Nahodha wa Timu ya Simba,Juma Kaseja akiongoza wachezaji wenzake pamoja na kocha wao kushangilia ushindi wa timu yao dhidi ya Kiyovu ya nchini Rwanda uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Simba imeshinda 2-1 na kujihakikishia kuendelea na mashindano ya Kombe la Shirikisho.
Dakika ya 19 na 32 za mchezo,Mshambuliaji wa timu ya Simba,Felix Sunzu anaipachikia mabao 2 ya kuongoza timu yake baada ya kumalizia pasi nzuri za Mchezaji Emmanuel Okwi (Balloteli).Mpira unaendelea ambapo timu ya Kiyovu inajipoli la 1 mnamo dk ya 76 kipindi cha pili na mchezo unaendelea.
Felix Sunzu akishangilia magoli yake.
Msambuliaji wa Simba,Emmanuel Okwi achonga pasi safi kabisa iliyozaa tunda la bao la kwanza.
Washabiki wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao.
Kikosi cha Simba.
Kikosi cha Kiyovu.









Ngoja Nyati aliyejeruhiwa atoke huko Cairo.Mtaipata na huo ushindi wenu wa kombe la kuku.
ReplyDeleteDavid V
tatizo wamevaa jezi zinazotaka kufanana na yanga, wangeuliza kabla.
ReplyDeletehaahaha acha wivu ila sasa mtakuja hapa algeria kucheza na etente de setif.jiandaeni hawajama mapafu ya mbwa wanacheza 90 bila kuchoka.tunawasubiri kuwashangilia nipo HAPA setif ALgeria.
ReplyDeleteYanga ndo tabia yenu,kila Simba ikishinda mnasema subirini watui fulani,nao tukiwashinda mnasema subirini watu fulani.
ReplyDeleteNdo maana hata ninyi mkicheza msitutake uzalendo wa kuwashangilieni.Tutashangilia timu pinzani tu.
Simba yasonga mbele mwaona donge.Zamalek imewashinda sasa mwaikandia Simba.Huko Algeria sisi hatuna wasiwasi kwani tulishawashinda si mara ya kwanza kucheza nao.
Naipongeza SSC kwa ushindi ila, timu ilichoka sana hasa kiungo. Nina mashaka makubwa na uwezo wa mwalimu kutengeneza stamina ya wachezaji. Sidhani kama Simba itaweza kushinda ikikutana na timu yenye nguvu.
ReplyDeleteKiyovu wameponzwa na Jezi (rangi ya kijani),,,wangelivaa hata Blue angalau!
ReplyDeleteSIMBA wanahitaji kuimarisha NGOME yao na pia wachezaji wengi hawana STAMINA.....Washambuliaji Okwi na Sunzu ni MOTO...!!!HONGERA SIMBA...!!
ReplyDeleteSimba kazeni buti wala msiogope timu za waarabu. Mpira uko kokote. Ila waarabu kwa vile Makao Makuu ya CAF yako Misri huwa wanajipendelea sana, kila mechi ni lazima wajipangie timu zao zianze ugenini n a kumalizia kwao. TFF hamlioni hili lalamikeni wafanye mabadiliko.
ReplyDeleteBongo Mpira bado maneno mengi kila mtu anajua kucheza na kila mtu ni kocha. Timfurani ikibahatisha kushinda wanachongaaa mpaka kero hivi sasa hawa jamaa wanajifananisha na Baca acheni upuuzi ninyi hamtafika popote mtakalia uchawi na maneno matupu.
ReplyDelete