Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika Peter Allum (kushoto) kumaliza kuongea na waandishi wa habari kuhusu uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishawa na ukame mwaka 2011. Bwana Allum pamoja na ujumbe wake walikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika Peter Allum akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishwa na ukame mwaka 2011 kulia ni Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu. Bwana Allum pamoja na ujumbe wake walikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.
aadhi ya wajumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika wakimsikiliza Mkurugenzi msaidizi wa shirika hilo Peter Allum wakati akiwaelezea waandishi wa habari jinsi uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishawa na ukame mwaka 2011. Ujumbe huo ulikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.
Mjumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika ambaye jina lake halikupatikana mara moja akimrekodi kwa kutumia simu ya mkononi Mkurugenzi msaidizi wa shirika hilo Peter Allum (hayupo pichani) wakati akiwaelezea waandishi wa habari jinsi uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishawa na ukame mwaka 2011. Ujumbe huo ulikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.
Tanzania Oyeeeeee! Uchumi wake umekua!!!!
ReplyDeleteHawa mnawaamini bado? Nyerere amka baba wanatufuata bado.
ReplyDeleteMiaka hamsini ya uhuru bado tunapata msaada wa kisera!!! Mkopo huu nao tutaulipa? Aibu. Hawa wasomi wetu wako wapi? Hizi capacity building projects zimekuwa miradi ya wafadhili na mashirika ya kimataifa!!
ReplyDeleteUchumi Umekua???mwandushi na wewe ukaamua kutuletea habari hii na msisitizo kwa picha zote!!!!Aibu na iwe juu yenu!!
ReplyDeleteHahahah wenye nchi wamekuja kuchukua gawio lao!! Ama kweli Tanzania yangu imeshapotea!
ReplyDeleteHa ha ha,,,e e e, ukisikia Maajabu ya Mussa ndio haya!
ReplyDeleteUnaweza ukasoma gazeti au kitabu gizani?
Uchumi wa nchi unaweza kukua gizani?
Haya ni Mazingaombwe au ndio Sayansi ya Kiza anatuletea Prof. Ndulu na IMF?
Hawa IMF ndio walitushauri tusitishe JKT (National Servirce) ili eti kupunguza matumizi ya Serikali matokeo yake sasa nchi imekuwa Taifa la vijana Magoigoi, Matapeli, Wasichana Machangu,Wavulana Mashoga na Mateja,,,huku maadili yakianguka kwa kasi ktk Jamii yetu!
ReplyDeleteSASA HAWA NDIO WASHAURI WA KWELI?
Mwadila Mayo?,,,Genehe,,Ulimphola?
ReplyDeleteUliokua 'gizani' utakuwa ni Uchumi wa Nchi au Uchumi wa Usukumani?
Nchi zenye ''Energy & Power Per Capita'' kubwa ya Nishati (Uwiano kati ya idadi ya watu na uzalishaji wa nishati) zaidi yetu kama Italy na Spain zinafilisika Kiuchumi halafu sisi tuliokuwa gizani tunaimarika Kiuchumi?
Prof. Ndulu ahhh, ni kweli maneno yako na hao IMF?
Ukuaji wa Uchumi ndani ya giza:
ReplyDeleteInawezekana Prof. Ndulu anamaanisha kukua kiuchumi kwa misingi ya Idadi ya ng'ombe kuzaliwa na mavuno kwa Idadi ya magunia ya Karanga hukooo Usukumani!