Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani 'almaarufu Profesa Majimarefu' akionesha sehemu ya kioo katika gari lake aina la lexus lenye namba za usajili T 265 BLS ambalo limevunjwa vioo na watu wanaohisiwa kuwa majambazi.
Na Ripota wetu, Tanga
MBUNGE wa jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani ‘almaarufu Profesa Majimarefu’, usiku wa kuamkia leo alivamiwa na watu wanaohisiwa kuwa majambazi  katika eneo la Mombo, walipoweka mawe barabarani kwa lengo la kuteka magari.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini, Profesa Majimarefu alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 7:00 usiku wa kuamkia jana katika eneo hilo alipopita wakati akitokea Jijini Nairobi kuelekea Tanga kwenye mkutano wa wadau wa mkonge  uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa.
Akielezea tukio hilo, mbunge huyo alisema kuwa wakati alipofika eneo hilo walikuta mawe yamepangwa barabarani na dereva wake alipoona hali hiyo aliingia kwenye mtaro kuyakwepa mawe hayo lakini wakiwa pembeni ya barabara, walitupiwa mawe ambayo yaliweza kuvunja kioo cha gari upande aliokaa mbunge huyo.
“Tulipofika eneo hilo Hoteli ya Liverpool naiona ile pale, tukakuta mawe barabarani dereva wangu Omari kuyaona akaingia pembeni kuyakwepa kule pembeni tulitaka kupinduka, lakini majambazi wale waliturushia mawe yaliyovunja kioo,” alisema mbunge huyo huku akionesha gari hilo kwa waandishi wa habari.
Akielezea zaidi alisema alitoka Jijini Nairobi majira ya saa 12:00 jioni Jumapili kuelekea Jijini Tanga kwenye mkutano huo lakini alipofika katika eneo la Manga –Kibaoni akiwa anaendesha yeye gari hilo lenye namba T 265 BLS aliamua kuweka gari pembeni ili wapumzike kisha waendelee na safari.
“Tulilala pale kama dakika 20 hivi dereva wangu aliamka akasema mzee hatuwezi kulala hapa bora tusogee mbele maana tumeshafika Korogwe bora tukalale nyumbani kisha kesho (jana) twende Tanga mkutanoni, nilimkubalia kumbe tunakwenda ‘kwenye mtaji wa masikini’,” alisema mbunge huyo.
Mbunge huyo alisema tukio atahakikisha anashirikiana na wananchi wa eneo la Mombo kuhakikisha vijana wanaojihusisha na uhalifu na kuchafua sifa nzuri ya wakazi wema wa eneo hilo, wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa polisi mkoani Tanga, Constantine Masawe alikiri kutokea kwa tukio hilo ambaloaalisema kuwa jeshi hilo tayari limeanza kazi ya kuwasaka watu hao waliofanya uhalifu ili waweze kuwakamata kutokana na vitendo hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. du jamaa hawajitakii mema? long water (maji marefu) wanamchezea kweli? wataota sehemu za siri usoni, ohoooooo!!!1?

    ReplyDelete
  2. Sasa baada ya kuingia mtaroni?.....habari haijakamilika.Hao watakuwa vijana wa hapo Mazinde.Pole sana mheshiliwa na dereva wako..mngeweza kupinduka na dereva wako.Halafu Prof.hapo unapopasema mbona lami imekuwa hivyo tena?,imejaa "mashimo viwembe" yanachana magurudumu ya magari..Fanyeni utaratibu lipatikane fungu la kurekebisha hicho kipande kiongozi


    David V

    ReplyDelete
  3. Mhe. Mbunge Stephen Ngonyani na Dereva wako Ndg. Omar poleni sana kwa balaa hili, sasa ni wakati muafaka kwako Mhe. kumiliki silaha ya moto!

    ReplyDelete
  4. Mhe. Mbunge usifikiri yaliyojiri kwenye Uchaguzi 2010 ukaleta Mageuzi Korogwe Vijijini itabaki kuwa Shwari tu kama vile zamani,,,hapana!

    Lazima utakuwa na Wabaya wako tu, jihadhari nao.

    ReplyDelete
  5. Ndugu yetu Bwana Mkubwa Mhe. Ngonyani usifikiri ktk Dunia hii watu wote watafurahi ukiendesha LEXUS mbichiiii,,,huku ukiwa na Suti murua na saa ya maana mkononi!

    Dunia imegeuka sasa na Wabaya ni wengi licha ya Uungwana, Undugu na Ujamaa ulionao kwa watu inabidi ujifunze kutumia Bastola!

    ReplyDelete
  6. Kiongozi pole sana na matatizo,

    Inakubidi uwe na moyo mgumu na kufanya maamuzi magumu inapobidi ili kujinusuru dhidi ya watu wasio wema kwako!

    ReplyDelete
  7. Pole Mheshimiwa!

    Hayo ndio mafao ya Mafanikio, Dunia yetu ukitoka Kimaisha panakuwa na wasiotaka iwe.

    ReplyDelete
  8. Pole Mhe. Mbunge !

    Wala usiandae Mtungi wa Maji (TV asilia), maharage makavu na majivu kupiga ramli kumtafuta mchawi wako!

    Hao sio wengine ni walewale Wapiga debe wa Mpinzani wako kipindi kile cha Uchaguzi Oktoba 2010!

    Bwana Mkubwa, Ubaya hauna kwao wala hauna kabila, ahalani wasaalani!

    ReplyDelete
  9. Muheshimiwa Mbunge pole na Mkasa!

    Wala usihangaike kuushusha Mkoba wako wa Uprofesa kutoka Darini ili kumtafuta mbaya wako.

    Kumbuka wengi wanaokuzunguka wanaweza kuwa sio wema kwa vile umefungua ukurasa mpya wa maisha na sasa unaitwa Mhe. Mbunge!

    ReplyDelete
  10. Pole Mhe. Mbunge!

    Ahhh, Mkubwa ndugu yetu suala la wewe kuendesha hiyo Lexus peke yake linaweza kukujengea maadui kibao tu!

    ReplyDelete
  11. Pole Daktari Mhe. mbunge!

    Kama Wadau wanavyotoa hapo juu,

    Haihitaji kuweka maji ktk Sinia wala Ungo ili kusaka saka,,,wengi wa Wabaya wako utawaona kwa dalili za haraka haraka kwa vile Mwisho wa Ubaya ni Aibu!

    ReplyDelete
  12. Mhe. Mbunge pole kwa kizaa zaa kilichokupata.

    Aha suala lipo wazi kabisa huo ni wivu na ubaya wa waiwazi Mchana kweupeee,

    Wala isiku gharimu ukakesha Mkubwa Dakitari ukipiga Makopo ya Manyanga wala kuchinja paka na kunywa damu ya paka kwa manyanyau kumsaka mbaya wako.

    Hao ni hao hao mnaokumbana ktk Majukwaa ya Siasa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...