Ndugu Michuzi Salaam
Napenda kutoa mchango wa mawazo kwa watanzania wenzangu kuhusu kusaidia uchumi wetu kufuatia ugumu wa maisha, hasa siku za karibuni, unaosababishwa na kuyumba kwa uchumi katika nchi zilizoendelea, ambazo ndizo mama mlishi wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Kuwepo kwa ugumu wa maisha kisiwe ni kikwazo pekee cha kushindwa kujikwamua kimaisha. Matatizo yetu mengi ya kiuchumi, na hata ya kijamii, hayatapata ufumbuzi toka kwenye vitabu tunavyosoma vyuoni au mashuleni kwani hata silabasi yetu ya elimu haiyatambui. Tukiyafanyia kazi yaliyotajwa hapo chini, nina imani maisha ya mtanzania wa kawaida yatainuka na hivyo kuongeza maendeleo ya haki nchini.
1. Watanzania tulipe kodi- Sehemu kubwa ya uchumi wetu imeshikiliwa na 'black market' pamoja na umachinga. Sehemu hizi hazijatengenezewa mazingira mazuri ya kuwezesha kujituma kulipa kodi ya mapato.
2. Watanzania tuwe wabunifu- Tuangalie nyuma nasi tuanze kusafirisha ubunifu wetu nje ya nchi sawa na wenzetu wachina wanavyofanya hivi sasa. Inakuwaje tunajisifia kunywa 'Heineken' ambayo inaua soko la rubisi, kimpumu, machicha n.k
3. Watanzania tusikubali kutoa rushwa- Tunapotoa rushwa hatusaidiwi bali tunaibiwa haki yetu ya kuhudumiwa, rushwa sio Tip!
4. Tusichukue mikopo- Kuna ukweli kwamba uchina, India na Vietnam zinaendelea kwa kasi tokana na wananchi wake kujijengea rasilimali wenyewe. Mikopo inarudisha nyuma maendeleo; inajenga tabia 'Tegemezi'- sababu kubwa iliyorudisha maendeleo ya bara la Afrika.
Salaam
Jogoo Makunja.
Mdau, 1) mojawapo ya sababu zinazofanya watanzania wengi waone shida kuilewa dhana ya kodi ni kwamba hawaelewi fedha za kodi ninafanya nini/zinapelekwa wapi, kuna wananchi wengi wameona wazi kabisa matumizi mabaya, yasio na uwiano ya serikali yanayotokana na fedha za kodi! Hivyo kuna hisia kali kwamba fedha yangu nikilipa kodi - inakwenda kuchezewa na wachache!!
ReplyDelete2) Wananchi wasipotoa rushwa ni wao ndio watakaopata shida, maana wengine wengi wanatoa na wataendelea kutoa ili wapate huduma, TATIZO LA RUSHWA LITAPUNGUA KWA KIWANGO KIKUBWA KAMA SIO KUISHA KABISA NI PALE VIONGOZI WAKUU WAKIONYESHA DHAMIRA YA KWELI KWA MANENO NA VITENDO KWAMBA KWELI WANACHUKUKIA RUSHWA.TATIZO LA RUSHWA LIPO DUNIA NZIMA - TOFAUTI YA SISI NA WENZETU KWA HILI NI KWAMBA TUHUMA ZINAPOJITOKEZA SHERIA HUFUATA MKONDO WAKE, WAKATI KWA SISI HAPA TUHUMA ZINAPOJITOKEZA SHERIA HAIFUATI MKONDO, BALI MADARAKA NA UWEZO WA FEDHA WA MHUSIKA NDIO HUFUATA MKONDO WAKE. WATU WA CHINI WANA NAFASI NDOGO SANA KUONDOA TATIZO HILI. BILA HIVYO RUSHWA ITAENDELEA KUWEPO MILELE NA MILELE.
Mdau Jogoo Makunja Hoja yako ni makini sana.
ReplyDeleteMimi nakuunga mkono ktk Mapendekezo yako kwa kipengele cha 4 (Mikopo)
Ni kweli kabisa kwa sababu kilichopelekea nchi za Magharibi kupata Matatizo ya Kifedha na Kiuchumi ni SERIKALI ZAO KUWA NA UTEGEMEZI WA MIKOPO ULIO KITHIRI ambao umezalishwa na UHCUKUAJI WA DHAMANA ZA MIKOPO ''TREASURY BILLS'' kutoka KTK BENKI ZA KIBIASHARA AMBAZO HUTOZA RIBA ILIYOPELEKEA KUKUZA MADENI MAKUBWA NA HATIMAYE SERIKALI KUSHINDWA KUYALIPA.
HIVYO ILI KUJINUSURU:
1.Ndio kama ulivyotoa ushauri Kujijengea Utamaduni wa kujitegemea kwa Uwezeshaji wa karibu kila kitu kuanzia Mitaji na Rasilimali. (MIKOPO YA RIBA INAONGEZA KASI YA UMASIKINI INGEFAA KUTUMIA NJIA YA MBADALA YA ''NON-INTEREST SEED MONEY'' MIKOPO YA 'GRANTS' AU YA 'ISLAMIC FINANCE COMPLIANCE' AMBAYO HATA IMF NA WORLD BANK IMETHIBITISHA NI YA UKOMBOZI DHIDI YA UMASIKINI.
2.Kuwa wabunifu mfano kuacha kutegemea sana Kodi ya Mafuta, Umeme, Sigara na Pombe kuwa vianzo vya Ukusanyaji wa Mapato ili Serikali iweze kuwa na Fedha za Kuendeshea Utawala wa nchi
-----------------------------------
Tumeshuhudia mara zote vitu hivi vimekuwa vikiongeza mfumuko wa bei za bidhaa na kupandisha gharama za maisha kuwa magumu kama Hoja inavyo sema,,,Pia vitu hivi vinaongeza Ukata ''Inflation'' kwa kasi zaidi na kufanya Uchumi kudorora.
-----------------------------------
3.Tujaribu kuongeza kasi ya Utegemezi wa Biashara ya nje Import and Export kwa vile inaleta ''imported Inflation'' yaani ''Ukata wa Kuingiza Nchini toka Nje'' ambao unasababisha kudorora kwa Uchumi,,,Badala yake Tuongeze Uzalishaji wa ndani na Tukuze Soko la ndani la Bidhaa zetu kwa Kujenga ''Home made Customer base'',,,KWA HIVI MZUNGUKO WETU WA FEDHA UTAKUWA HAURUHUSU KUTUGHARIMU DOLA NYINGI NA FEDHA ZA NJE KUAGIZA BIDHAA NJE,,,PIA HAITATULAZIMU KUJIKAKAMUA SANA KTK KUKUSANYA FEDHA ZA NJE ILI TUMUDU KUUWEKA SAWA UCHUMI WETU WA UJUMLA.
4.TUONGEZE UFANISI KTK USIMAMIZI WA UKUSANYAJI WA KODI PIA USIMAMIZI KTK MATUMIZI YA FEDHA ZA KODI KWA MAENDELEO YA NCHI.
5.ILI TUSONGE MBELE TUWE NA UTAMADUNI WA KUITANA, KUHOJIANA NA KUWAJIBISHANA (HASWA KTK MASUALA YA MAPATO,FEDHA,UCHUMI, UTEKELEZAJI, UENDESHAJI (Management Excellence) NA UWAJIBIKAJI) PINDI MAMBO YANAPOFANYWA BILA UWAJIBIKAJI MAKINI.
Jogoo Makunja umetoa changamoto na maoni mazuri. Nakubaliana na wewe ktk mambo 3 kati ya 4 uliyotaja. Nisilokubaliana nalo ni hilo la kwanza, tukilipa kodi wakati hakuna mfumo mzuri wa matumizi yake hapatakuwa na tija. Kodi zinaliwa na wajanja na hiyo inakatisha tamaa.
ReplyDeleteAise asante sana mtoa mada na wachangiaji wote 1-3 kutoka juu.Mmeshusha nondo si mchezo.Mimi si mtaalam sana wa haya masuala ila nina swali dogo..Waziri wa Fedha,maafisa wa fedha na uchumi,BOT n.k hawaelewi hayo mliyoandika?..Kwanini wasi-implement tuone itakuwaje.Labda tunaweza kutoka..Manake tulipo sipo jamani.
ReplyDeleteDavid V
Wewe David V umesema wewe ni mtaalamu sana wa mambo haya. Sasa vipi hujaweka input zako hapo ili tuone ulivyobobea? Umeishia kuuliza swali wala huweka mawazo yako mwenyewe hapo. Fadhali tupe dataz ili tuweze kuelewa zaidi. Asante.
ReplyDeleteMsemaKweli
Mdau David V,
ReplyDeleteHaya masuala Wizara ya Fedha na BOT yawezekana wanayajua lakini wanaathiriwa na Wana Siasa au inawezekana Waliopo ktk nafasi hizo Vyeti vyao ni vya kununua au wame foji kuingia Maofisini.
Mfano athari ya Ki siasa ni kuendelea kutumia Mafuta na kutegemea zaidi Kodi ya Mafuta kama kianzo cha mapato wakati nishati mbadala ipo ni Gesi asilia LNG inayozalishwa Songosongo tena yenaye ubora wa kiwango cha juu kabisa!
David V.
ReplyDeleteWizara ya Fedha na BOT wanayajua haya vizuri tu ila,
Mdau mchawi wetu mkubwa ni kutumia zaidi Siasa kuliko Sayansi!