BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica imezidi kuibomoa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ baada ya kumyakua mnenguaji wake mahiri,Lilian Tungaraza maarufu kama ‘Intanet’.

Meneja wa Mashujaa Band Maximilian Luhanga alisema kwamba wameamua kuwachukua wanamuziki hao ili kuimarisha bendi yao katika idara hizo na tayari ameshasaini mkataba wa kuitumikia bendi hiyo kwa miaka miwili ambao onyesho la utambulisho linatarajiwa kufanyika jumatano ijayo katika ukumbi wa Nyumbani Lounge.

Hii ni mara ya pili kwa Bendi ya Mashujaa kuchukuwa Mwanamuziki wa Bendi ya Twanga Pepeta ambapo mapema mwaka huu ilimyakua mmoja ya waimbaji mahiri, afahamikae kwa jina la Charlz Gabriel ‘Chaz Baba’.

Lilian Internet amesema kutokana na umahiri wake atahakikisha anaitumikia vyema Bendi yake hiyo Mpya na amewataka Mashabiki wake woote kuungana nae katika  sehemu yake hiyo mpya ya kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. No comment

    David V

    ReplyDelete
  2. kama dau kumbwa mama go for it! kila kitu pesa bwana.

    ReplyDelete
  3. Hongera,punguza uzito basi.

    ReplyDelete
  4. Huyu Lilian sasa aache mambo ya kunengua ajikite zaidi katika kuimba. Huyu akiwa kwenye 'mike' atakuwa kama yule chiriku wa kike ya DRC Deesse Mukangi.

    ReplyDelete
  5. Dada ,punguza kitambi

    ReplyDelete
  6. wewe kapunguze hayo manyama kwanza utapendeza mavazi uliovalia ni ya watu wembamba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...