Mahakama Kuu ya mkoa wa jijini Arusha imemvua Ubunge aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA,Godbless Lema (pichani) mapema leo asubuhi.
Ripota wa Globu ya Jamii aliyeko eneo la tukio anasema kuwa uamuzi huo umetokana na kesi ya kupinga matokeo iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Godbless Lema iliyokuwa ikiendelea mkoani humo.
Ripota wa Globu ya Jamii aliyeko eneo la tukio anasema kuwa uamuzi huo umetokana na kesi ya kupinga matokeo iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Godbless Lema iliyokuwa ikiendelea mkoani humo.
Habari zaidi kuhusu tukio hilo na hali ilvyokuwa wakati wa uamuzi wa mahakama jijini Arusha tutawaletea hivi punde.
pia sikiliza hapa kuhusiana na tukio hilo
Na Dixon Busagaga,Arusha.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya arusha leo imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA.
Uamuzi huo umefikiwa Aprili 5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo.
Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).
Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa wa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.
Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo nawadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5
kujitetea.
Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado cham hicho kipo katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani humo.
Tutaendelea kufahamishana zaidi
Na Dixon Busagaga,Arusha.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya arusha leo imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA.
Uamuzi huo umefikiwa Aprili 5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi wa Mbunge huyo.
Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).
Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa wa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.
Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao katika mahakama hiyo nawadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5
kujitetea.
Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado cham hicho kipo katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki mkoani humo.
Tutaendelea kufahamishana zaidi



kulaaaaaaaaaaaaaaaaaaaleeeeeeeeki
ReplyDeleteArusha ni ya Chadema... Atarudi kwa kishindo!
ReplyDeleteAnother election coming - hizo hela zitakzotumika zingeweza kujenga sekondari 300 enough to educate every student in Tanzania. We are wasting monies on these by-election. Lema atashinda tena, losers in sisi wananchi maana tunkosa hela za maendeleo. wake up Tanzania by elections are a waste of time.
ReplyDeleteKilichosababisha GodBless Lema kuvuliwa ubunge sio RUSHWA, bali ni matusi na kashfa. Ook. Let's wait after 90days, Mungu ibariki Tz.
ReplyDeleteNilikuwa najiuliza hivi ni kwa nini CCM walikubali matokeo ya Arumeru Faster Faster.
ReplyDeleteSasa Nimeelewa Mkakati uliowekwa!
kuna maana gani kumvua mtu ubunge na kumruhusu kugombea tena wakati kuna uhakika mkubwa atashinda tena? hizi hela za kampeni za kuchezea tunazipata wapi? I am so disappointed
ReplyDeleteI fail to understand how matusi yanavyoweza ku-affect matokeo ya uchaguzi. I thought Lema would have lost if he was using bad language. Ooohhh majaji zetu wabongo nao wanatia mashaka!!!
ReplyDeleteLusinde Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteHukumu ilishapangwaa longtime so hawakujua nini kitatokea Arumeru Mashariki. Lugha za matusi na kejeli kwa Lema what about MATUSI ya Lusinde???Anyways atapata tu unless otherwise....!!!!
ReplyDeleteAMA KWELI SIASA NI MCHEZO MCHAFUUUUU…! HEBU WAZEE KAENI PEMBENI ILI MUWEZE KUWA WASHAURI WETU; LAKINI KWA STYLE HII YA KUNG’ANG’ANINIA MADARAKA KWA KUKAA NYUMA YA PAZIA HATUTAFIKA POPOTEE... CCM NAIPENDA LAKINI PALE AMBAPO KUTWA WAO WAKO PALE KWA MALENGO YAO BINAFSI NDIPO NINAPOCHOKA. NADHANI UMEFIKA WAKATI WA WAKUJIVUA GAMBA KWA VITENDO NA SI KWA MANENOOOOO….. NAJUA HATA KAMA LEMA LEO ATAONDOKA LAKINI BADO JIMBO LITABAKI KUWA LA UPINZANI.
ReplyDeleteCHA KUSHANGAZA KUNA VIONGOZI KADHAA TOKA MIAKA YA 1970 MPAKA SASA UTAKUTA BADO MAJINA YAO YAPO KWENYE UONGOZI KANA KWAMBA BILA WAO NCHI HAITAKWENDA, HIVI VIJANA WATAJIFUNZA LINI… MARA MWENYEKITI WA BODI, MKURUGENZI, MBUNGE, WAZIRI N.K.!!! WAZEE WETU (BAADHI, MNIWIE RADHI SI WOTE) MMEKUWA VING’ANG’ANIZI WA UONGOZI MPAKA MNAKERA. WENZENU WAMEKUBALI UMRI WA KUACHIA NGAZI UMEFIKA NA WAMETOKA KWA AMANI, NA WAKO MITAANI, VIJIJINI NAFURAHIA MATUNDA YA JASHO. HAWANA PRESSURE, KISUKARI, N.K.
NADHANI UMEFIKA WAKATI TUWEKE UKOMO WA UONGOZI, KWANI NAONA HATA WENGINE WAMEONA ILI WAENDELEE KUWA JUU LAZIMA WARITHISHE WATOTO WAO.
WANDUGU HILI TABAKA AMBALO MMESHALIZALISHA (KATI YA WALIONACHO NA WASIONACHO) HAMLIONIIII….!!!! MSIPOFANYA JUHUDI ZA MAKUSUDI KULIONDOA ITAKUWA KWENU.
HAYO MAMBO YA KUJIDAI SIE MASAKI, OYSTERBAY, MBEZI BEACH KUWA NDIO BORA NA WANAOSTAHILI KUWANACHO HAWA MBAGALA!!! TEHE TEHE!!! KUNA SIKU WATAINUKA NAO WADAI CHAO!!!
fungeni milango tupigane
ReplyDeleteSaaaaaaaaaaafi na inapendeza, ngebe zimekatwa!!
ReplyDeleteHuko tunapoenda huu usemi wa "Mungu ibariki Tanzania" wakati tunafanya upuuzi mtupu, Mungu atachoka nao. Ni maoni tu kutoka Uholanzi.
ReplyDeleteMMH.. PESA ZA WALIPA KODI NDIZO ZITANDELEA KUCHEZEWA NA KUTUMIKA KWENYE UCHAGUZI MPAKA LINI……!!!
ReplyDeleteSERIKALI INAVITU VINGI VYA KUWAFANYIA WATANZANIA AMBAO SASA NAONA INATAKA KUWAGEUZA KUWA WADANGANYIKA!!!
WAKATI UMEFIKA WATANZANIA TUSIMAME NA TUUNGANE KUPINGA MAMBO HAYA AMBAYO SERIKALI INATUPOTEZEA MALENGO YA KUTIMIZA WAJIBU KWA WANANCHI WAKE.
HALI YA UCHUMI WA TANZANIA INATISHA SANA, SERIKALI INABIDI ITAMBUE KUWA HALI NI MBAYA NA WATU NAKULA MLO MMOJA, MAHOSPITALI HAYANA MADAWA, SHULE HAZINA MADAWATI, VITABU NA WALIMU ITAWEZAJE KUKOMBOA WATU WAKE?
HIVI HII SERIKALI YETU KWELI INA MALENGO KAMA JIBU NI NDIYO HAYA MBONA SASA HIVI IMEKALIA KWENYE UCHAGUZI TU KANA KWAMBA HAMNA LINGINE LA KUFANYA.
WATANZANIA TUSIMAME TUSIKUBALI KUWA WADANYIKA BALI WATANZANIA TUAMKE KWENYE HUU USINGIZI MNONO KWA SAUTI MOJA TUIWAJIBISHEEEE ….
NAJUA MTASEMA NINACHANGANYA SERIKALI NA CHAMA LAA!! VIONGOZI WALIOKO SERIKALINI NDIO HAO TUMEWAONA WAKIJA ARUSHA KI CHAMA. ZIARA ZA KICHAMA WANAKUJA NA MAGARI YA SERIKALI… !!!
LEMA NA CHADEMA WAKIAMUA KUINGIA KWENYE MPAMBANO NAMSHAURI LEMA APUNGUZE KIDOMODOMO.....WEKA SERA SAFI ZA CHADEMA MBELE MAMBO USIWAPE HAWA JAMAA ZETU WA CCM SABABU!!!
ReplyDeletewe anoy 12:21 matusi ni baadhi ya 'bad language'
ReplyDeleteOhh POor Tanzania! Why this? Kwann basi msingejuzia matokeo kipindi kile kile kile cha uchaguzi? why now?
ReplyDeletePlz haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma kha! hali ya uchum yenyewe mbovu, maisha magum kwa walio wengi halaf mkaharib tena pesa nyinginekurudia uchaguzi!Hamuwez kushinda acheni kutuharibia maisha zaidi .We are tired with this government!!!
Kwa tathmini yangu niliyofanya Arusha ni CHADEMA hata iweje, tofauti na hapo hofu yangu ni usalama wa raia wa wasio na hatia hapa arusha watapata taabu endepo zitafanyika namna tofauti. vile vile maisha kwa watanzania yatazidi kuwa duni ukizingatia ni mabilioni mengi yanatumika ktk uchuguzi kwa ajili ya maslai ya wachache. Inajulikana kabisa na wananchi kuwa jimbo la arusha kuchukuliwa na upinzani ilikuwa kero kubwa kwa chama tawala. Wito wangu kwa serikali yangu na tume itakayosimamia uchaguzi huo haki itendeke ili kuleta amani na utulivu vinginevyo maumivu yote wanayoyapata wananchi kwa kukosa huduma muhimu kwa sababu za maslai ya watu wachache hukumu yake ni hapahapa Duniani.Tumuombe Mwenyezi Mungu mambo yote yafanyike kwa mapenzi yake ili tudumishe amani yetu watanzania.
ReplyDeletewenye taarifa za hali arusha watupe data
ReplyDeleteHapo naona wanamtafutia umaarufu Bw. Lema maana iko waziiiiii Chadema watashinda tuuu si ukweli umeonekana hata kwenye viti vya udiwani na hicho cha Arumeru. Hela zetu walipa kodi kwa kweli zinachezewa. Kwa mantiki hii hiyo sheria ya uchaguzi inabidi iangaliwe upya. Mi sielewi na je wale wanaongea matusi wakati wakimnadi mgombea wao wanachukuliwa hatua gani? Tumeona uchaguzi wa Arumeru baadhi ya viongozi wametumia lugha chafu ambazo haizifai kusemwa mbele ya watoto au kusikiwa na mataifa mengine kwani ni vitu vya aibu.
ReplyDeleteArusha Mjini:
ReplyDeleteKiti kinarudi CCM piga ua , si mmeleta Ujanja kuchukua Arumeru Mashariki huko shamba?,,,sisi ni watu wa Mujini babake!
Jaji Mfawidhi aliyetoa hukumu au waliofungua Mashitaka wamesahau:
ReplyDeleteAliyevuliwa Ubunge ameshazungumzwa kuhusiana na Uhalifu (magari na silaha za moto),,,nadhani Faili lake liongezwe pale ili ikiwezekana hata kupendekezwa Kugombea tena asipate kabisaaa!
Wembe ni ule ule!
ReplyDeleteMnacheza na CCM siyo?,,,MTACHEMSHA MAWE MWAKA HUU.
HADI UCHAGUZI MKUU 2105 MTABAKI NA (SIFURI) TUTAKUWA TUMEWAVUA VITI VYOTE!
Jamani let us be seriuos kwa hili, wafanye wafanyavyo chadema itaendelea tu kutawala jimbo la Arusha Mjini.
ReplyDeleteKTK HUKUMU ILIYOTOKA:
ReplyDeleteZaidi ya lugha chafu haya hapa yazingatiwe:
1.Kutajwa kwake kuhusika na uhalifu
2.Kiwango cha Elimu yake ni utata
3.Mwenendo wake kiujumla ni utata
(kabla ya Ubunge alioupata kwa bahati hakuwa na shughuli zinazoelewaka)???...Mwenzi Sugu Mr.II anajulikana alitokea ktk fani ya Muziki yeye je?
! ! !
Vyovyote vile itakavyokuwa kilio cha wengi ni sauti ya Mungu. PIA USICHEZE NA NGUVU YA UMMA
ReplyDeleteAjiandae kwa kazi hizi 3 za haraka!
ReplyDelete1.Akalime Kahawa Mlima Meru!
2.Aandae leseni kaendeshe Bodaboda!
3.Awe Dereva wa Landcruiser lake kubeba wanaoenda Samunge kwa Babu kupata kikombe!
Wacha Mchezo na CCM, ukikoswa na Nyundo nzito Kilo 49 utosini mwa kichwa chako,,,Jembe lenye makali litatua shingoni kwako!
ReplyDeleteHabari ndio hiyo:
ReplyDeleteEndeleeni sasa na Sherehe za Ushindi Arumeru Mashariki!
Kama kuna haki basi Mhe. Kushinde avuliwe ubunge maana ametumia matusi sana kwenye kampeni za Arumeru....chaguzi ndogo zitatufanya maskini jamani....tuamke Watanzania
ReplyDeleteCHADEMA imarisha kampeni zaidi ya, Arurume Mashariki ili kulitwaa jimbo tena la Arusha.
ReplyDeleteHata kama ukirudiwa tena kwa asilimia 100% nawahakikishia kuwa CHADEMA ya Lema itashinda TU!
ReplyDeleteKama matusi ni kigezo kimojawapo basi ni dhahari LIVINGSTONE LUSINDE ameshapoteza tayari kiti cha ubunge Mtera!
ReplyDeletemimi nichadema damu lkn simkubali Lema ana jazba kashfa hana nidham kiukweli jamaa hafai.
ReplyDeleteHivi kweli tuna serikali? Sielewi kabisa, hii ndio sababu uliyowafanya CCM kuwapa jimbo la Arumeru CHADEMA, then uchaguzi ufanyike Arusha ili hapo CCM wachakachue halafu waseme mbona sisi tulikubali matokeo ya Arumeru. Mimi sipo kwenye chama chochote, lakini naona tunakokwenda si kuzuri sasa. Nchi masikini kurudia uchaguzi bila sababu ya msingi. Huu ni ujanja ambao hata mtoto mdogo anauona ulivyowazi! CCM mnataka kufanya nini?! Kweli nyinyi ni wapenda amani? Patakuwa na Amani hapo kwa style hii?! Mungu wetu tuangalie watanzania kwa jicho la huruma.
ReplyDeleteWatu walikuwa wanashangaa matusi ya Lusinde kwasababu karekodiwa. huyu hawasemi. Lusinde alisema ngumi ya kulipiza inauma zaidi. Huyu jamaa alidai Lowasa hawara yake Dr Batilda. hii siyo kazi ya kanisa....hahahahahahahahha. Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeleteSerikali ya TZ inahela wengi sana wa kuchezea kwa ajili ya chaguzi ndogo na uchaguzi kwa ujumla, kwa jimbo la arumeru kulikua hamna haja ya kupoteza pesa na kuitisha uchaguzi mpya kama katiba ingekua sawa, ilibidi mtu wa pili kwa uchaguzi wa kwanza ndio angeshika nafasi ya ubunge, kwa Lema kumvua ubunge na kuitihsa uchaguzi tena huku Lema mwenyewe akiwa eligible kushiriki ni sawa na kufanya hamna kitu maana atashinda tena na hilo liko wazi. Ni kwamba serikali ya bongo ina pesa za mchezo na watu wake wana muda mwingi wa kupoteza for nothing.
ReplyDeleteUbunge wa Arusha Mjini:
ReplyDeleteKwa Panga butu 'Mchagga' amenyolewa leo asubuhi,,,kaeni kimya mpatiwe Mbunge mpya wa CCM muda si mrefu, na mkileta ujinga mtakimbiana mkijikuta kwa miguu mnakimbilia Kenya !
Mkifika Kenya mtamkuta Ubalozini Mhe. Balozi Mteule Dr. Batilda S. Burian atawakodishia Lori la Fuso na kuwarudisha tena Arusha !
Kituuuuu,!
ReplyDelete'MNEMBA' UMEZAMA HADI NDANI!
BAO LIMEZAMA KIMIANI NYAVU ZINATIKISIKA!
CHADEMA Imekula kwenu!,,,NA KWA TAARIFA YENU JIMBO LA ARUSHA MJINI LINARUDI C.C.M MTAKE MSITAKE!
HATA KAMA WATAKAA WATATU KWA MPIGO WAKISIMAMA KAMA MMOJA 1.Freeman Mbowe ,2.Zitto Kabwe,3.Dr.Wilbroad Slaa JIMBO LAZIMA LIENDE C.C.M!
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
Kisuuuuuuuu!
ReplyDeleteDuhhh ah Mchagga anakwenda kulima !
Ahhh wapi wala hana wasiwasi baada ya kuukosa Ubunge atarudi kwenye kazi yake ya zamani (magari+silaha za moto)
ReplyDeleteAsalaleee,
ReplyDeleteJamani wimbi la Ujambazi litafumuka tena Arusha kama mnavyoona ajira zilipatikana hadi Bungeni na sasa watu wanarudi Mtaani patakalika kweli?
kwanini tuna ushabiki mwingi wa vyama badala yakuangalia maslahi ya nchi.Tuchague wabunge watakaoleta mafanikio katika nchi yetu bila kuangalia chama wanachotoka so far wachache wa opposition party wanachangamsha Bunge. Mimi nafurahia multipartism kwasababu najua inaleta changamoto bungeni kama tukipata wabunge nusu wa Chadema katika bunge najua Tutapata mafanikio Tanzania.
ReplyDeletekwakweli miminapenda sana chadema kwa sababu inachangamsha ccm na kuwaamsha lakini lema hapana wengine sina shida nao lema fujo mingi hasira isiyo na mipaka hana ustaarabu nina mashaka na elimu yake pamoja na ccm ni wabaya sana lakini sio hivyo lem anenda resi sana enewe tungoje tuone itakavyokuwa
ReplyDelete