TAARIFA ILIYOIFIKIWA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE,INAELEZA KUWA MELI YA MV. MAENDELEO INAYOFANYA SAFARI ZAKE KATI YA UNGUJA NA PEMBA IMEKWAMA ASUBUHI HII NJE KIDOGO YA BANDARI YA PEMBA (MITA KAMA 180) WAKATI IKIJIANDAA KUPAKI KATIKA BANDARI YA PEMBA ILI ABIRIA WALIOPO NDANI YA MELI HIYO WAWEZE KUSHUKA.
KWA MUJIBU WA NAHODHA WA MELI HIYO NA MDAU AMBAYE YUPO NDANI YA MELI HIYO ANAELEZA KUWA CHANZO CHA KUKWAMA KWA MELI HIYO NI KUTOKANA NA BOYA ZINAZOKUWEPO KWENYE BANDARI HIYO KWA AJILI YA KUELEKEZA MELI SEHEMU YA KUPITA ILI KWENDA KUPAKI,ZILIKUWA ZIMEHAMA KATIKA MAENEO YAKE KUTOKANA NA UPEPO MKALI ULIOZISUKUMA KUTIKA ENEO HILO NA KUPELEKWA ENEO LINGINE.
MPAKA SASA HAKUNA MADHARA YEYOTE TOKEA,KWANI TARATIBU ZA KUINASUA MELI HIYO MAHALI HAPO INAENDELEA HIVI SASA,HUKU ABIRIA WOTE WAKIWA BADO HAWAJASHUMA MELINI HUMO.
GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA KWA MAKINI TUKIO HILO NA TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.



siku Hizi GPS ya mkononi inpatikana kwa US dollar 200... Hata simu nyingi zinazo GPS.. Kama shirika halija invest kwenye kitukidogo namna hio kinachoweza kusaidia kiongozi wake haiwezi kazi
ReplyDeleteJAMANI TANZANIA,TUNAWAOMBEA ABIRIA WAFIKE SALAMA TUU,TUMECHOKA NA MAAFA YA HIZI MELI.
ReplyDeleteNi aibu sana kwa kapteni wa Meli, pengine alikuwa kalala. Njia ya kuingiza meli Bandari ya mkoani, ila land marks kibao ambazo hazihitaji kampasi au GPS, hata usiku wa manane wenye giza kubwa unaweza kuigiza meli! Shame on us
ReplyDeleteMuathirika wa MV Spice Islander!!
Sasa yule Mtaliana aliyekwamisha meli ya kitalii hapo kwao Italia alikuwa na kila kifaa cha GPS. GPS haionyeshi kina cha maji!!
ReplyDeleteTatizo kubwa ktk mambo mengi yanayopelekea Ajali na mambo kuharibika ni UBAHILI na RUSHWA!.
ReplyDeleteHebu angalia mtua anamiliki Meli ya thamani ya mamilioni ya Shilingi halafu anashindwa kuweka System makini ya kusimamia mwenendo wa Chombo(UBAHILI),,,huku akitumia fedha kuendesha Biashara kinyume na Kanuni na Taratibu(RUSHWA).