Steve,
Naandika kukujivya kwamba mimi na kikosi kizima cha Globu ya Jamii tulikuwapo katika shughuli ya kukuaga pale Leaders Club na baadaye makaburini Kinondoni jijini Dar es salaam katika nyumba yako ya milele.
Turuhusu maisha yaendelee kama kawaida wakati wewe umeshatangulia mbele ya haki. Taswira hizi zilizizonaswa na mpiga picha wetu mpya wa Globu ya Jamii, Steve, na nyinginezo kule katika libeneke la MATUKIO-MICHUZI ndizo ambazo kwa sasa tunazofungia pazia katika kusherehekea miaka 28 ya maisha yako. Buriani.
BOFYA HAPA
-Michuzi



Uncle kwanza nakushukuru sana na timu yako kwa kutupa tukio hili katika picha, inasikitisha sana.
ReplyDeleteBaada ya hapo naomba kuuliza kwa wale waliokuwa karibu na bwana Kanumba kikazi, alishiriki katika filamu ngapi? Nimesikitika kwamba nimemfahamu zaidi baada ya kututoka. Ni swali tu sina hoja yoyote ya siri.
Mungu amwangazie nuru ya milele
Huu ni MFANO wa kuigwa kwetu sote kwa maisha ya Kanumba na jinsi alivyotumia kipaji chake. Mimi ni mdau niko USA ,TEXAS, nimefukifuatilia huu msiba na jinsi ulivyotugusa, inaonyesha namna gani alivyokuwa wa PEKEE.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu baba ailaze roho ya Marehemu Pema Peponi.
MICHUZI UMEFANYA VIZURI SANA MUNGU AKUBARIKI TULIO MBALI TUMEWEZA KUWA PAMOJA NA FAMILIA YA KANUMBA. LAKINI KWA STAILI HIYO HIYO USIKOSE KUTUPA PART TWO TUNGE PENDA KUJUA NINI KINAENDELEA KWA MPENZI WAKE LULU. TUPE MATOKEO PALE UTAKAPO YAPATA. ASANTE NA UWE NA SIKU NJEMA KAKA.
ReplyDeleteTokea kanumba alipoanza kazi za uigizaji mpaka kuwa mcheza filamu maarufu na hatimae kututoka
ReplyDeletesipo bongo kwa muda huo wote na sijawahi kumuona kanumba wala sijawahi kuangalia sana filamu zake
naweza kusema ni filamu mbili tu ndio nimeangalia na yale mahojiano yake na ankali michuzi juu ya big brother
na mahojiano yake na mkasi salama jabir
lakini huwezi kuamini msiba wake umenigusa sana na kunichoma haswa
yote hayo yanatokana na upole na uchangamfu wake na kutokujiona na mapenzi yake kwa tanzania na watanzania wenzake
kweli nimeamini usemi usemao kizuri hakidumu na always mwenyezi mungu huwachukua wazuri mapema kabla hawajachafuka kwa ubaya ili wakapunzike maisha ya milele
mungu akulaze pema peponi steven kanumba mbele yetu nyuma yako njia ni moja kwa kila binadamu.
Thanx Ankal kwa kutuweka karibu sisi tuliombali, umetushirikisha kimatukio vizuri sana.
ReplyDeleteMimi ni mdau niko UK kifo hiki kimeniuma sana kama cha dada yangu aliyefariki ghafla miaka mingi iliyopita. Ukweli ni kwamba sifa au upendo wetu binaadamu tunaonyeshaga kwa maiti i mean mtu akisha kufa ndo tunapenda kumtolea sifa nyingi ambazo kwa bahati mbaya ni mwili tu hausikii wala hauoni.Ombi please wanadamu jamani ukimpenda mtu mwambie siku hiyo hiyo usisubiri kesho kwani kesho inawezekana akawa hasikii tena kama kaka yetu Kanumba, Laiti angejua wengi wanampenda kiasi hiki angeenda kwa Mola wake akitabasamu na kicheko chake. I wish Kanumba angeamka japo in one second aone umati wa watu walioacha kazi zao na kwenda kumuaga. Mwisho tusamehe haraka, tubebeane mizigo, tuombe kama leo tu ndo ipo kesho haipo, tusali kama tunadhambi nyingi. Kwa haya tutapata uwezo wa kutomtendea mwenzio mabaya. Please Kanumba lala salama byeeeee Kanumba sitakusahau kamwe wewe ni shujaa wa Africa
ReplyDeletePole anko MICHUZI, yaani i can imagine ni kwa kiasi gani moyo wako umejeruhiwa kutokana na msiba huu wa Steve. Nakumbuka asbh ya Jumamosi nlifungulia TBC1 na kumkuta Ahmed Salum anaripoti habari ya kifo cha Kanumba na mara nkaona mwili wake unashushwa toka kny gari yake kuingizwa mochwari, kwa kweli nliingiwa na hofu ya ajabu, nlijiona mkosaji mbele ya mwenyezi MUNGU, nkaona dunia inanielemea, sikujua nifanye nini, mwili wote uliishiwa nguvu. Lakini huo ndiyo ulikuwa ukweli KANUMBA IS GONE. Ninakuombea Mwenyezi MUNGU akupe pumziko la milele
ReplyDeletekaka michuzi na wadau wote naomba tujifunze kitu kinaitwa CPR(cardiopulmonary resuscitation)hasa hasa nyumbani TZ.ni njia mojawapo muhimu sana inaokoa vifo vya namna hii,hii itakusaidia wewe,family yako,jirani,mpita njia yaani mtu yeyote atakayekuwa karibu yako.ikibidi ifundishwe hata mashuleni
ReplyDeleteWewe Dada wa USA sisi hatu hitaji CPR wewe kama imekusaidia nursing home poa endeleza libeneke. Sisi tuna enda na mipango ya Mungu. CPR do not resascitate fanya na vibibi OK mama .
ReplyDeleteSasa wewe anny.wa saa 07.00 anataka kuelimisha kuhusu hiyo CPR au unataka kutuonyesha unaijua?
ReplyDeletePole sana kaka Michuzi kwa msiba wa rafiki yako na ndugu yetu sote. Asante pia kwa coverage hii ya tukio husika. Picha mwanana sana.
ReplyDeleteNduguyo,
Maggid Mjengwa.
Poleni sana watanzania wenzangu.Maisha ya mwanadamu ni kama maua huchanua na kunyauka.Watanzania wenzangu kuhusu wapi tutaelekea baada ya kufa Mungu ametupa fursa ya kuchagua wenyewe na sehemu ni mbili tu; pazuri(mbinguni kwenye raha ya milele)au pabaya(jehanamu kwenye mateso ya milele).Tengeneza njia yako kabla hujaondoka hapa duniani maana baada ya kifo ni hukumu inafuata hakuna kuombewa tena au marehemu kujiombea mwenyewe.Chagua uzima, njia pekee ni kuokoka(wokovu)kupitia kwa mwana pekee wa Mungu Bwana Yesu Kristo.
ReplyDeleteMm kwanza kabisa niseme kaka dikodiko au michuzi yu are number 1...kwa kubuni kitu kama hiki..sasa kaka nakuomba ulivalie njuga hili swala la mitanzania au watanzania kupenda vitu vya watu kuliko vyakwao...why nasema hivi tena kwa hasira za mbogo alie jeluhiwa...nianzie hapohapo kwenye fani ya malehemu nguli kanumba..je ni wangapi waliokua wananunua cinema zake...wengi wao walikua wakandiaji wa cinema za kibongo eti wanawaiga wa Nigeria then Leo wanajifanya wanamlilia kwangu mm huu ni unafiki mkubwa kabisa tena washindwe na walegee.miduka mingi inauza cinema za Nigeria
ReplyDeleteKama tupo abuja vile...kwenye mziki ndio kabisa...kaka nakuomba hili swala uliweke kama hoja ya haja...ni mm mdau wenu toka uk leicester...tuwe pamoja kwenye kipindi hiki kigumu...r.I.p kanumba.
WEWE MDAU UNAEKANDIA HILO SWALA LA CPR, NAONA BADO NI MUAFRIKA SANA NA UPEO WAKO WA KUONA MBELE NI FINYU! HUYO DADA ALIVYOTOA HILO WAZO NI SAWA YEYE KAOMBA KITU HICHO KIFUNDISHWE MPAKA MASHULENI SIO KUSUBIRI TU WAT WA RED CROSS NDIO WAJE WATOE HUDUMA, LAAAAA!!!
ReplyDeleteHIO INA MAANA NI HUDUMA YA KWANZA AMBAYO NI MUHIMU SANA KWA DUNIA YA HIVI SASA KWANI MUELEO WA SASA TUKO MBALI KI TEKNOLOGIA , SASA KWA NINI ASITOE WAZO? HUYO NDUGU YAKE MAREHEMU KAMA ANGEJUA KITU HICHO, KWA NAMNA FULANI AU NYINGINE LABDA ANGEWEZA KUOKOA MAISHA YA KANUMBA , JAPOKUWA KILA KITU NI MIPANGO YA ALLAAH KARIM. HATA MIMI NAPENDEKEZA IWE NI LAZIMA KILA FAMILIA KUJUA KITU HICHO NI MUHIMU SANA KWANI KUNA VIFO VINGI VINATOKEA HAPO NA MTU ANAFARIKI MBELE ZA WATU LAKINI HAKUNA MTU ANAEWEZA MSAIDIA MAJERUHI AU MTU ALIEPOTEZA FAHAMU.
HILO NI OMBI WEWE KAKA MBISHI, ANY WAY RIP BROTHER KANUMBA, KILA MTU UMAUTI UTAMKUTA NA HAKUNA ATAKAEBAKI MILELE!
INNALAAH IASHALLLA, MUNGU MUWEKE SEHEMU NZURI PEPONI, AMEEN
mdau copenhagen denmark
Watu wanalaumu kwamba kwa nini wakati wa msiba watu wawe wengi lakini wakati wa maonesho na au kusupport kazi zake hawakuwa wengi?
ReplyDeleteNi kweli, Ila lazima tujue kwamba katika maonesho yanayoendelea kila mtu atakuwa na muda wake wa kwenda kwani anajua at some time same onesho litarudiwa sehemu nyingine na ataweza kuhudhuria atakapokuwa tayari. Je, unaweza kusema kwamba "msiba wa kanumba nitaenda next time atakaporudiwa kuzikwa"?
Lakini vilevile maonesho siyo bure, ila kuhudhuria msiba ni bure. Hivyo wengi hawaendi kwenye maonesho kutokana na uwezo wao na vipaumbele vyao vya maisha na haina maana kama hawawapendi wahusika. Na je, katika hali ya kwaida mtu wa kawaida mtaani ni rahisi kumshika superstar anayelindwa na mabaunsa na kumwambia nakupenda na kazi zako? Labda ujitose kama yule jamaa aliyeingia uwanjani kumshika mkonoi Kaka wa Brazili ambao wengi walimlaumu kwamba akili zake siyo nzuri ila mimi nilmsifu kwa sababu ni mtu ambaye anaweka malengo na kuyafanyia kazi kuhakikisha yanatimia.
Kwa sababu matamasha ya wasanii wetu hayajai haimaanishi kwamba hatuwapendi. Ila ni kutokana na sababu ambazo nimezitaja pamoja na mengine.
Piga picha Justin Beaber anakuja Bongo, si ule uwanja wa Taifa unaweza kujaa hata watu wakiambiwa kiingilio cha chini zaidi ni TSH 20,000? Lakini je Diamond akitangaza kiwango cha chini 2,000 itakuwa vilevile? LAkini ni kwa sababu Diamond yupo na unaweza kuhudhuria onesho lingine. Lakini kwa vile Beaber atakuwa na onesho moja tu Bongo labda kwa maisha yake yote then kila mtu atataka kwenda.
Hivyo hata kwenye msiba wa kanumba wapenzi wake walichukulia kwamba ni mara hiyo moja tu na wote walikuja tofauti na kama ingekuwa onesho watu wa Morogoro wangesubiri pale atakapofika huko kitu ambacho hakiwezi kutokea kwa maziko mengine morogor.
Hivyo tuache huu utamaduni wa kulaumu na kuwasuta watu kuwa ni wanafiki bila kutengeneza mantiki za kuonesha hivyo.
R.I.P Kanumba.
Mdau wa Mwanza.