Na Mary Ayo,Arumeru
MGOMBEA ubunge kupitia CCM,Sioi Sumari amehaidi kutatua kero ya uhaba wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari ya Sakila iliyopo wilayani humo ikiwa ni pamoja na kuboresha majengo ya shule hiyo.
Sumari,alitoa kauli hiyo jana wakati akiomba kura za wakazi wa kijiji cha Sakila wilayani humo ambapo alikuwa ameambatana na mkewe,Pamela Lowassa.
Aliwaambia wakazi wa kata hiyo ya kwamba anatambua tatizo la uhaba wa vifaa vya maabara ndani ya shule hiyo na amejiapnga kulitatua pindi watakapompa ridhaa ya kuwa mwakilishi wao katika bunge la jamhuri ya muungano ya Tanzania.
Aliwaambia wakazi hao ya kwamba atajitahidi kuboresha majengo ya shule hiyo ili yaweze kuendana na hadhi ya shule za sekondari kwa lengo la kuboresha kiwango cha elimu ndani ya kijiji hicho.
“Kwa upande wa elimu natambua kuna tatizo la uhaba wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari ya Sakila nimejipanga kutatua tatizo hilo kikamilifu’alisema Sumari.
Hata hivyo,aliwaambia wakazi hao ya kwamba mbali na kutatua kero hiyo ya elimu pia amejipanga kutatua tatizo la kero ya maji ndani ya kijiji hicho kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama.
Alisema kwamba anatambua tatizo la uhaba wa maji ndani ya kijiji hicho kwa kuwa limeanzia kata ya Songoro ndani ya kijiji cha Kilinga hivyo amejipanga kutatua tatizo hilo kwa kushirikiana na serikali bega kwa bega.
Aliwaambia wakazi hao ya kwamba wamchague kwa kuwa ana nia ya dhati ya kuwatumikia kwa kuwa analifahamu jografia na jimbo la Arumeru Mashariki.
Hatahivyo,aliwaambia wakazi hao ya kwamba yuko tayari kushirikiana bega kwa began a wakzi hao kuchimba visima mbalimbali ndani ya kijiji hicho ili yaweze kusaidia wakazi wa kijiji hicho pamoja na mifugo.
Wakati huo huo alihaidi kuboresha uwanja wa mpira wa Sakila kwa kuweka magoli ya kisasa pamoja na kuuboresha kwa kiwango cha juu ili uendane na hadhi ya kimataifa.
Aliwaambia vijana wanaoutumia uwanja huo kuchezea ya kwamba yuko tayari kushirikiana nao kwa kuwapatia vifa vya michezo kama jezi na mipira ikiwa ni pamoja na kuhakikisha timu ya Sakila inashiriki ligi mbalimbali nchini.
Kaka Michuzi mbona picha za Chadema hutoi?usiwe bias bwana
ReplyDelete