Meneja wa Kanda ya Kaskazini Mashariki wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kasilo Msangi akizungumza na waandishi wa habari katika kiwanda cha TBL mkoani Arusha mwishoni mwa wiki, kuelezea mafanikio makubwa ya kampuni hiyo kwa kanda hiyo.
Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi (kushoto) akimkabidhi zawadi ya katoni tatu za bia mwandishi wa gazeti la Majira, Pamela Mollel ambaye alishinda shindano la kutambua radha za aina mbalimbali za bia zinazozalishwa na kampuni hiyo. Shindano hilo lilikutanisha wanahabari wa Mkoa wa Arusha mwishoni mwa wiki.
Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edithi Mushi (kushoto), akimkabidhi zawadi ya bia Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani wa Arusha (APC), Graud Gwandu baada ya kushika nafasi ya pili katika shindano la kutambua radha za bia za aina mbalimbali zinazozalishwa na TBL, katika shindano lililokutanisha wanahabari wa mkoa huo mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Arusha, wakitembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) mkoani Arusha, mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. duh mwanamke kushika nafasi ya kwanza kwa kuonja bia! noma!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...