Ankal na mdau John Ulanga wa The Foundation for Civil Society (BOFYA HAPA) wakiwa na Rais Mstaafu wa Nigeria Jenerali Olesegun Obasanjo uwanja wa ndege wa Sao Paulo nchini Brazil leo. Jenerali Obasanjo, aliyekuwa anatoka Brazil kuelekea Afrika Kusini, alishangaza wengi kwa kuja kukaa na akina ankal kwenye sehemu ya kusubiria safari kwa abiria wa 'ecocomy class' badala ya kwenda kungojea muda wa safari katika Lounge kama ilivyo kawaida kwa wasafiri wenye tiketi za daraja la kwanza. Isitoshe alikula stori na Ankal na John kwa namna ambayo haikuwa rahisi kumaizi kuwa huyu ni mkuu wa nchi mstaafu. Ila aliapotua jijini Johannesburg tu, Jenerali Obasanjo hakuwa mwenzao tena, maana maafisa ubalozi na wana usalama wa Sauzi walimzingira na kumpeleka VIP chapchap....
Home
Unlabelled
ankal na mdau john ulanga uso kwa uso na jenerali obasanjo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Safi sana Ankal! Kumbukumbu nzuri hiyo :)
ReplyDeleteHope you had a good time bro.
Mdau
Buckinghamshire
naona hata mobile phone ana ya mchina
ReplyDeleteTrue leader and gentleman,mtu wa watu kweli.
ReplyDeleteNimeipenda FULANAZZZZ! AKAL nitahakikisha unainadi na nitainunua . Taswira makini hii
ReplyDeleteHizo nguo alizovaa ni nguo za kulala au????
ReplyDeleteAnkal hako kafulana ka mistari mistari tena msalie mtume basi nipe mimi angalau nipate mavumba ya jenerali obasanjo umekashika kafulana hako muda mrefu sasa au kana dawa ya babu wa kikombe unakapenda najua nitumie mimi kwa anuani hii nijaribu bahati yangu labda nitapata kuonana na pope benedict.
ReplyDeletemdau.
mongolia.
jamani huko ulaya wana mambo hakuna VIP? au na nyie vile mlikuwa na JK ndo Ma VIP wenyewe?
ReplyDeleteAnkal Obasanjo kuja kukaa na ninyi ana lake jambo sio bure.
ReplyDeleteKtk maongezi mliyofanya naye hapo muda wote huo atakuwa amepata kitu au alikuwa anatafuta kitu!
teh!teh! Ze fulanazzzzzzzzzzzzzz!! ituwakilisha babu kubwa
ReplyDeletewadau FFU
Ankal the Fulanas umepewa na babu wa loliondo nini? Naona haitoki ukiwa unaenda majuu tu ipo mwilini au ndio nguzo ya kukulinda usipate balaa tetethhhetetetehh.nafikiri sasa imefika wakati tuifanyie mazishi ili tuiweke kwenye jumba la makumbusho.
ReplyDeletewatanzania kweli ni wasafiri yani wapo kila kona ya dunia na ukiangalia nchi yao haina hata vita useme wamekimbia vita
ReplyDeletesasa wewe mdau uliopo huko MONGOLIA kweli kiboko na ni shujaa mmmh wabongo noma.
Mr Ulanga uko juu sana kuendeleza The Foundation Civil Society, tunahitaji watendaji wa kujituma kama wewe,Hongera sana.
ReplyDeleteze fulanazzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
ReplyDeleteAnkal sio bure hiyo 'fulanazzz' ni ya Tambiko!
ReplyDeleteJamaa walikushuhudia ulipokuwa Ujerumani miaka kadhaa ukiwa unaifua kwa mikono fulana kwa maji na sabuni bila washing and drying machine !
Je ni kweli hiyo ni fulana ya kawaida?