Habari Ankal,
Leo maeneo ya Tegeta katika Junction ya kwenda Kiwanda cha cement cha Twiga (wazo Hill), imetokea ajali ambayo imeihusisha lori lilibeba kifusi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya new bagamoyo. Lori hilo lilikuwa linatokea maeneo ya kiwanda cha cement cha Twiga likiwa limejaza kifusi.
Wakati linashuka kuelekea junction ya bagamoyo road, break zikakatika. kilichotokea ni lori kumgonga mtu mmoja ambaye alifariki papo hapo, halafu likaruka barabara na kwenda kuigonga pick up iliyokuwa imepaki pembeni na almanusra iingie katika duka.
Kutoka kwa mdau wa Tegeta.







very sad
ReplyDeletemalori hayo yameoza,watoa tender lazime mkague magari hayo kabla
ReplyDeleteHili Lorry linaonekana wazi halikutakiwa kuwepo barabarani, lakini kama kawaida ya vyombo vya dola na wamiliki wa hii mitego ya mauti wanaangalia maslahi yao. Hivi tutaendelea kupoteza maisha ya watu kwa ubinafsi wetu mpaka lini?
ReplyDeleteLorry drivers coming down that hill do not take precautions mostov the times. This isnt the 1st time it has happened.
ReplyDeleteBy underestimating a small hill and overtrust your so-called "brakes" ths is what usually results.
siamini brake zilikatika, bali gari halikuwa na brake.dereva alishazoea kuliendesha kijanja ila siku hiyo likamzidi nguvu.
ReplyDeleteHiyo gari ingekua barabarani kweli?
ReplyDeleteduh poleni sana,tatizo la hapo njia panda ya wazo kwa hizi ajali limekuwa sugu,ni kila wakati,na pia ubovu wa magari hayo malori umekuwa sugu kabisa,ni kila wakati ajali zinatokea hapo
ReplyDeleteMaroli mengi yanayobeba mchanga, kokoto, mawe na kifusi kwa kawaida ni mabovu sana na yanaendeshwa na vijana wadogo wenye uwezo mdogo wa kufanya maamuzi ya busara. Polisi inabidi wachukue hatua mapema kabla ya maafa.
ReplyDeleteangalia vipara vya matairi! tanzania hatuogopi kufa!
ReplyDeleteTena hili lori linaonekana ni kongwe mno ni kuliko miaka 40 i am sure!
Haya malori yabadilishiwe ruti yawe yanaingilia boko na sio njia hii maana ajali aziishi, na trafiki kibao wapo njia ile kazi kupokea hongo tu bila kujali ubora wa haya malori.
ReplyDelete