Chanzo cha Moto huo kimesababishwa na hitilafu za umeme uuliotokea majira ya saa nne na nusu za asubuhi .
Mmoja wa wafanyakazi wa usafishaji wa Jengo hilo nd. Vuai Haji aliwaeleza waandishi wa habari kwamba hitilafui hiyo imetokea katika Chumba cha iliyokuwa afisi ya bodi ya mapato Zanzibar ZRB cha mtandao wa Kompyuta.

Msaidizi Kamishna wa Kikosi cha zima moto na uokozi Kamanda Simai Ame Simai amesema watedaji wake wamelazimika kuvunja vioo vya dirisha la Ofisi hiyo kwa lengo la kuzima moto ili kunusuru kuzagaa kwa maafa zaidi.
Kamanda Simai ametoa wito kwa jamii kutoa Taarifa za haraka pale yanapotokezea matukio kama hayo ili waweze kupata huduma za haraka na uhakika.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifika katika eneo hilo kujionea hali halisi ya tukio hilo .

Balozi Seif alisisitiza pia kufuata utaratibu wa kuzimwa kwa mashine zote za umeme wakati wanapomaliza shughuli zao za kikazi.
Hadi sasa bado haijajuilikana hasara iliyopatikana kutokana na moto huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...