Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa jana jioni na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.


Miongoni mwa shughuli ambazo Mheshimiwa Rais atafanya ni pamoja na kuzindua kampeni ya kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo ataizindua kwa kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro Speak Out, Climb Up”.

Shughuli hiyo itakayofanyika kesho Jumatatu, Machi 5, 2012 asubuhi, imepangwa kwenye Lango la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)
Mbali na kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua Mkutano wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi mjini Moshi.

Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea Mkoa huo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

kwa mapicha zaidi




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Mkuu wa mkoa..unahitaji kufanya mazoezi kwa usalama wako mwenyewe

    ReplyDelete
  2. Ivi Kilimanjaro ni karibu na Arumeru Arusha ee?

    ReplyDelete
  3. Karibu mkuu kwenye vitochi vya Mbege

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...