Ankal michuzi salama lakini mimi nipo salama tu kuna swali hapa naomba wadau wanisaidie ni kuhusu hiki cheo cha mkuu wa sekritalieti ya halmashauri kuu ya chama na uenezi wa siasa nchini  nakumbuka sana nilikisikia mwanzoni kwa kingunge ngombali mwiru sifahamu sasa ni nani kashika hicho cheo kwa sasa Na wa sijui ni watanzania wangapi wanajua maana ya cheo hicho na kazi yake hapa nchini ntafurahi sana kupata majibu kwani nimesoma somo la siasa hapo zamani lakini sijawahi kusoma hiki cheo na maana yake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. 100% confidence levelMarch 03, 2012

    Kawaulize wazushi wenzio huko mitaani na siyo kwenye blogi hii ya jamii ambayo habari zake zinasomwa na watu weledi na of course wenye taaluma zao.
    Na Ankal michuzi, wauliza maswali kama haya uwe unawajibu kupitia e-mail zao wanazokutumia ujumbe kama huu ambao majibu yake wanaweza kuyapata kwa wazushi wenzao huko mitaani.

    ReplyDelete
  2. Mdau mara nyingi Madaraka na Vyeo vya Kisiasa hutolewa kwa Misingi ya Kugawana Madaraka na Kuridhishana.

    Hali hii pia hutokea ktk Mfumo wa Serikali inayoundwa ikiwa na Misuguano na yote ni ktk lengo la Kugawana Madaraka na Kuridhishana.

    Mfano unaweza kukuta Mtu akawa na Cheo kimoja na akaongezewa Kingine ili aridhike...kama ilivyotokea Kenya baada ya machafuko yaliyofuatia Uchaguzi mwaka 2007 ikawa Uhuru Kenyata akapewa Uwaziri wa Fedha na Makamu Waziri Mkuu kitu ambacho hata ktk Katiba yao hakikuwepo.

    Hivyo muundo wa Vyeo ktk Vyama vya Siasa na Serikali tete hutegemea upepo ulivyo pia majukumu yao au kazi zao hutegema Mipaka watayopangiana wenyewe.

    ReplyDelete
  3. Wadau, mtu kauliza swali kwa heshima kabisa, tunachopaswa kufanya ni kumjibu na kama hatuna majibu basi tunyamaze badala ya kulalama, sio lazima kila mtu apost comments hapa
    - kama huna cha kuongea nyamaza

    ReplyDelete
  4. huo ni utaratibu wetu sisi ndani ya chama chetu cha chukua chako mapema, sio lazima kila mtu ajue cheo hicho kina majukumu gani, tukiona kuna ulazima tunatengeneza nafasi ya cheo ili mradi tunaona kutakuwa na manufaa kwetu.

    ReplyDelete
  5. unauliza maana,just google,unauliza chama gani? vyama vyote vina website google, hata ukitaka cha uchina

    ReplyDelete
  6. mdau wa kwanza 100% hili swali huyu jamaa ndo maaana kaliita la kizushi sio lazima liwe na maana kwa watu wote kwangu mimi nadhani cheo hiko kipo katika chama cha ccm na kipo katika halmashauri kuu ila sijui wana maana gani labda kugawana madaraka

    ReplyDelete
  7. damn it!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...