![]() |
Miss Tabata 2011 Faidha Ally |
Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2012, watatambulishwa Jumapili ya Pasaka Aprili 8 katika ukumbi wa Dar Wes Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema jana kuwa mashabiki wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo hao siku hiyo kabla ya kushiriki kwenye shindano la Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni mwa Mei.
Kapinga amesema utambulisho huo utasindikizwa na burudani mbalimbali ikijumuisha muziki wa dansi, taarab, bongo fleva na muziki wa asili.
Mratibu huyo alisema warembo wanaotaka kushiriki kwenye shindano la Miss Tabata wanatakiwa kuripoti katika ukumbi wa Dar West Park Tabata kuanzia saa nane mchana kwa ajili ya kujiandaa na maandalizi ya Miss Tabata.
Kapinga alisema warembo 13 wameshajitokeza kushiriki Miss Tabata. Warembo hao ni Neema Saleh Kazumari (18), Paulina Valentine (18), Khadija Nurdin (19), Phillos Lemi (20) na Mercy Mlay (21).
Wengine ni Neema Innocent (19), Ellen Sule (22), Wikllihemina Mvungi (20), Queen Issa (20), Suzane Deodatus (19), Everline Andrew (21), Josephine Peter (20) na Jamila Omary (19). Warembo hao wako chini ya wakufunzi watatu- Beatrice Joseph, Neema Chaki na Bokilo Junior.
Zaidi ya warembo 10 kutoka Tabata watafuzu kushiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu. Mrembo anayeshikilia taji la Tabata ni Faiza Ally.
Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds. Katika shindano la mwaka juzi Julliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya taifa.
Miss Tabata inaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.
Tembelea Libeneke la Miss Tabata BOFYA HAPA
Tembelea Libeneke la Miss Tabata BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...