Bi Margreth “Kanyamale” Laban Mwaijibe/Njwaba
 (Kafariki Tarehe 18/12/2011)

Kwa niaba ya Familia ya Mzee Laban Mwaijibe/Njwaba, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wote ambao kwa njia moja au nyingine, walishirikiana nasi katika kumuuguza Ndugu yetu Margreth (Kanyamale) Laban Mwaijibe, na hatimaye katika msiba wake Sinza, Dar es Salaam na mazishi nyumbani kwake Lugombo, (Kilosa Mission) Mwaya, Kyela Mbeya tarehe 20.12.2012.

Kwa namna ya pekee, tunapenda kuwashukuru sana Ndugu, Marafiki, Majirani na Jamii nzima kwa ujumla pamoja na Mchungaji Mwakyusa wa Kanisa la Moravian, Mburahati pamoja na washirika wote kwa huduma ya neno la kiroho.

Vile vile tunapenda kulishukuru Kanisa la Moravian Kilosa Mission na Wanakijiji wote wa Kilosa Mission kwa mapokezi makubwa ya mazishi.

Tulineemeka kwa Sala na Maombi yenu, pia tulifarijika kwa Upendo na Misaada yenu. Daima tutakumbuka wema na upendo wa kila mmoja aliyemhudumia Marehemu Ndugu yetu Margret na wote walioshirikiana nasi wakati wa msiba.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe. Amen.

Kwa taarifa zaidi: 0754 311315

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...