Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,Balozi Khamis Kagasheki (wa tatu kutoka kulia mwenye miwani) akishirikiana na viongozi wa Usalama barabarani pamoja na viongozi wa Club ya Rotary ya Dar es Salaam kubandika machapisho ya Usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na Club ya Rotary yenye ujumbe wa kuhakikisha kuwa madereva wanaendesha kwa usalama zaidi bila kutumia siku za mkononi.Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mh. Mohamed Mpinga, muwakilishi kutoka Club ya Rotary Dar es Salaam,Bw. Zainul Dossa pamoja na Bw. Hamza kassongo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Balozi Kagasheki akishirikiana na viongozi wa usalama barabarani akibandika machapisho ya usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na Club ya Rotary ya Dar es Salaam kulia ni kamanda Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mohamed Mpinga, kushoto ni Afisa uhusiano wa kampuni ya Airtel Bi. Jane Matinde akishuhudia zoezi hilo.
Kamanda Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mohamed Mpinga,akibandika machapisho ya usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na club ya Rotary yenye ujumbe wa kuendesha +simu =kifo kuhakikisha kuwa madereva wanaendesha kwa usalama zaidi, kulia ni ni Afisa uhusiano wa kampuni ya Airtel Bi. Jane Matinde akishuhudia zoezi hilo.
Afisa uhusiano wa kampuni ya Airtel Bi. Jane Matinde akizungumza na vyombo vya habari wakati wa zoezi la kubandika machapisho ya usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kushirikiana na Club ya Rotary yenye ujumbe wa kuendesha +simu = kifo kuhakikisha kuwa madereva, zoezi hilo limefanyika jijini Dar es Salaam.

Serikali imesema kutokuwepo kwa sheria ya barabarani inayozuia matumizi ya simu za mkononi wakati wa uendeshaji wa vyombo vya moto kunachangia kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria madereva ambao wanaonekana kutumia simu za mkononi huku wakiwa wanaendesha vyombo hivyo.

Hayo yamesemwa na naibu waziri wa mambo ya ndani Balozi Hamis kagasheki wakati wa zoezi la kubandika ujumbe katika magari mbalimbali unaokataza matumizi ya simu za mkononi wakati wa kuendesha vyombo vya moto.

Ni kweli hadi sasa hakuna sheria inayomkataza moja kwa moja dereva kuacha kutumia simu awapo barabarani lakini naomba wananchi wafahamu kuwa hili linafanyiwa kazi na wafuate maelekezo yalioyotolewa na wadau kama hawa ambayo kiukweli yanatoa elimu ya kupunguza madhara ya ajali za mara kwa mara” alisema Balozi Khagasheki kwa mujibu wa tathmini ya jeshi la polisi baadhi ya ajali nyingi zinazotokea barabarani zinatokana na matumizi ya smu za mkononi wakati wa kuendesha vyombo vya moto hali inayopelekea kuongezeka kwa ajali nyingi na kusababisha vifo ambavo vingeweza kuzuilika kwa urahisi.

Balozi kagasheki amesema kuwa upungufu wa kutokuwa na sheria ya kuzuia matumizi ya simu za mkononi wakati kuendesha gari unapelekea kushindwa kuwachukulia hatua kali madereva ambao wanaonekana kufanya hivyo.

Naye muandaaji wa zoezi hilo Zeinul Dossa kutoka klabu ya Rotary ya jijini dare s salaam pamoja na Jene matinde afisa uhusiano wa kampuni ya smu za mkononi ya Airtel wamesema kuwa zoezi hilo la kubandika ujumbe huo litafikisha ujumbe kwa madereva wengi pamoja na kupunguza ajali.

Zaidi ya machapisho elfu 5 yametengenezwa kwa ajali ya kubandika pamoja na kusambazwa katika magari mbalimbali ambayo yatarahisisha kupunguza ajali za barabarani ambazo zinaweza kuzuilika kwa kshirikiana na jeshi la polisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mmefika ubungo manzese mbagala mwenge na pembezoni au kampeni katikati ya jiji tu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...