Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika Peter Allum (kushoto) kumaliza kuongea na waandishi wa habari kuhusu uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishawa na ukame mwaka 2011. Bwana Allum pamoja na ujumbe wake walikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika Peter Allum akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishwa na ukame mwaka 2011 kulia ni Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu. Bwana Allum pamoja na ujumbe wake walikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.
aadhi ya wajumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika wakimsikiliza Mkurugenzi msaidizi wa shirika hilo Peter Allum wakati akiwaelezea waandishi wa habari jinsi uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishawa na ukame mwaka 2011. Ujumbe huo ulikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.
Mjumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Idara ya Afrika ambaye jina lake halikupatikana mara moja akimrekodi kwa kutumia simu ya mkononi Mkurugenzi msaidizi wa shirika hilo Peter Allum (hayupo pichani) wakati akiwaelezea waandishi wa habari jinsi uchumi wa Tanzania ulivyokuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa umeme uliosababishawa na ukame mwaka 2011. Ujumbe huo ulikuwa hapa nchini kwa ajili ya kufanya majadiliano ya mapitio ya awamu ya nne ya mpango wa msaada wa kisera.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Tanzania Oyeeeeee! Uchumi wake umekua!!!!

    ReplyDelete
  2. Hawa mnawaamini bado? Nyerere amka baba wanatufuata bado.

    ReplyDelete
  3. Miaka hamsini ya uhuru bado tunapata msaada wa kisera!!! Mkopo huu nao tutaulipa? Aibu. Hawa wasomi wetu wako wapi? Hizi capacity building projects zimekuwa miradi ya wafadhili na mashirika ya kimataifa!!

    ReplyDelete
  4. Uchumi Umekua???mwandushi na wewe ukaamua kutuletea habari hii na msisitizo kwa picha zote!!!!Aibu na iwe juu yenu!!

    ReplyDelete
  5. Hahahah wenye nchi wamekuja kuchukua gawio lao!! Ama kweli Tanzania yangu imeshapotea!

    ReplyDelete
  6. Ha ha ha,,,e e e, ukisikia Maajabu ya Mussa ndio haya!

    Unaweza ukasoma gazeti au kitabu gizani?

    Uchumi wa nchi unaweza kukua gizani?

    Haya ni Mazingaombwe au ndio Sayansi ya Kiza anatuletea Prof. Ndulu na IMF?

    ReplyDelete
  7. Hawa IMF ndio walitushauri tusitishe JKT (National Servirce) ili eti kupunguza matumizi ya Serikali matokeo yake sasa nchi imekuwa Taifa la vijana Magoigoi, Matapeli, Wasichana Machangu,Wavulana Mashoga na Mateja,,,huku maadili yakianguka kwa kasi ktk Jamii yetu!

    SASA HAWA NDIO WASHAURI WA KWELI?

    ReplyDelete
  8. Mwadila Mayo?,,,Genehe,,Ulimphola?

    Uliokua 'gizani' utakuwa ni Uchumi wa Nchi au Uchumi wa Usukumani?

    Nchi zenye ''Energy & Power Per Capita'' kubwa ya Nishati (Uwiano kati ya idadi ya watu na uzalishaji wa nishati) zaidi yetu kama Italy na Spain zinafilisika Kiuchumi halafu sisi tuliokuwa gizani tunaimarika Kiuchumi?

    Prof. Ndulu ahhh, ni kweli maneno yako na hao IMF?

    ReplyDelete
  9. Ukuaji wa Uchumi ndani ya giza:

    Inawezekana Prof. Ndulu anamaanisha kukua kiuchumi kwa misingi ya Idadi ya ng'ombe kuzaliwa na mavuno kwa Idadi ya magunia ya Karanga hukooo Usukumani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...