Mshindi wa tuzo ya Wimbo Bora wa Zouk Rhumba,Ali Kibaa akikabidhiwa tuzo yake na Mwanadada Dina Marios wa Clouds Fm na Mkongwe Rainfred Masako wa ITV.
 Muwakilishi wa kundi la Arusha Gold akipokea tuzo ya Wimbo bora wa Ragga,kutoka kwa mwanadada Khadija Mwanamboka.
 Wasanii wa Muziki wa Ragga kutoka jijini Arusha wafahamikao kwa jina la Arusha Gold wakitoa shukrani kwa wadau wao waliowapigia kura mpaka kupata ushindi huo.
 Mshindi wa tuzo ya Dancehall,Quen Darlin akiifurahia tuzo yake mara baada ya kukabidhiwa usiku huu.
 Waendeshaji wa hafla hii usiku huu ni Milard Ayoo na mwanadada Vanessa Mdee.
Burudani kutoka kwa vijawa T.H.T.
Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar usiku huu ukiwa umefurika kwa washabiki wa muziki nchini ikiwa ni siku ya utoaji wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012.
Mchekeshaji wa Ze Komedi,Mpoki akitambulisha moja kikundi ya utumbuizaji usiku huu.
Vijana wa T.H.T wakitoa burudani usiku huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Eeeeehh bwaanaa eehh!!I love the colours

    ReplyDelete
  2. Tanzania ni nchi yenye utajili wa wanasanii wenye vipaji,Mungu katubariki kwa amani,upendo na vipaji,huu ndio urithi wetu,
    Mungu Ibariki Tanzania
    Mungu Ibariki Afrika
    wadau
    Ngoma Africa Band aka FFU

    ReplyDelete
  3. I love THT styles

    ReplyDelete
  4. Jamani huyo Quen Darlin vipi? Anapatikana kwa simu au e-mail gani, maana ana mvuto wa haja. Na je, kaolewa? Kama bado tafadhali aweke hadharani namba zake ili tuanze kuwajibika! Mwacheni Mungu aitwe Mungu!

    ReplyDelete
  5. Inakuwaje Lady Jay Dee anashinda kila mwaka???? Ina maana hakuna vipaji vingine kila mwaka??? Kwani Jay Dee amefanya kitu gani mwaka huu ambao alikuwa ufaransa na south africa muda mrefu na mpaka sasa yuko huko bila kutoa hata single moja kilichomfanya ashinde hiyo award ya mwibaji bora wa kike? Lazima kuna upendeleo sana!!! NI AIBU KUBWA!

    ReplyDelete
  6. Wewe mtoa maoni wa Apr 15, 03:15 PM vipi? Una ugomvi na Lady Jaydee? Ataendelea kuwa mwimbaji bora tu, mpaka apatikane binti atakayekuwa juu yake kiuimbaji. Hata asipotoa 'single' kwa miaka 10 mfululizo. Hii ni rekodi, kama ilivyo ktk ukimbiaji ambako rekodi inaweza kudumu hata kwa miaka 50 mpaka apatikane mtu wa kuipiku. Saa Jaydee bado ni kijogoo. Mwenye wivu na ajinyonge!!!

    ReplyDelete
  7. Tz bado hakuna binti anayemfikia kama jay dee, acha majungu apr 15, 03:15 PM! Angalia tunzi zake,sauti yale na video zake utaona hawa kina linah,shaa,na wengine wote wanaruka ruka tu..kipaji ZERO.

    ReplyDelete
  8. Dah, Kaka ee,

    Eee bwana huyo KWIN DALIN na huyo DADAKE ALIKIBA naweza kupataje kontakts zao?

    Duh!

    ReplyDelete
  9. Vp anonymous wa hapo juu unaugomvi na lady jaydee nini??? sasa wewe kwa akili yako kuna mwana dada gan ambae anaweza kumpiku lady jaydee tanzania nzima???? acha wivu jamaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...