Polisi wenye silaha kutoka wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma wakiangalia maguduria yanayodhaniwa kuwa na mfuta aina ya diesel yaliyoibiwa katika moja ya kambi ya kampuni za ujenzi wa barabara ya kutoka Songea kwenda Mbinga kwa kiwango cha rami,katika kijiji cha Mkako wilayani humo.kumekuwa na vitendo vya wizi katika kampuni za ujenzi mkoani Ruvuma hali inayohatarisha na kuchelewesha ujenzi wa barabara hizo.
ASKARI POLISI KUSHOTO AKIWA NA MTUHUMIWA WA WIZI WA BETRI YA GARI AMBAYE HAKUTAKA KUTAJA JINA LAKE (KULIA) ALIYEKAMATWA KATIKA KIJIJI CHA MKAKO MBINGA, KUFUATIA MSAKO MKALI WA JESHI LA POLISI KUWASAKA WATU WANAOJIHUSISHA NA VITENDO MBALIMBALI VYA UHARIFU WILAYANI MBINGA.
WACHUUZI WA NDIZI KATIKA MITAA MBALIMBALI MJINI SONGEA WAKITAFUTA WATEJA KANDO KANDO YA BARABARA YA SOKINE MJINI HUMO,KAMA WALIVYOKUTWA NA MPIGA PICHA WA GLOBU YA JAMII.
AKINA MAMA WANAOJIHUSISHA NA KUUZA MATUNDA NA MBOGA MBOGA WAKIWA WAMEPANGA BIASHARA ZAO CHINI JIRANI NA HOTEL YA SAFINA MJINI SONGEA KUFUATIA KUFUKUZWA KATIKA ENEO WALILOKUWA WAKIFANYIA BIASHARA HIZO NA MANISPAA YA SONGEA.PICHA NA MUHIDIN AMRI WA GLOBU YA JAMII,RUVUMA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...