Mwigulu akionyesha kadi za TLP na ya CHADEMA alizokabidhiwa baada ya aliyekuwa Katibu Mwenezi wa TLP Kata ya Seela Sing'isi, Augustine Kyungani na aliyekuwa mratibu wa kampeni za CHADEMA Anna Silas kumkabidhi baada ya kuhamia CCM kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Sing'isi jana
 Aliyekuwa mratibu na mhamasishaji wa kampeni za CHADEMA katika uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki, katika kijiji cha Singisi, Anna Silas akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka baada ya kutangaza kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni ulofanyika jana katika kijiji hicho. Wengine kutoka kulia ni Mwigulu Nchemba na Sioi
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha, Nameloki Sokoine akimuombea kura mgombea wa CCM Sioi Sumari kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyikaKijiji cha Sing'isi jana
Msafara wa mgombea Ubunge wa CCM jimbo la Arumeru Mashariki Sioi Sumari ukitoka kwenye kambi ya CCM kwenda vijijini kwenye mikutano ya kampeni jana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Chama cha Kiimani kiogopwe kama 'UKOMA' !

    Katika mchakato mzima wa Kampeni za awali ulivyo jiri Arumeru Mashariki tumeshuhudia chama kimoja jina naweka kapuni kikiegemea upande mmoja wa Dini moja tu !

    Tanzania ni nchi yenye watu wa Imani tofauti kama hapa:

    -Wakristo,
    -Waislamu,
    -Watu wa Dini zingine za Asili,
    -Watu wasio na Dini kabisaaa.

    Sasa basi tumeshuhudia Chama hicho ambacho nakiweka kapuni kikiegemea Kanisani zaidi bila kujali Makundi ya Imani zingine kama hapo juu.

    Hivi kweli mtawala anaetokea chama chenye mwelekeo kama hiki atafaa ?

    Hawa watu na Siasa yao ya Dini moja wanataka Dunia ituelewe vipi ?

    Hivi kweli hii ni sawa ?

    ReplyDelete
  2. Wanaohama chama wakati wa kampeni hawajui wanalolifanya....ni vigeugeu......ina maana kuhama ni had wasubiri kampeni

    ReplyDelete
  3. wewe mtoa hoja wa kwanza,ua myopic,bias,na umelose focus,hiki chama unachojaribu kukitetea kwa kutukana kingine chenyewe kinafanya nini,mbona wenyew ndio wadini,wakabila,mabebari na wabinafsi?am sure unanufaika nao na ndo maana umekua kipofu,kama una uzalendo wa kutosha na taifa hili sidhani kam unaweza kuwasuport magamba ni kama kutaka kuitakatisha kaniki wakati rangi yake inajulikana
    bye bye magamba ua days are numbered na sisi vijana hasa tusiona ajira na hamtujali ingawa tumesoma tutawatoa

    ReplyDelete
  4. CCM ndicho chama pekee Tanzania ambacho kina Watanzania wa rangi, dini na makabila yote. Falsafa ya CCM ni ile ile ya ANC (SA), Frelimo (Msumbiji), MPLA (Angola) na Swapo (Namibia). Hatuna udini wala ukabila wala ubaguzi wa rangi na amani na maendeleo ni chanda na pete. Kwa kushindwa kukemea kampeni za wazi zilizokuwa zikifanywa makanisani 2010 na kusababisha makanisa kubadilisha siku ya ibada kuu kutoka jumapili kwenda jumamosi, slaa na uongozi wa chadema walionyesha wazi udini wao. Lakini chadema lazima waelewe kuwa kama wana azma ya kuwatenga watu wa dini moja na kuleta "apartheid" ya kidini katika kisiwa chetu hichi cha utulivu na amani basi jahazi letu litazama, kwani Watanzania hatutakubali kamwe kuruhusu udini uitawale nchi yetu. Na ndiyo maana NGO yetu (jina kapuni) tumepeleka majina ya slaa na godbless lema ICC (mahakama ya jinai ya kimataifa), the Hague, Uholanzi ili wawe katika 'watch list' ya wachochezi, huku tuliwa na ushahidi ulionukuliwa kutoka katika magazeti mbalimbali hapa nchini yakiwemo magazeti yanayofadhiliwa na Mheshimiwa F Mbowe (Mbowe SI mchochezi). Slaa mnamo 2010 alitamka mara nne kuwa "lazima tumwage damu" na mwaka jana, 2011, mara mbili kuwa "tutahakikisha nchi hii haitawaliki", wakati lema mwaka jana na mwaka huu ametamka kuwa "amani haina faida inapumbaza watu". Kwa nyinyi wote mlioko chadema AMABAO MNA NDOTO YA KULETA VURUGU mnaosoma maoni haya nawaambia wazi TANZANIA ITAENDELEA KUWA NA AMANI NA HATUTAWARUHUSU KAMWE KUTUMIA MAITI YA WATANZANIA KUWA NGAZI YENU YA KUTWAA MADARAKA. Jumapili iko karibu: slaa, tundu lissu na lema mtaangukia tena pua. To be forewarned is to be forearmed. ccm4life.

    ReplyDelete
  5. kama chadema ni chama cha wananchi wote na hakitakuwa na udini basi tutakipigia kura na ipo siku tutawapa nchi

    lakini kama watajikita zaidi kwenye udini basi wakae wakijuwa kamwe hawatofika popote kwani waislam tulio wengi na wazee wa mjini tuliomkaribisha nyerere hatuwezi kuwapa chadema nafasi ya kuongoza nchi.

    ReplyDelete
  6. CCM ndiyo mume wao

    ReplyDelete
  7. Kila unapotokea uchaguz maneno ndo hayo hayo ya udini. Ingawa mm ni mwana ccm till to die, ila hoja hii ni dhaifu na ukwel wake ni mdogo. Ni siasa tu

    ReplyDelete
  8. ha ha haaaaaa weye mchangiaji wa Thu Mar 29, 08:18:00 AM 2012,USHAJITUNGIA kiji propaganda chako,hio trick ya UDINI hamuiachi tu nyie GAMBA????safari hii ni KILIO tu kwenu pamoja na kujitapa kwenu.

    ReplyDelete
  9. kama huna cha kuandika sio lazima uandike utumbo humu kwenye mtandao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...