Ajali mbaya sana imetokea jana majira ya saa tisa/kumi katika eneo la Mbande Mkoani Dodoma, Njia Panda ya kuelekea Kiteto ikihusisha magari matatu,likiwemo Lori aina ya Scania, Toyota Mark II na Toyota Carina ambayo ndio iliyoharibika vibaya san na kusababisha watu wawili wamepoteza maisha papo hapo.Chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni gari hiyo aina ya Toyota Carina ilikuwa ikijaribu kuovertake Gari nyingine aina ya Toyota Mark II huku mbele kukiwa na hilo Lori aina ya Scania,hali iliyompelekea dereva gari hiyo aina ya Carina kushindwa kulipita lile gari lingine na kujikuta ikiigonga ile gari nyingine na kwenda kujipiga tena kwenye Lori hilo.Abiria waliokuwemo kwenye hiyo gari aina ya Toyota Carina ndio waliofariki papo hapo ambapo mmoja alikuwa ni mgonjwa na alikuwa akikimbizwa hospitali (kwa mujibu wa mtoa taarifa) huku deveva ambaye alionekana kuwa ni mzima aliwahishwa hospitali kwa matibabu ya haraka.
Hii ndio gari aina ya Toyota Mark II inavyoonekana baada ya kugongana na hiyo gari nyingine
Mmoja wa wasamalia waliofika katika eneo la tukio akijaribu kuangalia kama anaweza kuwatambua Marehemu waliokuwemo kwenye gari hilo.
That's Jesus.
ReplyDeleteInna lillahi wainna illaihi rajiun. Ajali ajali ajali... mpaka lini jamani? madereva msiwe na haraka jamani! pole sana wafiwa huyu mzee ni Baba wa rafiki yangu. Insha allah Mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahala pema peponi.
ReplyDeleteWhy but why?
ReplyDeleteKila ukiona picha za magari yaliyopata ajali Bongo, waona magari hayo yamebomokabomoka vibaya sana kama vile hayakuwa yametengenezwa kwa bodi za chuma.Yanavunjika kama mitungi ya maji.
Yaani.
ReplyDeleteAliyefariki hapo hapo ni pamoja na Alfan Shams, mjasiliamali maarufu Shelui na ni mtu wa watu, ni mwema sana na nimewahi kushuhudia wema wake akinifanyia mwenyewe. ana asili ya Kiarabu ila narudia tena ana roho nzuri sana.
Habari nilizopata ni kwamba, alienda Dar kumzika Bibi yake, wakati wa kurudi, akafika Dodoma akiwa na Mdogo wake na Wajomba zake wawili, wakapigiwa simu kuwa Kaka yao Dar naye amefariki. wakarudi na hio Carina (waliacha Prado Dodoma), mdogo wake akiwa anaendesha... ndio yakatokea hayo tunayoshuhudia.
Mungu awapokeee na awape nguvu Familia na watoto wake Wanne, Youngest around 12!
mungu awalaze mahala pema peponi,na wafiwa haswa mama mzazi wa aliyefiwa kabla ya siku4 mwanae na leo mwanae na ndugu 2 na mama mzazi kabla ya wiki kama 3 hivi ,mola ampe subra kwani ni mtihani mkubwa sana.inalilah waina ilah rajiun .kwa kweli umetuuma sana ni msiba wetu wote
ReplyDeletemola awalaze pema peponi
ReplyDeleteMungu awape faraja jamaa,marafiki wa marehemu.
ReplyDeletePoleni sana wahusika na msiba!!!
ReplyDeleteBarabara za masafa marefu na hata za mijini inabidi waongeze lane nyigine kila upande au angalau moja ya kati ya kwezesha magari yaendayo kasi kupita magari yanayoenda polepole.
Watu watakufa sana kwa mtindo wa barabara za njia moja kila upande.
Makongoro Wassira
inna lilah wainna ilaihi raajioun, hakika mola wetu ni mpangaji wa kila jambo hakuna cha kusema zaid ya kumshkuru yeye kwa kusema ALHAMDULILAH..
ReplyDelete