Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini China Mhe.Philip Marmo ikulu jijini Dar es salaam wakati Rais alipokuwa akiagana na mabalozi wanne wapya wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje wakati walipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Mabalozi hao waliapishwa hivi karibuni. Mabalozi wapya walioagana na Rais Kikwete ni pamoja na Mhe.Philip Marmo anayekwenda China, Mhe.Grace Mujuma anayekwenda Zambia, Mhe.Mohamed Haji Hamza anayekwenda Misri na Mhe.Dkt.Batilda Burian anayekwenda Kenya.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya Mhe.Dkt.Batilda Burian ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na balozi mpya wa Tanzania nchini Misri Mhe.Mohamed Haji Hamza ikulu jijini Dar es Salaam leo subuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi mpya wa Tanzania nchini Zambia Mhe.Grace Mujuma ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha zote na Freddy Maro)


Inakuwa kama ni ''Mujibu wa Sheria'' kama ilivyokuwa wakati wa kupelekwa JKT miaka ileee.
ReplyDeleteSasa jamani hawa Mabalozi kazi walizopewa wamelazimishwa?, mbona hawaondoki kila kukicha wanaaga tu!
Inakuwa kama ni ''Mujibu wa Sheria'' kama ilivyokuwa wakati wa kupelekwa JKT miaka ileee.
ReplyDeleteSasa jamani hawa kazi walizopewa wamelazimishwa?, mbona hawaondoki kila kukicha wanaaga tu!
PICHA MBILI ZA CHINI:
ReplyDeleteUnajua Saikolojia ni Sayansi ya ajabu sana, maeneo yake makubwa ni
1.Utambuzi
2.Maumbile
3.Mwenendo
TWENDE NAMBA 1 (Utambuzi)unashirikisha uso wa mtu.
Kulingana na nyuso za picha mbili za Chini Mabalozi Wateule wanaonyesha kama hawajiamini au hawakuridhika na Walichopangiwa.