Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Sudi Madega (katikati) akitoa tamko la kusitishwa kwa maandamano ya amani kuelekea Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa yaliyotakiwa kufanyika kesho (3.3.2012). Wengine katika picha ni Afisa Habari na Uhusiano wa Kimataifa (TALGWU) Shani Kibwasali (kulia) na Afisa Habari Mkuu wa MAELEZO Mwirabi Sise . Chama hicho kimesitisha maandamano baada ya kufikia muafaka na Serikali.
Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
Chama cha Cha Wanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimesitisha maandamano ya amani yaliyokuwa yafanyike kesho kuelekea Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kuipa Serikali nafasi ya kutimiza kuwalipa wananchama madai yao.
Wanachama wa TALGWU wanadai Serikali malimbikizo mbalimbali ambayo ni jumla bilioni 26 ambayo yanahusiana na fedha za likizo, matibabu, malimbilikizo ya mishahara, madai ya fedha za kujikimu pamoja na gharama za masomo .
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania(TALGWU) Sudi Madega wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tamko lao la kusitisha maandamano hayo.
Madega amesema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya viongozi wa pande mbili kukutana, kujadiliana na kufikia muafaka ambapo Serikali imedai kupokea madai hayo , hivyo itahakiki na kuanza kuwalipa hivi karibuni.
Katika hatua nyingine , Katibu Mkuu huyo amesema kuwa wamepokea kwa masikito tukio la kuvunjwa kwa majengo ya Ofis mpya ya Halmashauri ya Bahi mkoani Dodoma kulikosababisha na watumishi kushindwa kuhamia katika majengo hayo kwa muda mrefu na kupelekea wananchi kuyavunja majengwa kwa hasira.
Amesema kuwa timu ya viongozi wa TALGWU inatarajia kutembelea Halmashauri zote zenye matatizo yanayofanana na hayo kama vile Uyui Tabora, Mvomero Morogoro na Bahi kwa ajili ya kuzungumza na uongozi wa Halmashauri hizo na Matawi TALGWU kisha kuishauri Serikali utaratibu wa kumaliza matatizo hayo.
mbona wamekaa kama wamefiwa jamani?
ReplyDelete