Meneja Mahusiano kwa Umma na Habari za Mtandao wa Vodacom Tanzania Bw. Matina Nkurlu akionesha nambari za washindi 100 wa droo ya siku ya promosheni ya M-PESA waliojishindia Sh. 50,000 kila mmoja. Wanaoshuhudia ni Mtaalamu wa huduma za ziada kwa wateja wa Vodacom Bi Reenu Verma na Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Bw. Bakari Maggid.Droo hiyo imechezeshwa leo jijini Dar es salaam.
Mkaguzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Bw. Bakari Maggid akirekodi taarifa za washindi 100 wa droo ya siku ya promosheni ya M-PESA waliojishindia Sh. 50,000 kila mmoja baada ya kuchezeshwa na Mtaalamu wa huduma za ziada kwa wateja wa Vodacom Bi Reenu Verma(katikati) leo jijini Dar es salaam.. Kushoto ni Meneja Mahusiano kwa Umma na Habari za Mtandao wa Vodacom Tanzania Bw. Matina Nkurlu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...