Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati wa halfa fupi ya uzinduzi wa huduma mpya inayomwezesha mteja kununua mboga kwaajili ya familia kupitia huduma ya Airtel money inayotelewa na Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya Stake Agrobase International limited. Wanaoshuhudia toka (kulia) ni meneja wa Airtel money Asupya Nalingingwa na Afisa Mauzo wa SAIL bwana Daniel Kimati (kushoto).
Afisa Mauzo wa SAIL bwana Daniel Kimati akiongea na waandishi wa habari wakati wa halfa fupi ya uzinduzi wa huduma mpya inayomwezesha mteja kununua mboga kwaajili ya matumizi ya nyumbani kupitia huduma ya Airtel money inayotelewa na Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya Stake Agrobase International limited. Wakishuhudia katikati ni Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akifatiwa na meneja wa Airtel money Asupya Nalingingwa.
Waandishi wa habari wa vyombo vya habari tofauti wakishuhudia uzinduzi wa huduma mpya inayomwezesha mteja kununua mboga kwaajili ya familia kupitia huduma ya Airtel money inayotelewa na Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya Stake Agrobase International limited katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya kampuniya Airtel Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. i just wonder kama hii ina faida or makes any difference!!

    ReplyDelete
  2. Mambo mengine mnayo zindua niya upuuzi bila kuyafanyia uchunguzi tena haingii akilini kwa mazingira yetu ya Tanzania bado atujafikia hali hiyo kununua vitu na kuletewa nyumbani kwanza ubabaishaji mwingi wizi kukosa uhaminifu ujanjaujanja kwa nini nisiende mwenyewe sokoni nikanunua mboga .ila kama mnataka mwonekane kwenye vyombo vya habari kitu chochote unaweza ukakizindua

    ReplyDelete
  3. I'm confused! Do we really need this? Nafikiri mwisho wa siku tutakuwa tunasambaza pesa toka mtandao mmoja kwenda mwingine.

    Inarahisisha?...nini?

    Ni kitu kipya?... inasaidia nini?

    Tuna tatizo ambalo hii inatatua?

    Seriously, kuna mtu alishawahi kuibiwa pesa (less than tsh 5,000 )akienda kununua matunda au mchicha?

    Au ni njia ya kuwanufaisha kwa kukatwa pesa tunazozitafuta kwa nguvu zote.

    Considering that network zina JAM kila wakati naweza hata kushindwa kununua Mbogamboga familia ikalala njaa.

    Sipati picha. mnisaidie hapa.

    ReplyDelete
  4. hahaaa, afadhali na nyie mseme! siku hizi kampuni za simu zimezidi kuzindua promo uchwara! waandishi kipindi cha neema sasa . . . press conference kwanza kisha vibahasha.. Mungu awape nini zaidi?

    ReplyDelete
  5. Acheni watu imaginative wajaribu vitu vipya. Wapo wataotumia hii service - hao waendelee. Kama we hutaki, acha, what is your problem?

    ReplyDelete
  6. Itamfikiaje mlaji kwa sababu hata anuani za mitaa yetu hazijulikani, miji na viji vyetu hazijawa tayari kwenye google map angalau tungeweza kusema ingefanikiwa kwamba mtu anaweza tumia GPS kupeleka hizo mboga kwa mteja. Halafu hao wanaojiita Stake Agrobase Int wamesambaa kiasi gani hapa Tz? Hii ni kuuza sura tu kwenye vyombo vya habari na kutafuta umaarufu kila kitu mnazindua hiki leo hiki kesho hiki wala sioni lolote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...