Wadau, jana jumamosi mimi nikiwa na rafiki zangu tulifika pale Baracuda Beach, KIgamboni mida ya saa tatu asubuhi kwa ajili ya mazoezi ya Kuogelea. Kwa bahati mbaya tukiwa pale, tukashuhuduia wavuvi wanavua amaki kwa kutumia baruti/mabomu. 

Tuliwasiliana na Askari mmoja ACP Khanga ambaye kwa taarifa zilizowekwa mahali mbali mbali ndiye msimamizi wa vikosi vya kwenye maji. Majibu aliyotupa ndiyo yalituchosha, akatushangaa kwa kutoa taarifa hizo na kutuuliza ni kipi kinachotushanganza. 

Tukapiga simu kwa polisi kigamboni, wakasema watashughulikia na mwisho tukampigia simu Kamanda Kova, ambaye nae alikuwa kwenye kikao na simu ilipokelewa na msaidizi wake na akaahidi kuwa itashughulikiwa. Baadae sana Kamanda Kova ailipiga simu yeye mwenyewe wakati tayari wavuvi wale walishaondoka kwenye maeneo hayo. 

Sasa kwa hali kama hii wananchi wakichukua sheria mkononi watalaumiwa kweli? Baracuda Beach imekithiri kwa vitendo hivi na iko takrbani kilometre chache toka Ikulu ya Tanzania. Hali itakuwaje huko Misungwi, Mwanza?
MDAU KIGAMBONI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Pole sana mdau mzalendo wa nchi hii. Tatizo ni moja hukujua kuwa hao wavuvi ni watu wa hao uliowapigia simu tena inaonekana wanasimamiwa na huyo ACP Khanga. Hii ndiyo bongo bwana. Nakushukuru hata kwa ujasiri wako wa kutuletea mada hii. Mimi ningekuwa Rais wa nchi hii ningenyonga watu wengi sana ili ifike mahali watu tuwe serious na maaendeleo ya nchi yetu. Nacho kuomba MUNGU akipenda 2015 tuwahimize watu watumie kalamu zao vizuri kwenye uchaguzi.

    ReplyDelete
  2. Hili jeshi letu la polisi linahitaji 'rais kichaa'2015 aje kulioverhaul.

    Kwa wale baadhi tunaoendesha magari kupitia mbuga za wanyama ngorongoro na serengeti maeneo ya ,Naabi,Seronera,Ikoma,Ndabaka sina uhakika na games/parks zingine wakakubaliana na mimi,kuna wale askari wa porini wale("magema" kwa jina maarufu)..Wale askari huwa wanachukua mavunzo yao chuo gani?..Wale jamaa wako 'disciplined' ni balaa na ni wakali na hawapokei rushwa,wakisema utaratibu ni huu hapa hata kama una milioni ngapi hawapokei..kwa ufupi hawapokei rushwa na wako strick,ukiambiwa umeoverspeed na fine ni 100,000 utailipa tu.Lia..toa machozi utailipa tu..¨Wakisema njia imefungwa utazunguka hivi utazunguka tu.wala usipoteze muda kulalamika.nk.Point yangu ni kwamba labda badala ya hawa polisi kwenda hicho chuo cha Moshi wapelekwe kwenye hivi vyuo vya hawa askari pori.Mwema umechemka Bwashee..tutakutana Kilanya aise!!

    David V

    ReplyDelete
  3. Hii nchi inachosha especially hilo jeshi la polisi. Huyo jamaa sijui ndiye Kanga hawezi kufuatilia kwani ana hesabu yake ya siku toka kwa hao wavuvi. Au mtu anategemea tufikirie nini?
    Kibongobongo mtu akipewa kitengo chenye maovu mengi basi huwa ni mradi amekabidhiwa. Same kwa wanaosaini mikataba ya madini, wanaouzia wazungu ardhi na kuacha wananchi wakifukuzwa kwao mfano Loliondo n.k.
    It is a shame!

    ReplyDelete
  4. Hongera mdau kwa kuchukua hatua kama hizo. Umetimiza wajibu wako, na kila Mtanzania akitimiza wajibu wake kwa namana yako, hakika tutapiga hatua.

    ReplyDelete
  5. KWA KWELI HII NCHI INAHITAJI MWENDAWAZIMU,HUWA NAWAAMBIA WATU KWAMBA TUNAHITAJI CHIZI MMJOA AJE KUWANYONGA WATU KAMA MDAU WA KWANZA ANAVYOSEMA,WATU HUWA WANANISHANGAA NIKISEMA HIVYO ILA KWA KWELI NCHI INA WAJINGA WENGI SANA..HUKU WATU WANVUA SAMAKI KWA MABOMU,KULE MAZIWA FEKI YA WATOTO YANAINGIZWA WATU WANAKUFA,WENGINE WANAPEWA SUMU WAFE WASIONGEE UKWELI..HIVI TUNAISHI NCHI YA NAMNA GANI?

    ReplyDelete
  6. Very well reported, i hope the authorities take action...

    ReplyDelete
  7. Aa tatizo hatuna uhakika kwamba hapo ni comoro au tanzania au shelisheli kwasaabu membe mwenzako ametia saini ya kugawa eneo la bahari yetu kwa upya na mpaka wa bahari yetu unaishia wapi kwa sasa anayejua ni bw.membe.

    ReplyDelete
  8. Ndio yale yale aliyosema Mwakyembe jana kuhusu jeshi la polisi la Tanzania - Kwa kweli jeshi la polisi linahitaji overhauling kama wadau mliosema hapo juu. Ukweli nikuwa hakuna uzalendo tena katika nchi yetu na wazalendo wachache waliobaki wanaonekana kama taahira.

    ReplyDelete
  9. TUMELALAMA WAPI ILIYOPO SASA, TUNAONEWA,TUNAUWAWA UWIIIII!

    ReplyDelete
  10. Kaka hiyo haliipo eneo lote tokea fukwe ya Ikulu, seaview,cocobeach hadi seacliff...mimi ninakaa seaview na nina ofisi oysterbay nashuhudia kila siku na tumetoa taarifa mpaka tushachoka

    ReplyDelete
  11. Yaani wewe unaihofia Ikulu?

    Mimi nililazwa kipindi fulani pale Ocean Road mtoto wangu alikuwa ana cancer, nikaangalia kwa haraka aharaka watoto wengi waloletwa pale ukiondoa wachache kama mwanangu ambae alikuwa na tatizo ya cancer nyingne ni kwamba, wengi wao wanatokea Pemba, Mwanza, Shinyanga... haraka haraka nikagundua kuwa Pemba itakuwa tu uvuvi haramu wa kuvua na mabomu ndio unaathiri w\atoto wanaozaliwa wakati mama zao wakiwa waja wazito imma wanakunywa maji yanayotokana na uvuvi haramu au samaki wanaovuliwa na mabomu.

    NA wale wa Shinyanga nadhani ni yale maeneo watu wanapochimba dhahabu na maji kutiririka hovyo yaani ni mfasno wa hayo! serikali inatakiwa kufanya research sehemu hizi kugundua chanzo cha cancer hizi za watoto wengi wengi wengi kutokea maneneo hayo! kwa hiyo ndugu yangu sio tu Ikulu itadhurika ni kwamba WATOTO WANADHURIKA NA UVUI HUO !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...