Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Bw. Nape Nnauye ametangaza majina ya waliopendeekzwa na halmashauri kuu kuwa  wagombea viti wa chama hicho katika bunge la Afrika Mashariki.

Kwa Tanzania Bara wanawake waliopendekezwa ni 12 wanaume 17 wakati kwa Zanzibar wanawake waliopendekezwa ni watano na wanaume wanane. 

Nape alisema vigezo vilivyotumika viko ndani ya chama hicho na kwamba chama kinajivunia kujitokeza kwa wasomi wengi kuwania nafasi hiyo wakiwemo vijana na akinamama. 

Aidha, alisema Kamati Kuu imeteua wajumbe watatu wa kusimamia uchaguzi huo ambao ni 
Abdulrahman Kinana, yeye mwenyewe Nape na Dogo Mabrouk. 

Alitaja wanawake waliopendekezwa kwa Tanzania Bara kuwa ni Janeth Mmari, Janet Mbene, Fancy Nkuhi, Nora Mukami, Shally Raymond, Shy-Rose Bhanji, Ngollo Malenya, Godbertha Kinyondo, Hamidah Kalua, Angela Kizigha, Happiness Lugiko na Ruth Msafiri. 

Kwa upande wa wanaume Bara aliwataja Dk. Aman Kabourou, John Ngongolo, Dk. Evans 
Rweikiza, Siraju Kaboyonga, Benard Murunya, Dk. Edmond Mndolwa, Christopher Awinia na 
Dk. Hilderbrand Shayo. 

Wengine ni Makongoro Nyerere, Adam Kimbisa, Elibariki Kingu, Simon Berege, Mrisho Gambo, Handley Mafwenga, William Malecela, Mussa Mnyeti na Godfrey Mosha. 

Wanawake waliopendekezwa upande wa Zanzibar ni Septuu Mohammed Nassor, Safia Ali Rijaal, Rukia Seif Msellem, Sabah Saleh Ali na Maryam Ussi Yahya. 

Wanaume Zanzibar kwa mujibu wa Nape ni Dk. Said Gharib Bilal, Abdallah Ali Mwinyi, Dk. Haji 
Mwita Haji, Dk. Ahmada Hamad Khatib, Zubeir Ali Maulid, Khamis Jabir Makame, Abdul-Aziz Salim na Mbwana Yahya Mwinyi. 

Bunge hilo kwa sasa lina wajumbe 52, wakiwa tisa kutoka kila nchi mwanachama wa EAC 
pamoja na wajumbe wengine saba wanaoingia kwa nafasi zao. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...