Nahodha wa Timu ya Simba,Juma Kaseja akiongoza wachezaji wenzake pamoja na kocha wao kushangilia ushindi wa timu yao dhidi ya Kiyovu ya nchini Rwanda uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Simba imeshinda 2-1 na kujihakikishia kuendelea na mashindano ya Kombe la Shirikisho.
  Dakika ya 19 na 32 za mchezo,Mshambuliaji wa timu ya Simba,Felix Sunzu anaipachikia mabao 2 ya kuongoza timu yake baada ya kumalizia pasi nzuri za Mchezaji Emmanuel Okwi (Balloteli).Mpira unaendelea  ambapo timu ya Kiyovu inajipoli la 1 mnamo dk ya 76 kipindi cha pili na mchezo unaendelea.
Felix Sunzu akishangilia magoli yake.
 Msambuliaji wa Simba,Emmanuel Okwi achonga pasi safi kabisa iliyozaa tunda la bao la kwanza.
Washabiki wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao.
 Kikosi cha Simba.
Kikosi cha Kiyovu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ngoja Nyati aliyejeruhiwa atoke huko Cairo.Mtaipata na huo ushindi wenu wa kombe la kuku.

    David V

    ReplyDelete
  2. tatizo wamevaa jezi zinazotaka kufanana na yanga, wangeuliza kabla.

    ReplyDelete
  3. haahaha acha wivu ila sasa mtakuja hapa algeria kucheza na etente de setif.jiandaeni hawajama mapafu ya mbwa wanacheza 90 bila kuchoka.tunawasubiri kuwashangilia nipo HAPA setif ALgeria.

    ReplyDelete
  4. Yanga ndo tabia yenu,kila Simba ikishinda mnasema subirini watui fulani,nao tukiwashinda mnasema subirini watu fulani.

    Ndo maana hata ninyi mkicheza msitutake uzalendo wa kuwashangilieni.Tutashangilia timu pinzani tu.

    Simba yasonga mbele mwaona donge.Zamalek imewashinda sasa mwaikandia Simba.Huko Algeria sisi hatuna wasiwasi kwani tulishawashinda si mara ya kwanza kucheza nao.

    ReplyDelete
  5. Naipongeza SSC kwa ushindi ila, timu ilichoka sana hasa kiungo. Nina mashaka makubwa na uwezo wa mwalimu kutengeneza stamina ya wachezaji. Sidhani kama Simba itaweza kushinda ikikutana na timu yenye nguvu.

    ReplyDelete
  6. Kiyovu wameponzwa na Jezi (rangi ya kijani),,,wangelivaa hata Blue angalau!

    ReplyDelete
  7. SIMBA wanahitaji kuimarisha NGOME yao na pia wachezaji wengi hawana STAMINA.....Washambuliaji Okwi na Sunzu ni MOTO...!!!HONGERA SIMBA...!!

    ReplyDelete
  8. Simba kazeni buti wala msiogope timu za waarabu. Mpira uko kokote. Ila waarabu kwa vile Makao Makuu ya CAF yako Misri huwa wanajipendelea sana, kila mechi ni lazima wajipangie timu zao zianze ugenini n a kumalizia kwao. TFF hamlioni hili lalamikeni wafanye mabadiliko.

    ReplyDelete
  9. Mdau wa soka BongoMarch 05, 2012

    Bongo Mpira bado maneno mengi kila mtu anajua kucheza na kila mtu ni kocha. Timfurani ikibahatisha kushinda wanachongaaa mpaka kero hivi sasa hawa jamaa wanajifananisha na Baca acheni upuuzi ninyi hamtafika popote mtakalia uchawi na maneno matupu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...