Mmoja wa Wafanyakazi akielezea tukio lilivyokuwa.

Muonekano wa nje wa Royal bakery mara baada ya Camera ya Jiachie ilipowasili eneo la tukio usiku huu na kukuta difenda ya polisi kutoka kawe ikiwa imewasili eneo hilo,wakati huo huo kukiwa na heka heka za hapa na pale.

Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Royal Bakery hiyo ameeleza kuwa tukio la kuvamiwa na majambazi eneo hilo imetokea mnamo majira ya saa 3 na ushehee hivi (usiku huu),anasema majambazi hao walikuwa watano waliwasili eneo hilo wakiwa na piki piki mbili na gari. Mmoja aliyekuwa ameshika bastola aliingia ndani na kuwaamuru wafanyakazi waliokuwemo ndani wote walale chini,na kuanza kuchukua fedha za mauzo zilizokuwemo kwenye droo zao za kuhifadhia fedha,huku wengine nje wakifyatua risasi hewani na kufunga barabara kwa muda wa dk 10 hivi.

Dada huyo aliyejikuta akiangua kilio wakati akielezea,anasema kuwa yeye amepigwa pigwa makofi na hakujeruhiwa,kama vile haitoshi anasema kuwa eneo hilo pia kulikuwepo na wazungu wapatao watatu ambao walienda pale kujipatia huduma mbalimbali,kwa bahati mbaya wakakutana  na dhahma hiyo,ambapo nao walilazwa chini na kuporwa wallet zao sambamba na pete zao walizokuwa wamevaa mikononi,baada ya ambush hiyo majambazi wakatoweka kusikojulikana ndipo difenda ya polisi ikawasili na kuanza kuchukua maelezo kadhaa kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa bakery hiyo.
Askari wa kituo cha Kawe,wakichukua maelezo kwa baadhi ya wafanyakazi wa bakery hiyo,namna tukio lilivyokuwa,mmoja wa wafanyakazi aliyenaswa vibao akilia kwa uchungu.

Masikini Dada wa watu akilia kwa uchungu,huku polisi wakiendelea kuchukua maelezo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Bakery hiyo wakiwa wameduwaa wasijue la kufanya kwa muda huo mara baada ya majambazi kupora kiasi cha fedha ambazo haikuweza kubainika mara moja ni kiasi gani mpaka Camera ya Jiachie inaondoka eneo la tukio usiku huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Kama kuna CCTV za Nje wafatilie mpaka Nyuma hiyo Milio ya bastola Jeshi hawakusikia? Basi watalaumiwa wafanyakazi na maboss wao.Wanajeshi nao tunawawekea mashaka. MJ

    ReplyDelete
  2. Jamani hapo pembeni si kuna makao makuu ya Jeshi, iweje barabara ifungwe kwa dk 10 wao wasijue, daah kweli bongo tambarare...

    ReplyDelete
  3. SASA NINYI WATANZANIA HUKO INAKUWAJE KWENYE DUKA KUBWA KAMA HILO HATA CAMERA HAKUNA? HII NI DUNIA YA YA KISASA LAZIMA SECURITY CAMERA ZIWEKO KWENYE KILA BIASHARA YA KUINGIZA PESA! AU TATIZO HUWA NI UMEME?, SASA UTAWALA WA KIKWETE LAZIMA UBADILISHWE HAIWEZEKANI KILA SIKU NI MAJAMBAZI TU NA SILAHA NA HAKUNA YEYOTE ANAESHIKWA KWA MATUKIO KAMA HAYO , TANZANIA SASA TUNAENDA KUBAYA

    ReplyDelete
  4. Poleni wahusika..walifunga baraX2 kwa dakika 10?? Kama ni kweli walifunga njia kwa muda huo wote wakipiga risasi watakuwa ni wanajeshi hao,maana dk hizo ni nyingi sana..au mwandishi umeongeza chumvi kwenye dk hizo??dk 10??

    ReplyDelete
  5. USALAMA WA RAIA HAKUNA KABISAAAA, WACHA TUENDELEEE KUPIGWA BARIDI NA KUBEBA MABOKSI TU, NA HAO WAZUNGU WANAKUJA KUÍNVEST MNAWAIBIA HADI PETE NA PESA HAYA WAKIACHA KUJA MUANZE MALALAMIKO OOH UTALII HAULETI PESA OOH SIJUI NINI. NCHI INGEUZWA TU HII, TENA KWA SALE KUBWA KABISA

    ReplyDelete
  6. swali hakuna camera humo ndani ya bekary inayonasa video!!? kama hakuna basi waweke hiyo itawasaidia sana vinginevyo wataingiliwa tena tu! siku zijazo!! poleni kwa huo mtihani! mushukuru nyinyi mpo salama!!

    ReplyDelete
  7. Pole ziwafikie

    ReplyDelete
  8. wanachukua hesabu kamili ya hela zilizoibwa ili wasidhurumiwe na wenzio walioiba.hahahaha polisi wabongo bwana hapo wanajua kila kitu wanazuga kama vile hawajui kitu kumbe wakitoka hapo wanawapigia simu kudai mshiko wao.

    ReplyDelete
  9. Wazee wa kazi hao wamechukua chao.

    ReplyDelete
  10. mimi nanvyopajua pale royal bakery cctv camera zipo za kutosha kitamboo tu, ila mkae mkijua cctv hazifanyi majambazi wasivamie sehemu muwe na fikra indelevu nyinyi mliokuwa nchi za watu mkijivunia kubeba mabox ni ujiiinga watu nyumbani huku wanaendelea nyinyi hata kijiwanja hamna!!!!kila cku maisha ni kulipa bills tu hata shule wengi wenu mmeshindwa kumaliza.

    ReplyDelete
  11. Poleni, lakini pia invest in CCTV, Ulinzi wa kuaminika na get a proper cash register and/or safe! Unless sijaelewa vizuri "...na kuanza kuchukua fedha za mauzo zilizokuwemo kwenye droo zao za kuhifadhia fedha...." Droo??

    ReplyDelete
  12. Kuna Maswali mengi kuliko Majibu !

    1.Duka la Mikate lipo Jeshini,

    2.Pamoja na Mauzo yote hayo hawazingatii tahadhari kama kuweka kamera za Usalama na ving'amuzi,

    3.Tukio linachukua Dakika 10 eneo la Jeshini,

    4.Haijulikani pesa kamili iliyoibwa,

    5.Wahalifu hawajapatikana pamoja na kuwa tukio limetokea sehemu nyeti kama karibu na Kikosi cha Jeshi,

    ***MASWALI NI MENGI KULIKO MAJIBU***

    ReplyDelete
  13. HONGERA WEZI MLIOKWIBA HAPO,NI WAKATI WA KUGAWANA MAANA GAP KATI YA WENYE NACHO NA WASIO NACHO LINAZIDI KUWA KUBWA KWA HIYO NI BORA KULIPUNGUZA KWA STYLE HIYO

    ReplyDelete
  14. Wewe mtoa maoni kwetu sisi wabeba box, nani anataka ujinga wa huko tanzania, kila tukija kila kitu tutoe rushwa kabla ya kufanikiwa unachokita na hata ukileta biashara watu wa TRA inabidi ule nao , polisi, na majambazi waje wamalizie hio $1000 iliobaki sasa nani unataka mshauri kuja wekeza huko ushenzini mtu anatoka roho hata kwa shs 10,000/=. Hio wewe unahesabu ni nchi ? Mimi nawaombeni watanzania wote mkimbie mwende mkabebe box hata SYRIA . kwani wao wana vita ya siasa sio ya umaskini! Hata kama wakishikwa watatoka kwa dhamana within 1 week, nchi haina sheria hata kama zipo huweza kuvunjwa kwa dakika kumi na mahakimu waliogubikwa na wimbi la RUSHWA. Hao Wazungu ambao ndio watalii wanafanyiwa vitu kama hivyo mnafikiri nani atakuja tena watembeleeni huko na $ mtazitoa wapi sasa? Uongozi umeoza , Police Force, na miundo mbinu ,yote kwishnehi! Mitaa ya Area kama hiyo ya Mikocheni ni giza kitupu hakuna umeme, tena kuna jeshi na Rais mstaafu anaishi hapo hapo karibu lakini hapatokeki usiku kwa sababu ya KIZA KINENE.
    MIMI SIWEZI KUJA WEKEZA HUKO USHENZINI JAPOKUWA NI KWETU!
    Mtanzania,London

    ReplyDelete
  15. Jamani hapo mahali ni JKT, is not far, close to the main gate. Ivi tunakwenda wapi???????
    Inatisha. Halafu mtu wa piki piki ndo afanye hivyo na asishikwe??? na gari juu iwe imepaki. Hii ni mipango inayofanywa kuanzia bekary penyewe na hapo JKT. Nothing else.
    Poleni. The country is rotten!!

    ReplyDelete
  16. HAHAHA MDAU HAPO JUU MBONA UNAJIBU KWA GAZABU UKWELI TU WATU WANATOWA

    USIWE NA HASIRA TEHTEHTEH!

    HAKUNA ALIYEKATAA HATA KAMA CCTV ZIPO ILA UZEMBE KAMA JAMAA ANAVYOELEZA KUNA MAJIBU MENGI YA KUJIULIZA JE HIZO DK 10 NI CHUMVI WAMEONGEZEA AU KWELI?

    INASIKITISHA CHA MUHIMU HAWAJAUWA. NDIO KUJIFUNZIA HAPO MENGI.

    ReplyDelete
  17. Kuna kitu nyuma ya pazia, mara food poisoning, mara ujambazi. Kiwali watafute wabaya wako. Bakery sio yako tu iliyopo barabara hiyo. Ila wewe inaonekana una wateja wengi, maanake products zako ni za uhakika. washindani wako wa kibiashara watakuwa wanahusika. Sidhani kama mauzo yako yanaweza kuwafanya majambazi waje na silaha kuvamia. Huu ni ushindani wa kibiashara tu, wanataka watu wapaogope.

    ReplyDelete
  18. Hawa askari wa Kawe wamekalia kutafuta rushwa tu na kuacha majambazi yafanye yanavyotaka katika sehemu huyo na maeneo ya jirani.

    ReplyDelete
  19. Hawa askari wa Kawe wamekalia kutafuta rushwa tu na kuacha majambazi yafanye yanavyotaka katika sehemu huyo na maeneo ya jirani.

    ReplyDelete
  20. Kitu cha kushangaza ni mijitu ya nyumbani kufagilia matatizo eti "CCTV hazizuii ujambazi na muwe na mambo endelevu" whatever that means. Sasa what is proactive measure mtu ujuwe uko secured? Sisi "wabeba mabox" tunaupenda nchi yetu na tuna haki ya kukataa ulimbukeni. Kama wewe unaona hayo Maisha bora poa. Hata kama unaviwanja kumi na nyumba nzuri, mshahara mzuri matatizo ni yale yale kwa wote. Maji matatizo, umeme wa mgao, barabara folleni, dawa hadimu, shule mbovu, madaktari wanagoma, darasa la Saba na form four rate ya wanao fail ni kubwa kupita wanaopasii. Hongo kwenye haki,haki kwa polisi..... I mean

    ReplyDelete
  21. MIE NILIVYOKUWA MDOGO NILIKUWA DARAJANI HAPO TUNACHEZA SANA NA KUMBUKUMBU ZANGU KULIKUWA GARI LA SECURITY LINAEGESHA SANA KWA KUPOKEZANA WANAEGESHA KWENYE MITI, SASA SIJUI SIKU HIZI UTARATIBU UNAENDA VIPI? KAMA WANAENDELEA NAO WAWEKEWE MKAO WA MASWALI ILIKUWAJE?

    ReplyDelete
  22. huyo alosema sisi wabeba box hatuna maendeleo!! tukuulize sema kweli wewe unamaendeleo gani huko?? au ulikuja huku umechemsha! mtoto wa mama huwezi sulubu!! ushazoea kupewa! au sio na mfano wako wapo wengi kama wewe wamekuja huku hawezi kazi!! wameamua kurudi huko!! halafu mnajifanya kusagia huku!! namalizia jitambulishe jina lako na utaje maendeleo yako kama kweli unaweza!!

    ReplyDelete
  23. kubeba box mnaona deal mtabaki kuwa watumwa wa wazungu maisha yenu yote....states/london/sweden/dubai ni sehemu nnazokwenda very often kikazi washkaji zangu almost wote wamelost tena class walikuwa very smart lkn baada ya kufika huko naona maisha yao ni yaleyale daily wengi wanapiga mizinga nyumbani mifano hai ipo....wazeee msilete ubishi ambao hauna manufaa njooni nyumbani msaidie na wazazi wenu kutwa wazazi wanalalamika "najuta kupeleka mtoto nje angekuwa hapa angekuwa msaada"......kuna mengi ya kusema mimi sijisifii ila at least am somewhere settled having happy family nk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...