
John Heche Mwenyekiti wa BAVICHA
---
BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) kwa masitiko makubwa linachukua fursa hii kutoa salaam za rambirambi na pole za dhati kwa vijana nchini na hususan kwa wasanii wa fani mbalimbali kwa msiba wa mmoja wa waigizaji mahiri, Steven Charles Kanumba.
BAVICHA inamtambua kijana Kanumba kuwa mmoja wa vijana wapambanaji ambao pamoja na serikali kushindwa kuboresha mazingira ambayo wasanii wangeweza kunufaika na kazi zao ipasavyo kama moja ya maeneo muhimu ya ajira yenye staha, yeye na wenzake wachache walimudu kupambana na vikwazo vingi hata wakaweza kuikuza na kuipatia jina, tasnia ya uigizaji nchini.
BAVICHA tunatambua juhudi binafsi za Kanumba na wenzake, ambazo zilisababisha vijana wengine kuweza kupata ajira kutokana na kazi zinazotokana na mchakato wa hatua mbalimbali za ukamilishaji wa filamu, kuanzia katika utungaji, utengenezaji hadi hatua ya uuzwaji wa filamu hizo.
Kwa dhati kabisa, BAVICHA inapenda kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na kwa Watanzania wote kwa ujumla walioguswa na msiba huo. Tunawaombea kwa Mungu, awajalie moyo wa subira wakati huu wa majonzi makubwa.Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Marehemu Kanumba, Amina.
Imetolewa kwa vyombo vya habari na
John Heche
Mwenyekiti wa BAVICHA


sasa chadema mmefilisika kisera siasa mpaka kwenye msiba badala ya kutoa rambi rambi mnajitafutia cheap popularity , Kanumba ni kipenzi cha watu wote ndani na nje ya nchi.chama chenu kikikosa sera basi kinabaki kudandia matukio misiba, migomo na maandamano, kwenye katiba Jk Amewafunga gori la kisigino, Tuache siasa tuomboleze maana huu msiba umetuunganisha, rest in peace my hero, indeed, Kanumba was the great.
ReplyDeleteMnamlilia vipi Kanumba kwa kuweka picha ya mwenyekiti wenu!? Orbituary zote kwa kawaida unaweka picha ya marehem!
ReplyDeleteAu ndo kujitafutia umaarufu!!
Amina.
ReplyDeletewatu wapo kwenye msiba nyie mnaanza serikali hivi mara vile,kila kitu siasa tu tushawachoka.
ReplyDeleteNadhani angepaswa kuonekana anasaini kitabu cha rambirambi ingeleta maana zaidi.
ReplyDeleteR.I.P Steve wetu
Hahahahah,
ReplyDeleteSiasa za Kiusanii ndio hizi Chadema?
Chadema wana lengo lao ukiona hivyo, sio ajabu ukasikia walitarajia kumsimamisha Marehemu Steve Kanumba Jimbo la Uchaguzi Shinyanga Mjini mwaka 2015 isipokuwa kifo chake kimewakatisha !