Wanachama, Wapeni pamona na wananchi waliofika uwanja wa ndege wakimsalimia Profesa Ibrahim Lipumba alipowasili jana.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julus Nyerere kuhusiana na ziara yake
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiwasalimu wanachama pamoja na wapenza wa CUF waliofika Uwanja wa Ndege kumlaki. Kulia ni Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad na kushoto na Makamu Mwenyekiti wa CUF Machano Khamis

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na mwandishi wa habari wa kituo cha Radio na Televisheni cha Africa 24 bibi Camille Thomas aliyefika nyumbani kwake Maisara kwa ajili ya kuzungumza nae.Picha na Salmin Said -Ofisi Ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. what a sellout...

    ReplyDelete
  2. Ankali/Wadau kuuliza si ujinga na aulizae ataka kujua. Hivi Profesa Ibrahim Lipunba kupata mapokezi kama haya ina maanisha nini? au inaashiria kwamba ni dalili ya kitu gani? mie sielewi na kwa kweli nimeshangaa sana au labda mie nimepitwa na wakati???

    ReplyDelete
  3. prof Lipumbaamepeperusha bendera yatu vyema kti ya wanazuoni 500 bora DUNIANI..HUONI KAMA HILI NI JAMBO LA KUJILINGIA KWETU KULIKO KWENDA KUWAPOKEA WATU TOFAUTI NA HILI.KAMA MDAU AMBAYE ANAPENDA ELIMU BASI PROF LIPUMBA NI MFANO BORA SANAA KTK TZ YETU.

    ReplyDelete
  4. Ukweli wa Mambo utabaki palepale kuwa Prof.Ibrahim Haruna Lipumba ni Dakitari wa kweli ni kwa vile tuna Siasa zisizokuwa na tija tungemtumia yeye na Safu ya Wasomi wengine kuunda Kikosi kazi nchi isingefika hapa ilipo.

    MFANO WA WATU KIKOSI KAZI TULIONAO:
    1.Prof.Ibrahim H. Lipumba
    (ametengwa kutokana na Kisiasa)
    2.Dr.Harrison Mwakyembe
    (Amehujumiwa Kiafya)
    3.Dr.Ramadhan K. Dau
    (Hapewi ushirikiano)
    4.John P. Magufuli
    (Anakwamishwa na Wapinga maendeleo)
    5.Prof. Anna Tibaijuka
    (Anababaishwa na Wasanii Serikalini)
    6.Prof.Mark Mwandosya
    (Amehujumiwa Kiafya)
    7.Prof.Ali T. Mtanda
    (Ametengwa Kisiasa)
    8.Prof.Mbele
    (Anahujumiwa ,ona juzi ameibiwa hadi Laptop yake mpya ya apple)
    9.Prof. Philemon Sarungi
    (Ameharibiwa na kuwa Mwanasiasa badala ya kuwa Mwanasayansi)
    10.Prof.Simon Mbilinyi
    (Ametengwa Kisiasa)
    11.NA WENGINE WENGI WAPO NJE YA NCHI
    (Wametengwa kwa kigezo wapo nje!)

    ReplyDelete
  5. Kukwamishwa kwa Prof. huyu kushiriki ktk ujenzi wa Taifa kunakuja kutokea kwa Wanasiasa wasio na elimu na mwamko ambao wengi wao ni watu wa Maslahi binafsi tu badala ya Uzalendo!

    WENGI WA WANASIASA HAO WANA ELIMU ZA KUGHUSHI TU NA MTAZAMO WAO NI FINYU!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...