Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Injinia John Ndunguru (mwenye shati la pinki) akiwa pamoja na Mainjinia wengine wa Wizara ya Ujenzi wakitoka ndani ya Kivuko cha Mv Magogoni mara baada ya Ukaguzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Injinia John Ndunguru (katikati mwenye shati la pinki) akiwa pamoja na Mkurugenzi msaidizi wa Ufundi,Injinia Ngome wakiwa ndani ya chumba cha Nahodha wa Kivuko cha Mv Magogoni wakipata maelezo kutoka kwa nahodha huyo wa kivuko cha Magogoni.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Injinia John Ndunguru wa (kwanza kushoto) akikagua moja ya Injinia ya kivuko cha Mv Magogoni jijini Dar es Salaam leo mchana.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Injinia John Ndunguru akikagua moja ya mlango wa kuingilia kwenye kivuko cha Mv Magogoni jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. It's great, but where is helmet? We better be serious for safety!

    ReplyDelete
  2. 100% confidence levelMarch 02, 2012

    Should i appreciate this kind of Motor Vehicle inspection for the Magogoni infrastructure.This kind of accountability however should go parallel with continuous mechanical maintenance for efficiency and effectiveness working of our infrastructures. Congratulation engineer Ndunguru for playing this role for the sake of users of the marine MVs.

    ReplyDelete
  3. bongo nzuri jamani, hebu ona watu walivyo na vitambi. tulioko ughaibuni huwezi kukuta tuna vitambi kama wenzetu mliobaki bongo. maboksi yananyausha mwili sio utani.

    ReplyDelete
  4. Imefaa hili zoezi la Ukaguzi wa Chombo !

    Tahadhari ni muhimu kabla ya Ajali kutokea.

    ReplyDelete
  5. Hahahaha Mdau wa Ughaibuni Anonymous wa Sat Mar 03, 03:26:00 AM 2012

    bongo nzuri jamani, hebu ona watu walivyo na vitambi.

    Majuu maboksi yanakondesha, yanatoa sugu mgongoni na kumtoa mtu vigimbi vya mikono ktk kuyabeba kwa uzito wake!

    Ni leo tumempaka Jamaa mmoja Mdau aliyepo Majuu akisema kuwa Bongo akiwemo Ankal Michuzi wamepigika na maisha ni magumu!

    Tumemjibu kuwa Bongo Tambarale, sawa shida zipo ila kila mtu ana mipango yake na pia wapo wana michongo ya fedha zao!

    ReplyDelete
  6. Kwani kuna ulazima wa kuanza kuwaita hawa jamaa injinia......., kwani ukisema Ndugu Nduguru tutakosa nini? If that is the case mbona hamsemi, mhasibu....,mwalimu........,mkulima....., mwandishi........secretary......mfamasia........,mwanajeshi.........mlinzi........ n.k

    Hilo neno litatia kichefuchefu, Ulaya haya mabo waliacha hata kuitana Dr. ama Prof hawataki siku hizi

    ReplyDelete
  7. Helmet ya nini mdau wa kwanza? wakati hapo unaona ni kivuko na sio construction site wala kiwanda, nyie ndo wale mnaokalili picha za viongozi wamevaa helmet wanapokwenda viwandani mkadhani ni utaratibu, hicho ni chombo cha abiria kama vile ndege, bus au meli sasa issue ya helmet hapo inakaaje sijui wakati unaona kabisa kivuko kipo katika kazi ya kutoa huduma na sio matengenezo

    ReplyDelete
  8. Nyie endeleeni kubeba maboksi huko Majuu, watu wanaota Vitambi huku na vyeo mikononi ninyi mkirudi hata Ujumbe wa nyumba kumi hatuwapi ni vile wengi mmesha saliti nchi mmeshaukana Uraia wa Tanzania.

    Tafrija mbili zilimfikisha Fisi na tamaa yake njia panda matokeo yake akataka kuhudhuria zote kwa pamoja akachanika msamba!

    ReplyDelete
  9. Wewe mdau wa Sat Mar 03, 02:17:00 PM 2012, huyo Injinia Ndunguru ameenda kufanya ukaguzi(Inspection)na msaidizi wake,ninavyo fahamu mimi na uzoefu nilio nao kwani mi mwenyewe kazi yng ni ya ufundi wa engine, walitakiwa wavae inspection gears, ili wasichafue mavazi yao au kuumia, si unaona wameingia mpaka kwenye engine ya hiyo vessel sasa chochote kinaweza kutokea, kujigonga, kujikwaa, kuchafuka...
    Sio unaingia engine room na mashati mmechomekea, vichwa wazi, hamna miwani ya kuficha uso...aaagh basi kibongobongo tu ili mradi mtu kaenda kuonesha sura tu! Sasa pipe ya oil ikipasuka ghafla oil ikatema moja kwa moja usoni kwako? Utasema nini? UZEMBE!!!
    Napita tu, tunafahamishana!

    ReplyDelete
  10. Inaleta moyo kidogo kuona uwajibikaji kama huu.

    Ila injinia angevaa hata glovu basi halafu japo akapapasapapasa ule mnyororo wa kunyanyua mlango wa feri na kushikashika vyuma vya mle ndani ya injini room!!

    Kuangalia kwa mbali hivyo au alikuwa hataki shati lake la pinki lichafuke?

    Mimi naona hapo ni kama vile ameenda for "Joy ride!!"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...