Assalam allaikum Ankali michuzi. tafadhali nisaidie kutundika tangazo langu la kazi ili niweze kuanza huu ujasiliamali wangu.
natafuta kijana wa kitanzania ambae ataweka maskani Dodoma kwa ajili ya kazi ya Bakery. Awe amesomea VETA na ana ujuzi wa wa kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotokana na unga wa ngano. awe mchapa kazi na awe tayari na mwepesi wa kujifunza.
Shukrani ankali michuzi


Wasomi MPO?
ReplyDeleteNaona taarifa imetoka tangu jana kimyaaa, sasa je akija Mkenya, Mnyarwanda,Mmalawi au Mganda akaomba akapata mtamlaumu nani?
Kazi ni kazi bora mkono wende kinywani ili mradi iwe halali!
Unaweza kuanzia Bakery ya Mikate Dodoma halafu ukatafuta pengine huku ukijishikiza!
Tena kwa sehemu ndogo kama hii ndio utajifunza mengi sana na ya faida kitaaluma,,,sio utegemee kuanzia juu kama TRA au Vodacom na Benki kwa vile umesoma.