Uncle Mithupu habari yako bwana.
naomba utoe habari hii watanzania waone jinsi vyombo vyetu vya usalama vinavyotumia vibaya magari na vifaa vya kazi wanavyopewa vilivyonunuliwa kwa kodi zetu.Hiyo gari yenye plate number STK leo mchana mida ya saa saba kasoro imenigonga kwa nyuma nikiwa na gari yangu aina ya Toyota Carina ti nikiwa nafika hapo Gold star ofice ndogo za tigo.Huyo askari magereza aliekuwa anaendesha gari hilo alikuwa spidi mbaya akiwa anakata kona ya co-cabs akakutana foleni ghafla akanigonga nyuma kwa nguvu nikaenda kuigonga gari ya mbele yangu kama unavyoona hizo picha hapo.Askari huyo akataka kukimbia nikamzuia hapo na kmuita trafiki apime.Reaport iliyoandikwa hapo nilitamani nilie maana imeingizwa siasa na kuonekana jamaa hana makosa eti trafick anaandika reaport twende mahakamani.Nikaona hapa hizi siasa nimeshagongwa bado nikapigishwe kwata la kwenda mahamani na gari ikapaki centro kunguru wainyee pale iendelee kuoza? na bado reaport imeshachakachuliwa,Bosi wangu nampa taarifa anaona nadaiveji nimeenda kwenye ishu zangu sasa na huko mahakani ntaenda jumapili isiyo siku ya kazi?.nikaamua nikokote kamkokoteni kangu niondoke, Hapa ankal na deni la kumlipa jamaa wa mbele + nirekebishe kisoteo changu kweli nchi hii bado hatuja pata uhuru.
Mbeba box wa dar.
 KBUUUUMMMM.....
inabidi nikaripee hasara hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. ulichukua uamuzi wa maana kamanda. mshikaji wangu aligongwa nusu afe halafu ule mchoro ukageuzwa ili yeye aonekane ana makosa ili huyo mwenye hiyo gari nyingine (ambaye anazo za kutesea mjini) alipwe gari mpya na bima. Akiwa anasubiri huyo aliyemgonga amlipe akashtukia anapelekwa mahakamani kesi inasomwa fasta, unatolewa mchoro ambao umeeditiwa na yeye ndiyo mzumbe sana hukumu ikasomwa siku hiyohiyo aende jela miezi 3 au alipe fine. akalipa fine nimesahau hata ilikuwa sh. ngapi. toka siku hiyo nikapoteza imani kabisa na hawa askari wetu.

    ReplyDelete
  2. Kosa ni la STK 5905m hakuna cha ubishi wala nini, yeye ndo kagugonga na alisababisha wewe umgonge wa mbele yako.

    ReplyDelete
  3. kwa nn umeogopa kwenda mahakamani, ndio sheria kule mahakamani hata kama ww ndio mwenye kosa usingepata gharama ya kutengeneza hayo magari, kila gari itashughulikiwa na bima tatizo ww mwenyewe umetaka short cut. acha kulaumu mtu

    ReplyDelete
  4. Kwani huna bima?

    ReplyDelete
  5. na kuendesha gari ni lazima ukiwa nyuma ya gari la mbele yako UONE BARABARA CHINI UNAPOSIMAMA PIA NA WAKATI WA KUENDESHA NA KWENYE FOLENI.

    tatizo la wabongo wanasogeza magari bila kufikiria kuwa ukigongwa nyuma basi utamgonga wa mbele.

    Ndio ni lazima wewe ulipie matengenezo la gari la mbele yako, then next time acha kuwa karibu na magari.

    Pole kwa uhuni wa hao maaskari. Watu wengine najua huwa wanapiga picha na kuchukua insurance details za wa gari la nyuma na kwenda kuweka madai, hii ukiwa na picha insurance ya hilo gari lazima washughulikie na hiyo ya wao kuchakachua ni vigumu.
    Mie ningewapiga picha wote kwa kweli.

    Ila tafadhali sana mkiwa mnaendesha magari muwe mnaacha nafasi ni muhimu sana. najua kuna kakujisahau tukiwa tunaendesha ila hii n muhimu sana pia kuokoa kupoteza mapesa na bima kuwa kubwa siku ingine esp wakati wa renewal.

    ReplyDelete
  6. Sasa wewe ulitaka trafiki atoe hukumu gani? Taratibu ni kwamba nyie wenyewe mnatakiwa muelewane ikishindikana, polisi anandika maelezo halafu hakimu ndie anaamua nani mwenye makosa. Huu mchezo wa kuwageuza polisi mahakimu ndio chanzo cha rushwa. Unachotueleza wewe ni stori yako, na mwenzako nae ana stori yake, ndio maana hakimu anatakiwa atoe uamuzi baada ya kuwasiklizeni wote. ACHA JAZBA, DEREVA MZURI NI YULE ANAYEFIDIA MAKOSA YA WENZAKE.

    ReplyDelete
  7. Mbona ni ajali ya kawaida ulevi umetokea wapi hapo? Najua magari mengi ya serikali yanatumika vibaya lakini kisa cha mdau hakijakidhi viwango katika kueleza hilo.

    ReplyDelete
  8. usijiingize gharama za bure ndugu yangu BIMA unayolipia kazi yake ni nini?

    ReplyDelete
  9. Sasa wewe ulitaka trafik ikishapima akupe pesa uende ukalale na mkeo Serena Hotel? hueleweki! Mahakama ndio inaditamini haki!

    ReplyDelete
  10. HII AJALI NIMEIONA NIKIWA UPANDE WA PILI,POLE ULIYEGONGWA LAKINI UKWELI UPO PALE PALE YULE ASKARI ALILEWA,HATA NINGEKUWA MIMI NIENDE KUPOTEAZA MUDA MAHAKAMANI HUJUI KESI ITACHUKUA MIEZI MINGAPI,TATU MUDA WA KILA MARA KUHUDHURIA HIZO MAHAKAMA INATIA TABU,HONGERA KWA UAMUZI WAKO NI SAHIHI ULIYVOAMUA

    ReplyDelete
  11. Ulitumia kipimo gani kupima kwamba askari alikuwa kalewa? Unaongelea haki, wewe umemtendea haki gani huyo askari?

    ReplyDelete
  12. Ndugu zangu acheni kumdanganya huyu bwana aliwezaje kupiga picha gari aliyoigonga yeye kwa nyuma akashindwa kupiga picha gari la STK likiwa limemgonga??pia sheria iko pale pale ukigonga kwa nyuma unashitakiwa kwa hiyo uyo wa STk atashitakiwa lakini na wewe unashitakiwa basi

    ReplyDelete
  13. Mimi kidogo nina tatizo na hizo picture za ajali yenyewe, hebu wadau ziangalieni uzuri hizo Picture ya gari tuliyowekewa ya Stk 5905 haioneshi kabisha kama ni gari ilogonga gari nyengine kwa nyuma haina hata scrath na kama ingegonga kweli nayo ingeumia pia, ikiwa ilogongwa imeweza kumpiga wa mbele yake hadi akabonyeza bumper hebu tusaidianeni jamani. Au picture ilipigwa kabla ya ajali?

    ReplyDelete
  14. POLICE HANA KOSA, KAZI YAKE NI KUSIMAMIA USALAMA NA KUFIKISHA SHAURI HILO MAHALA PANAPOHUSIKA, YEYE AMEANDIKA KWENDA MAHAKAMANI AKIJUA KABISA YEYE HANA MAMLAKA YA KUTOA HUKUMU SAS WEWE ULITAKA POLICE AFANYE NINI, AMLIPISHE FAINI AMBAYO INAINGIA SERIKALINI ALAFU WEWE HUPATI KITU AU ULITAKA AFANYE NINI?HAPA UMEJIHAIBISHA MWENYEWE MDAU KWA KUSHINDWA KUELEWA KWAMBA MAHAKAMA NI CHOMBO CHA KUDAI HAKI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...