Na Mery Ayo,Arumeru

ZOEZI la kumtafuta mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki linaendelea ambapo kwa sasa wagombea nane kutoka katika vyama mbalimbali wamesharudisha fomu za uteuzi ambapo wamethibitisha kushiriki katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani humo msimamizi mkuu wa uchaguzi katika jimbo hilo Bw Trasias Kagenzi alisema kuwa wagombea wote hao wamedhibitisha kushiriki

Aidha Bw Trias aliongeza kuwa kwa sasa kampeni zitaanza Leo ambapo wagombea na wanachama wao wote wanatakiwa kufuata taratibu na sheria za uchaguzi ndani ya jimbo hilo

Alieleza kuwa ambao watashiriki ni pamoja na Bw Sioi Sumari (CCM),Joshua Nassari(CHADEMA), Shabn Moyo(SAU)Charles Msuya (UDPP), Abraham Chibaka(TLP),Abdlah Mazengo (AFP), Mohamed mohamed (DP) na Bw Khamisi Kihemu kutoka katika chama cha NRA

"hawa ndio waliochukua fomu na wote wamefanikiwa kurudisha foimu hizi kwa maana hiyo basi kitu kinachofuata hap ni kuhakikisha kuwa kila mmoja anafuta taratibu za uchaguzi ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na aina yoyote ile ya rushwa"aliongeza Bw Kagenzi

Pia katika hatua nyingine alisema kuwa majina ya wapiga kura yatabandikwa haraka iwezekanavyo ili kuweza kuruhusu kila mwananachi kujitambua kama yupo kwenye orodha hiyo ya wapiga kura ambapo majina ambayo yatatumika ni ya daftari la kudumu la mwaka 2010.

Bw Kagenzi alibainisha kuwa mbali na kutumia daftari la mwaka 2010 katika uchaguzi huo pia kwa sasa kuna vituo 327 ambapo watakaopiga kura ni watu mia moja na ishirini na saba elfu.

kwa upande wake mgombea kutoka katika chama cha mapinduzi Bw Sioi Sumarri alisema kuwa uchaguzi unatakiwa kuwa wa huru na haki na wananchi wanatakiwa kujiepusha na aina yoyote ile ya Rushwa pamoja na Vurugu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Huyu msimamizi wa uchaguzi Bw. Kagenzi ndiye aliyesimamia uchaguzi uliolalamikiwa sana na wapinzani kanda ya ziwa?

    ReplyDelete
  2. Wagombea nane wengi mno hata kama ni demokrasia

    David V

    ReplyDelete
  3. Vyama vya msimu...HUWA VINANIUDHII agh@#%&$?&*^?>@mara sijui SAU.mara AFP mara sijui upuuzi gani vinaibuka kwenye uchaguzi tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...