Mkurugenzi wa fedha wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Kalpesh Mehta(wa kwanza kushoto) akikabidhiwa jezi namba kumi ya timu ya Manchester united na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Quinton Fortune katika hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kuwawezesha wateja wake zaidi ya 200 kushuhudia live kombe la ligi kuu ya uingereza ambalo limeletwa na timu ya manchester united kushirikiana na Airtel nchini Tanzania, katikati ni mchezaji mchezaji mstaafu wa timu ya Manchester united Gary Bailey hafla hiyo imefanyika katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam mwisho wa wikiendi hii.
Mkurugenzi wa dawati la ufundi wa shirikisho la soka Tanzania Bw.Sunday Kayuni akikabidhiwa jezi namba tisa ya timu ya Manchester united na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Gary Bailey katika hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kuwawezesha wateja wake kushuhudia kombe la ligi kuu ya uingereza ambalo limeletwa na timu ya iManchester united kushirikiana na Airtel nchini Tanzania, wa kwanza kulia ni mchezaji mstaafu wa timu ya Manchester united Quint Fortune, hafla hiyo imefanyika katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam mwisho wa wikiendi hii.
Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania Bw,Juma Pinto na mshabiki mkubwa wa timu ya Liverpool akiwa amevalia jezi ya Manchester United mara baada ya kukabidhiwa jezi hiyo na wachezaji wa zamani wa timu ya Manchester united katika hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kuwawezesha wateja wake kushuhudia kombe la ligi kuu ya uingereza ambalo limeletwa na timu ya Manchester united kushirikiana na Airtel nchini Tanzania, kulia ni mchezaj wa zamani wa timu ya Manchester united Quinton Fortune na kushoto mchezaji wa zamani wa timu hiyo Gary Bailey,hafla hiyo imefanyika katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam mwisho wa wikiendi hii.
Waandishi wa habari za michezo wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na kombe la ligi kuu ya uingereza katika hafla fupi iliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kuwawezesha wateja wake kushuhudia kombe la ligi kuu ya uingereza ambalo limeletwa na timu ya Manchester united kushirikiana na Airtel nchini Tanzania,hafla hiyo imefanyika katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam mwisho wa wikiendi hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Haya Kiongozi Juma Pinto kazi kwako Jezi ya Man U,,,unaisikia inawasha mwilini?

    Wala Usiwe na wasiwasi !!!

    Unaonekana kama vile unahamishwa kutoka Anfield kwenda Old Trafford !

    ReplyDelete
  2. Wala usijali upo ktk uenezi wa kimajukumu:

    Kiongozi Juma Pinto picha ya kwanza unakuwa kama unavalishwa Jezi ya (Man UTD) iliyoshonwa kwa Gunia chafu la mkaa!

    Ama kweli ni umkweli na mwaminifu kwa Liver unaona kama unalisaliti Chama vileee?

    ReplyDelete
  3. Hahaha Pinto,

    Uzi wa Man-U

    Unakuwa kama unavalishwa ngozi ya mbuzi aliyekufa bila kuchinjwa kisheria !

    ReplyDelete
  4. Ahhh Juma Pinto !!!

    Uhamisho kutoka Anfield to Old Trafford !

    Au jamaa wa Man U wamekuletea Cheki ya POUNDS au nini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...