigezo cha Uadilifu na Uongozi bora uliotukuka na sio gharama za Ujenzi kama huu!
Angalau mzungu kajaribu, lakini sanamu haifananii Edward Moringe Sokoine hata binti yake ameona hilo ;TAZAMA SURA YAKE!
ReplyDeleteMbona picha kama ya mwanamke, haiendani kabisa na Edward mwenyewe! Kwani hii sanamu ilikuwa lazima itengenezwe kama watengenezaji hawakuwa na uwezo wa kutoa picha inayofanana na mwenyewe?
ReplyDeletenaomba niwe wazi , picha hiyo inabidi ishushwe na kuwapa kazi wanaoweza kutengeneza sanamu yenye mfano wa Mheshimiwa wetu (Hayati Sokoine) Pls! Pls!!! nakumbuka hata ya baba Nyerere Tanga ilikosewa na kurekebishwa so we need to do that as fast as ......
ReplyDeletembona hiyo sanamu iliyo simama kama ya makamba?
ReplyDeletemh, yani huyo sio sokoine jamani bora ile sanamu ya kwanza hii ya pili sio kabisaaa! si mngemwambia tu ukweli kuwa amechakachua au kwa vile ni mzungu na binti naye kauchuna hivi hiyo sanamu inafanana na dingi wako kweli manake binti umechukua sura ya baba copy sasa mbona hufanani na hiyo sanamu hapo?!
ReplyDeleteMbona sanamu ndefu inafanana na nyerere as opposed to Sokoine
ReplyDeleteitengenezwe ingine huyu si SOKOINE tunaemjuwa sisi mtu safi namba moja wa wakati ule
ReplyDeleteMaelezo chini ya picha yamekosewa , Sanamu ya marehemu Sokoine ni hiyo ya ukubwa mdogo Siyo hiyo ndefu, Nadhani mchongaji amejitahidi Maana hilo ni jiwe la Njombe ,nawashukuru kwa ukosoaji uliofanya nitambue palipokosewa. Hiyo ndefu ilikusudiwa Mwl Nyerere ila haikuwa sehemu ya uzinduzi.
ReplyDeleteDr Emmanuel Nchimbi
Asamnte mheshimiwa. Lakini hapo hatuono sanamu ya Mwalimu wala ya Mheshimiwa Marehemu Sokoine. kweli akichonga yako kwa jinsi hiyo utaikubali?
ReplyDeleteOmbi: kazi iludiwe. Ni kweli ni jiwe la njombe lakini kazi iwe safi.
Asante.