TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Longinus Kyaruzi Rutasitara kuwa Naibu Katibu Mtendaji (MARCO) Tume ya Mipango.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Peniel Lyimo leo, Ijumaa, Februari 2, 2012, Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa uteuzi huo ulianza tokea Februari 20, mwaka huu wa 2012.

Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Rutasitara alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwisho.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.
Dar es Salaam.
02 Machi, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...