Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiufungua Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wapanda Mapiki Piki wa CCM hapo ukumbi wa Mikutano wa CCM Mkoa uliopo Amani Mjini Zanzibar.Kulia ya Balozi ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Mjini ambae pia ni Mbunge Viti Maalum Mh. Tauhida Gallos Nyimbo na Kulia ya Balozi ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mjini Magharibi Nd. Yussuf Mohd Yussuf.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi amewataka Wanachama wa Umoja wa Wapanda Mapiki Piki wa CCM kufanya maamuzi Magumu lakini ya Busara katika kuhakikisha wanachagua Viongozi bora kwa ajili ya kujenga safu ya Ushindi wa chama hicho kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Ametoa wito huo katika Mkutano Mkuu wa Umoja huo uliokutana kufanya Uchaguizi wa Viongozi wake watakaoongoza Umoja huo katika kipindi cha Miaka mitano ijayo hapo katika Ukumbi wa CCM Mkoa Amani Mjini Zanzibar.

Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema CCM iliwahi kupata uvamizi ndani ya Jumuiya na Baadhi ya Taasisi zake na hatimaye kupelekea Matatizo hasa katika chaguzi zilizopita.

Alitahadharisha kwamba wakati umefika kwa Wanachama wa Chama hicho kuwa makini na watu kama hao hasa katika kipindi hichi kinachoingia cha chaguzi mbali mbali za Viongozi wa Chama hicho.

“ CCM haioni shida kupoteza wanachama watatu, watano ambao wana tabia na njama za kukidhoofisha Chama kwa maslahi yao binafsi”. Alisema Balozi Seif.

Balozi Seif amewaomba Vijana hao kujisaidia katika kuachana na mifarakano kwa lengo la kutengeneza safu nzuri ya muelekeo bora wa Uongozi makin.

Akiwapongeza Vijana hao Balozi Seif aliwaomba kuendelea kukiimarisha Chama chao kwani wao ndio nguvu ya Chama wakati wote.

Balozi Seif ameahidi kwamba kwa kushirikiana na mlezi wa Umoja huo ataangalia hatua za namna ya kuisaidia Taasisi hiyo muhimu kwa CCM katika masuala ya uhamasishaji Wanachama.

Katika Taarifa yao iliyosomwa na Katibu wa Umoja huo wa wapanda Mapiki Piki Mkoa Mjini Magharibi Nd. Amour Ali Mwinyi amesema Umoja huo umepata mafanikio makubwa tokea kuanzishwa kwake.

Hata hivyo Nd. Amour alisema Taasisi yao bado inakabiliwa na baadhi ya changamoto zinazokwaza utendaji wao ikiwa ni pamoja na msingi wa kianzio cha kuelekea katika uzalishaji mali.

Mapema Mlezi wa Umoja wa Wapanda Mapiki Piki Mama Asha Suleiman Iddi amempongeza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni kwa jitihada zake za kuunga mkono umoja huo.

Mama Asha ameziasa Taasisi za CCM zinazoingia kwenye uchaguzi kuwachagua Viongozi wao kwa kigezo cha Uwezo na kuachana na tabia ya kuangalia udugu au rafiki.

Alisema tabia hiyo ikiendekezwa inaweza kukijengea mazingira mabovu Chama katika utekelezaji wa Sera na Majukumu iliyojipangia ndani ya Ilani yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kuchagua viongozi bora sio uamuzi mgumu. Iwe jambo la busara na kawaida kuwachagua viongozi bora.

    ReplyDelete
  2. Naona hizi jumuiya hazijakamilika bado ndani ya chama. kwani zawapanda baiskeli,wavuta mikokoteni,wapanda punda, farasi,waendeshao magari na wapiga debe, waendao kwa miguu, na wengineo sijawasikia wakivuma katika chama wala kutafutiwa viongozi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...